Tukio liko mubashara TBC.
Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
RIP Kwandikwa
======
View attachment 1882693
View attachment 1882692
View attachment 1882668
Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza shughuli ya Kuaga mwili wa Waziri wa Ulinzi na JKT, John Kwandikwa, leo tarehe 6 Agosti, 2021
Kinachoendelea kwasasa ni katibu mkuu kusoma wasifu wa Kwandikwa ambae kitaaluma ni mkaguzi wa hesabu na kufanya kazi ofisi ya mkaguzi mkuu wa Serikali kwa muda mrefu na kumaliza na cheo cha mhasibu mkuu kwenye ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali mwaka 2015. Mwaka 2017 akateuliwa kuwa naibu waziri wa iliyokuwa wizara ya Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano sekta ya ujenzi.
December 2020 aliteuliwa kuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, nafasi aliyohudumu mpaka umauti unamfika
Mussa Azzan Zungu – M/kiti Kamati ya Kudumu ya Bunge -Ulinzi na Usalama
Amehudumu kachukua mda mfupi sana kufanya kazi na kamati. Katika kipindi kifupi alichofanya, alikuja siku akaniomba: Mwenyekiti nisaidie, mimi mgeni kwenye hizi shughuli.
Tukamwambia, ili mradi Mwenyezi Mungu amekuteua, atakutia maneno na utaweza kufanya kazi hii.
Kuandikwa alikuwa ni mtu ambaye alikuwa tayari kujifundisha na alikuwa tayari kuona na kujua umuhimu wa vyombo hivi vya ulinzi.
Jen. Venance Mabeyo – Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
Upekee wa kwanza wa marehemu ni upole wake, usikivu wake na unyenyekevu wake.
Pamoja na upole huo, alikuwa ni kiongozi mchapakazi aliyependa kujifunza kutoka kwa wafanyakazi wenzake
Kitaaluma alikuwa Mhasibu, lakini kwa moyo wake wa kupenda kujibunza alijifunza masuala mengi ya kijeshi nakuonesha ubobevu katika masuala yake
Hakupenda kutumia muda mwingi ofisini. Alitumia muda mwingi kuwatembelea Maafisa na Askiari katika maeneo yao ya kazi ili aweze kujionea hali halisi ya zana, vifaa, mazingira ya kufanyia kazi na ustawi wa wanajeshi.
Mfano wa hili ni pale alipoamua kutembelea makao makuu ya Kamandi zote – Jeshi la Nchi Kavu, Jeshi la Anga na Jeshi la Wanamaji -- siku chache baada ya uteuzi wake ikiwa ni kwa nia hiyo hiyo ya kujionea hali halisi badala ya kusubiri kupelekewa taarifa ofisini.
Tulia Ackson -- Naibu Spika wa Bunge
Asema Kwandikwa kama mtu mwema ambao pia umeshuhudiwa na viongozi mbalimbali ikiwemo yeye ambae ameshawahi kufanya nae kazi na kumtaka kila mmoja kutenda wema ili siku yake ikifika utaambatana nae kama neno la Mungu linavyosema.
Kasssim Majaliwa -- Waziri Mkuu wa JMT
Amemtaja Kwandikwa kama mtu aliyekuwa anatoa ushirikiano na ametoa pole kwa Familia, Rais na wanaushetu. Kassim Majaliwa amemuombea alazwe mahala pema peponi.
Hussein Ali Mwinyi – Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Alikuwa Waziri wa kwanza kuja kunitembelea kule Zanzibar baada ya kuteuliwa akiwa Waziri wa Ulinzi kwa ajili ya kuzungumzia suala zima la Ulinzi na Usalama wa nchi yetu.
Nitamkumbuka sana kwa ucheshi, ukarimu, nidhamu na hulka njema alizokuwa nazo.
- Amesema wote wamegubigwa na majonzi na kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar anato pole kwa familia na Rais wa JMT, wananchi wa Ushetu.
- Anasema Taifa limeondokewa na Msomi mahiri na anamkumbuka kama waziri wa kwanza wa JMT kwenda kumtembelea Zanzibar na kuzungumzia usalama wa Nchi.
Samia Suluhu Hassan – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Binafsi katika ngazi tofauti nilimjua Kuandikwa.
Alishiriki katika ziara tulizofanya mikoa mitatu: Singida, Tabora na Shinyanga. Katika ziara hiyo alikuwa mfuatiliaji mtulivu, makini, msikivu na asiye na makuu. Hakuwahi kutoa sababu ya kutoka nje ya ziara mpaka tunamaliza.
Hizi ni baadhi ya Sifa zilizotusukuma mimi na Marehemu Magufuli kumpa dahamana ya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi mwaka 2017 na baadaye Waziri wa U na JKT mwaka 2020.
Sifa hizohizo ndiyo zilizonipa sababu ya kuendelea kumuamini kuendelea kuendesha wizara nyeti ya Ulinzi na JKT.
Nilipata taarifa nikiwa Rwanda pamoja na Rais Kagame na ametuma salamu za rambirambi kwa Watanzania.