Rais Samia awapa shavu Wazanzibar: Ajira asilimia 21 za Muungano kuwa za Wazanzibar

Nyerere aligive up rights nyingi za Tanganyika ili kuwatongoza Wazanzibar na kuwavuta ili nao wagive up zao halafu mdogomdogo tuunde serikali moja, Ila Wazanzibar wajanja, wakastuka, wakagoma kuachia chao, na wakaendelea kudai kingi zaidi ndani ya muungano. Matokeo yake Watanganyika wapowapo tu kama kondoo asiye na mchungaji, na kilicho chao kinaliwa na mzanzibar free, wakati cha Mzanzibar kinaliwa na mzanzibar Mwenyewe.

Watanganyika tukubali, licha ya kupeleka majeshi kule, kuwasimikia viongozi lakini hakuna kitu chochote tangible tunachokipata kule, Ila Wazanzibar wananufaika sana na stahiki za Tanganyika zisizo za muungano.

Juzi Samia kakopa Trillion 1.3 IMF, kawamwagia Wazenji zaidi ya Sh bilion 230, about 25% ya pesa zote. Guess nani atalipa hizi, Ni Watanganyika na Wazanzibari lakini zinaenda kutumika huko Zenji kwenye SMZ ambayo si serikali ya muungano.

Na 75% zilizobaki zitatumika kwenye mambo ya muungano ambayo ni yetu sote na pia zitatumika kwenye mambo yasiyo ya muungano ambayo nayo pia wazanzibar bado ni wanufaika maana hawazuiwi popote kuenjoy matunda ya mambo yasiyo ya muungano ikiwemo ajira kwenye masuala hayo!

Sasa baada ya mkopo huo, tunaambiwa na ajira eti 21% ziwe Wazanzibar

Watanganyika tumeliwa!
 
Mkuu, kwa uhalisia wake wote huu muundo wa muungano wetu ni kwa manufaa ya CCM ili kulinda historia ya waasisi wake hasa Mwl. Nyerere. Labda ulifaa kwa mazingira ya kisiasa na kiusalama kwa nyakati za uwepo wa uhasama uliokuwepo kati ya "Eastern & Western blocks'

Kwa nyakati tulizopo, muundo wa muungano wetu ni kero kubwa kwa Watanganyika na Wazanzibari. Kama watawala hawakubaliani na suala, basi waitishe "referendum" itakayobaini ukweli. Ambayo itakayosimamiwa na tume huru itakayoundwa na jopo la majaji kutoka pande mbili za muungano.
 
Nadhani Watanganyika tunapaswa sasa tujitafakari upya .Hii si Saw a,
 
Duuh!
Watanganyika wanapigwa kotekote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…