Pre GE2025 Rais Samia awalipua watu kwa shangwe, nderemo na vifijo mitaani baada ya kuwahakikishia kuwepo Madarakani hadi 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi uchaguzi wa mwakani umeshafanyika na Tume huru imeshahesabu kura na kuyatangaza matokeo yake??

Iweje huyu Lucas Mwashambwa atangaze kuwa Rais Samia ataendeoea katika kiti chake hicho Hadi mwaka 2030!

Hivi sasa ndiyo tunalazimika kuyaamini maneno ya Nape, kuwa katika nchi hii, haitegemei kura zinazopigwa Kwenye maboksi, Bali inategemea nani anayehesabu na kutangaza kura hizo!
 
Kamuulize Magufuli alikuwa na matarajio yapi na sasa yuko wapi
 
Hata Jiwe kuna waimba pambio alikua akiwakosoa hadharani kwa aibu....

Nakuhakikishia hata Samia akisoma huu ujinga wako anasikia kinyaa....
 
Sasa kama kweli una akili Timamu na unajitambua vyema ,unaona ni nani anayeweza kushindana na Rais Samia katika sanduku la kura? Ni nani mwenye ubavu au ushawishi wa kuweza kupata kura hata laki tano tu?
 
Hata Jiwe kuna waimba pambio alikua akiwakosoa hadharani kwa aibu....

Nakuhakikishia hata Samia akisoma huu ujinga wako anasikia kinyaa....
Kauli na jibu ni moja tu kuwa ni Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan hadi mwaka 2030.
 
Eti "Kuripua" acha kuharibu lugha wewe chawa ni " Kulipua".

Halafu labda ailipue nchi kwa ufisadi uliotamalaki huku yeye akiwa anajiita ni chura kiziwi.

Mafisadi na majizi yaliyotajwa kwenye ripoti ya CAG yanapeta huko mitaani na hakuna hatua yoyote wamechukuliwa.

Kagawa bandari na mbuga zetu kwa waarabu huko ndio kulipua nchi kwa shangwe chawa?
 
hilo halina ubishi.
kura yangu ni kwa dkt Mama Samia tu, sina mwengine.
Mama mchapa kazi, mwadilifu asiye majivuno, mnyenyekevu asiye lewa madaraka.
 
Taifa kwa Kauli Moja na Sauti Moja ya kishindoo limeamua kuwa Mwakani ni Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu hadi 2030. Mheshimiwa Kafulila Mungu amsaidie ili aingie Bungeni hapo Mwakani.
Kwa kauli yako hiyo, mbunge wa jimbo lake wa sasa mwanaCCM mwenzenu Mungu asimsaidie kama mama nae afike 2030.
 
Kuna Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…