Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Business as usual,sijaona Cha maana,zaidi ya watu kupata ulaji tu,
Katanga amekosea nini?kutoka kuwa katibu mkuu kiongozi(mkuu wa wa watumishi wote serikali kuu) kwenda kuwa balozi tu!!!
Diwani ameulamba,
Hoyce Temu vipi,na madudu yake Bado hajatumbuliwa tu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za ziongozi Serikalini Ikulu jijini Dares Salaam, leo tarehe 03 Januari, 2023.

Amesema Mwezi Novemba 2022 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa na mjadala mzito kuhusu matumizi ya fedha na madaraka katika ofisi za kibalozi zilizoko nchi mbali ulimwenguni. Kutokana na hilo serikali inafanyia kazi kasoro zilizoletwa ili kurudisha hadhi za balozi zetu.

Mabadiliko hayo ni;
Mabadiliko katika Ofisi ya Ubalozi New York ambayo inakuwa na mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Taifa.

Hussein Othamn Katanga anachukua nafasi ya Prof. Kennedy Gaston ambaye anarudi Tanzania. Hussein Othman Katanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi na aliwahi pia kuwa Balozi nchini Japan.



Sawa tu, ila mabadiliko kwenye idara ya usalama hautukuzoea yawe mara kwa mara, kulikoni miaka ya karibuni?
 
Back
Top Bottom