Pre GE2025 Rais Samia awalipua watu kwa shangwe, nderemo na vifijo mitaani baada ya kuwahakikishia kuwepo Madarakani hadi 2030

Pre GE2025 Rais Samia awalipua watu kwa shangwe, nderemo na vifijo mitaani baada ya kuwahakikishia kuwepo Madarakani hadi 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Mitaani ni shangwe, nderemo, vifijo , chereko chereko,furaha,hoihoi na tabasamu tupu kwa wananchi mbalimbali. Hii ni baada ya Rais Samia kukata kiu ya mamilioni ya watanzania waliyokuwa nayo mioyoni mwao. Kiu ya kutaka kuona Rais Samia akiendelea na muhula wa pili wa Urais kwa kuchukua ,kujaza na kurejesha Fomu ya Urais.

Shangwe hiyo imekuja baada ya Rais Samia kutamka hadharani kuwa anataka kuacha alama katika uongozi wake atakapokuwa anajiandaa kurejea Nyumbani Kizimkazi na kuja kuwahoji walipofikia kimafanikio na kimaendeleo katika Masuala Mazima ya ushirika na ugani.

Kauli ya kusema kuwa atakapo Kuwa anajiandaa kurejea Kizimkazi miaka hiyo ya mwishoni kuelekea 2030.imemaanisha kuwa Rais wetu Mpendwa amekubali Ombi na Maombi ya Mamilioni ya watanzania wa makundi mbalimbali waliohitaji kuona akiendelea kuwa Rais Wetu.

Ndio maana makundi kama Walimu walikuwa wamemchangia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuchukulia Fomu ya Urais.pia wahandisi nao pia walikuwa wamechanga mamilioni ya pesa kwa ajili ya kumpatia Usafiri wa helikopta atakayo kuwa anaruka nayo angani na kuteka anga lote la Tanzania kikomandoo wakati wa kampeni,huku bendera ya kijani ikipepea angani.

Kwa hakika Rais Samia ameleta furaha kubwa sana hapa Nchini kwa kauli yake hiyo.ikumbukwe ya kuwa mamilioni ya watanzania chaguo lao ni Rais Samia tuu hapo Mwakani. Watu wengi sana walikuwa wamesema kuwa wanahitaji kuona CCM ikimpatia Rais Samia ugombea Urais.jambo ambalo hata hivyo CCM kupitia viongozi wake ilijibu kwa kusema kuwa Ni Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mpaka 2030.

Kwa hakika Rais Samia ndiye ameshikilia Furaha ya Mamilioni ya watanzania.kama Ingetokea akakataa ombi la watanzania,kwa hakika angewakatisha sana tamaa na kuwavunja moyo mamilioni ya watanzania ambao kwa sasa wamejaa matumaini tele na uhakika wa kutimiza ndoto zao.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Uchaguzi wa 2025 umekwisha anaandaliwa Mzalendo Kafulila kuelekea 2030 ni bandika bandia

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Taifa kwa Kauli Moja na Sauti Moja ya kishindoo limeamua kuwa Mwakani ni Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu hadi 2030. Mheshimiwa Kafulila Mungu amsaidie ili aingie Bungeni hapo Mwakani.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mitaani ni shangwe ,nderemo,vifijo , chereko chereko,furaha ,hoihoi na tabasamu tupu kwa wananchi mbalimbali. Hii ni baada ya Rais Samia kukata kiu ya mamilioni ya watanzania waliyokuwa nayo mioyoni mwao. Kiu ya kutaka kuona Rais Samia akiendelea na muhula wa pili wa Urais kwa kuchukua ,kujaza na kurejesha Fomu ya Urais.

Shangwe hiyo imekuja baada ya Rais Samia kutamka kuwa anataka kuacha alama katika uongozi wake atakapokuwa anajiandaa kurejea Kizimkazi na kuja kuwahoji walipofikia kimafanikio kimaendeleo katika Masuala Mazima ya ushirika na ugani.

Kauli ya kusema kuwa atakapo Kuwa anajiandaa kurejea Kizimkazi miaka hiyo ya mwishoni kuelekea 2030.imemaamisha kuwa Rais wetu Mpendwa amekubali Ombi na Maombi ya Mamilioni ya watanzania wa makundi mbalimbali waliohitaji kuona akiendelea kuwa Rais Wetu.

Ndio maana makundi kama Walimu walikuwa wamemchangia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuchukulia Fomu ya Urais.pia wahandisi nao pia walikuwa wamechanga mamilioni ya pesa kwa ajili ya kumpatia Usafiri wa helikopta atakayo kuwa anaruka nayo angani na kuteka anga lote la Tanzania kikomandoo wakati wa kampeni,huku bendera ya kijani ikipepea angani.

Kwa hakika Rais Samia ameleta furaha kubwa sana hapa Nchini kwa kauli yake hiyo.ikumbukwe ya kuwa mamilioni ya watanzania chaguo lao ni Rais Samia hapo Mwakani. Watu wengi sana walikuwa wamesema kuwa wanahitaji kuona CCM ikimpatia Rais Samia ugombea Urais.jambo ambalo hata hivyo CCM kupitia viongozi wake ilijibu kwa kusema kiwa Ni Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mpaka 2030.

Kwa hakika Rais Samia ndiye ameshikilia Furaha ya Mamilioni ya watanzania.kama Ingetokea akakataa ombi la watanzania,kwa hakika angewakatisha sana tamaa na kuwavunja moyo mamilioni ya watanzania ambao kwa sasa wamejaa matumaini tele na uhakika wa kutimiza ndoto zao.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Samia miaka mia

#2025-2030
 
Back
Top Bottom