Rais Samia awabadili nafasi Mawaziri wa Wizara ya Utalii na Maliasili na Wizara ya Utamaduni na Michezo

Rais Samia awabadili nafasi Mawaziri wa Wizara ya Utalii na Maliasili na Wizara ya Utamaduni na Michezo

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii

Aidha, Balozi Dkt. Pindi Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amehamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas Said, amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii

Dkt. Hassan Abbas anachukua nafasi ya Prof. Eliamani M. Sedoyeka

Aidha, Rais Samia amemteua Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas

EF9A7D0D-435B-457D-9FBA-B3B673E99CC9.jpeg

12F9FB61-47D5-434A-9D52-45691F95299A.jpeg
 
Profesa Sedoyeka alikuwa mkufunzi na mkuu wa chuo pale Arusha (AIA) juzi juzi akateuliwa kuwa katibu mkuu maliasili na utalii na kuupiga chini ukufunzi, leo ametumbuliwa! Sasa sijui atarejea kwenye ukufunzi au atakaa benchi kungojea vyeo vya dezo, uchawa na kujipendekeza kutoka kwa rais!

Ni fedheha sana.
 
Ila Samia kuna muda unakera sana. Mkwe wako unambeba utakavyo. Said Yakubu mwizi mkubwa akiwa msaidizi wa Ndugai Bungeni leo anakuwa KM. Achana na akina Othman wanakupoteza unarudia makosa ya JPM.
 
Back
Top Bottom