Rais samia awapa supu washiriki baada ya mwenge vijana marathon

Rais samia awapa supu washiriki baada ya mwenge vijana marathon

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Vijana walioshiriki Mwenge Vijana Marathon leo asubuhi katika Manispaa ya Sumbawanga wamepata fursa ya kupata supu iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hatua iliyopokelewa kwa shukrani na washiriki hao.

Akizungumza baada ya mbio hizo zilizoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Mhe. Dkt. Joel Arthur Nanauka, Waziri ameeleza namna Serikali inavyoendelea kuweka mazingira ya kuwawezesha vijana kiuchumi, ikiwemo kupitia mikopo isiyo na riba.

Baadhi ya washiriki wamemshukuru Rais kwa supu waliyopewa na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kufungua fursa mbalimbali za maendeleo kwa vijana.


 
Kuna balabala moja hivi ya 1km inazinduliwa na mwenge... 😂 Na ni mbovu, hii nchi hiii
 
Back
Top Bottom