Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyerere aligive up rights nyingi za Tanganyika ili kuwatongoza Wazanzibar na kuwavuta ili nao wagive up zao halafu mdogomdogo tuunde serikali moja, Ila Wazanzibar wajanja, wakastuka, wakagoma kuachia chao, na wakaendelea kudai kingi zaidi ndani ya muungano. Matokeo yake Watanganyika wapowapo tu kama kondoo asiye na mchungaji, na kilicho chao kinaliwa na mzanzibar free, wakati cha Mzanzibar kinaliwa na mzanzibar Mwenyewe.Hayo ni matokeo yenye utata ya muungano wa vitu viwili wenye kuleta vitu viwili badala ya kimoja. Hili si jambo la kawaida.
Nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar zilipoungana zilileta nchi moja utambulizi kama JMT, lakini cha ajabu ni kwamba Tanganyika ilimezwa na kupoteza hadhi yake yote ya utambulizi wake wa awali kama nchi, lakini kwa upande wa Zanzibar yenyewe ilibakia na hadhi yake na kutambulika kama nchi iliyo ndani ya muungano.
Mtetezi wa Tanganyika ndani ya JMT atakuwa ni nani, nchi ambayo haipo na hata siku ya uhuru haiadhimishwi kwa kulitambua jina lake la asili. Rais wa jmt anatoka upande wa Zanzibar, kwa upande huo yupo Rais wake ambaye anatetea maslahi ya Wazanzibari. Je! Kwa upande wa Tanganyika ni kiongozi gani anayetambulika kikatiba mwenye uwezo wa kutetea maslahi ya mama Tanganyika? Si Makamu wa Rais wala Waziri Mkuu mwenye uwezo wa kufanya hivyo, kwa kuwa wao ni wateule na wasaidizi wa Rais wa JMT.
Mkuu, kwa uhalisia wake wote huu muundo wa muungano wetu ni kwa manufaa ya CCM ili kulinda historia ya waasisi wake hasa Mwl. Nyerere. Labda ulifaa kwa mazingira ya kisiasa na kiusalama kwa nyakati za uwepo wa uhasama uliokuwepo kati ya "Eastern & Western blocks'Nyerere aligive up rights nyingi za Tanganyika ili kuwatongoza Wazanzibar na kuwavuta ili nao wagive up zao halafu mdogomdogo tuunde serikali moja, Ila Wazanzibar wajanja, wakastuka, wakagoma kuachia chao, na wakaendelea kudai kingi zaidi nsani ya muungano. Matokeo yake Watanganyika wapowapo, na kilicho chao kinaliwa na mzanzibar free, wakati cha Mzanzibar kinaliwa na mzanzibar Mwenyewe.
Watanganyika tukubali, licha ya kupeleka majeshi kule, kuwasimikia viongozi lakini hakuna kitu chochote tangible tunachokipata kule, Ila Wazanzibar wananufaika sana na stahiki za Tanganyika zisizo za muungano.
Juzi Samia kakopa Trillion 1.3 IMF, kawamwagia Wazenji zaidi ya Sh bilion 230, about 25% ya pesa zote. Guess nani atalipa hizi, Ni Watanganyika na Wazanzi ar na zinaenda kutumika huko kwrnye SMZ ambayo si serikali ya muungano.
Na 75% zilizobaki ziratumika kwenye mambo ya muungano ambayo ni yetu sote na pia zitatumika kwenye mambo yasiyo ya muungano ambayo wazanzibar bado nao ni wanufaika maana hawazuiwi popote kuenjoy mambo yasiyo ya muungano ikiwemo ajira kwenye mambo hayo!
Sasa baada ya mkopo huo, tunaambiwa na ajira eti 21% ziwe Wazanzibar
Watanganyika tumeliwa!
Nadhani Watanganyika tunapaswa sasa tujitafakari upya .Hii si Saw a,View attachment 2015004
Watu milioni 58 wanagombania asililia 79 ya Ajira
Ila watu milioni 1.5 unawapa asilimia 21 ya Ajira
Hongera mama, Charity begins at home.
Watanganyika huu ni muda wa kukaa na kutafakari huu muungano una faida na sisi au la?
Hebu tazama
1. Mzanzibar ana haki ya ardhi yote ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ila wewe Mtanganyika huko Zanzibar unaweza kupata ardhi kwa masharti ya wageni
2. Mzanzibar anahaki na Ajira zote za mambo hata yasiyo ya muungano kwa mfano TAMISEMI
3. Mzanzibar anaweza kushika nafasi yoyote ya uongozi huku Tanganyika hata kwa mambo yasiyo ya muungano kwa mfano balozi wa nyumba kumikumi lakini Mtanganyika hawezi kuwa kiongozi wa shehia kule Zanzibar
4. Ajira zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni exclusive kwa ajili ya Wazanzibar, Yaani Wao wanakula kotekote Tanganyika na kule Zanzibar
5. Wao wamepambana kuondoa mafuta kwenye mambo ya muungano, lakini sisi Ardhi yetu wanaitaka, na wanaienjoy sana tu kwa sababu nawajua Wazanzibar wanaomiliki ardhi TZ
Sasa katika hali kama hii, Huu muungano una faida kwa Watanganyika kweli?
Duuh!View attachment 2015004