Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika tuna Rais wa nguvu, Rais wa viwango vya nyota tano, Rais mzalendo, msema kweli, wa kujivunia, mwenye misimamo, kujiamini, na ufahamu wa masuala mbalimbali. Watanzania tuna Rais anayewajua vyema na kwa undani wasaidizi wake na kutambua nani anafaa wapi.
Watanzania tuna kila sababu ya kutembea vifua mbele. Binafsi najivunia sana na kujiona fahari kuongozwa na Rais Samia. Huyu Rais wetu ni mtu wa kipekee, kiongozi kwelikweli, ni jembe haswa, chuma cha reli, mama wa shoka na jasiri. Ni mama imara, hodari na madhubuti. Ni raha na furaha sana kuwa na Mama yetu Ikulu.
Nimeshuhudia Watanzania wakiwa na furaha kubwa sana baada ya kusikia maneno ya uzalendo na yenye kugusa hisia zao. Mama yetu ameongea kwa hisia kali sana na uchungu mkubwa leo hii. Kama tungepata uwezo wa kuonyeshwa moyo wa Rais wetu leo hii, nchi nzima ingebubujikwa kwa machozi ya furaha na huruma kwa Rais wetu.
Rais wetu ameongea kwa hisia kali sana toka ndani ya moyo wake, alipokuwa anawaambia na kuwakumbusha viongozi wote kuwa uongozi ni dhamana na utumishi kwa watu. Na kila kiongozi anatakiwa kutambua kuwa uongozi unatoka kwa Mungu.
Maneno haya ni mazito sana ndugu zangu. Mama yetu mpendwa alikuwa anawakumbusha wateule wake kuwa vyeo walivyonavyo na walivyopewa ni kwa neema tu ya Mwenyezi Mungu na siyo kwa uwezo wao au kuwa na akili kupita wote wasio na vyeo.
Hata mimi napenda kusema kuwa ukiteuliwa na Mheshimiwa Rais ni heshima kubwa sana na neema ya Mungu aliyekupatia kibali hicho. Jiulize leo hii wewe ni Waziri, Mkurugenzi wa Halmashauri, DC, RC, DAS, au RAS. Jiulize imekuwaje wewe tu ndio ukapata nafasi hiyo kati ya mamilioni ya Watanzania?
Kwanini uwe wewe? Kwanini upate uteuzi wewe tu? Kwanini waachwe wengine upate wewe? Kwanini wewe tena umepata saini ya Mheshimiwa Rais? Kwanini watu wamesoma na wana elimu zao lakini wapo mitaani wakifanya kazi za vibarua kwa ujira mdogo huku wakiwa na vyeti vyao majumbani mwao, lakini wewe ukapata uteuzi?
Jiulize umesoma na wangapi? Kwanini umeinuliwa wewe na kuachwa wengine au wenzako? Wangapi wanatamani wangepata uteuzi wa Mheshimiwa Rais lakini hawajawahi kupata au hata kufikiriwa? Jiulize kwanini wewe tu umepata na umeendelea kupata? Umempa nini Mungu? Tumbo lililokubeba lina utofauti gani na matumbo ya wanawake wengine?
Ukijiuliza maswali haya utagundua kuwa ni kwa neema tu ya Mwenyezi Mungu ndio maana umepata heshima hiyo ya kupata uteuzi na kuaminiwa na Mheshimiwa Rais. Umepewa nafasi ya kuwatumikia Watanzania waliobaki nyuma ili wainuke. Ni fursa ya kipekee uliyopewa na Mungu kugusa maisha ya watu, kuwafuta machozi na kuwapa tabasamu na matumaini kupitia wewe.
Hivyo jitahidi kuwa mwenye huruma, upendo, ukarimu, unyenyekevu, na muungwana kwa watu. Jitahidi kuwatendea watu haki, kuwa na hofu ya Mungu. Usiwe mtu mwenye kiburi, dharau, kejeli, roho mbaya, visasi na moyo wa kuwakomoa watu pasipo sababu. Acha majivuno ndugu yangu, acha kiburi. Vyeo ni vya kupita tu. Leo upo hapo lakini kesho hupo. Acha alama njema za kukumbukwa na watu hata usipokuwepo kesho.
Naomba mniruhusu niweke kalamu chini ili nisiwachoshe maana kichwa changu kimejaa mambo mengi sana ambayo nikisema niandike yote sitaweza kumaliza.
Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama anatosha kuendelea kuliongoza taifa letu kwa muhula wa pili.