Rais Samia awatumbua Wakurugenzi wa Halmashauri wanne kwa ubadhirifu wa Fedha zikiwemo za UVIKO-19

Pongezi kwa Rais wetu kwa kuwa makini katika usimamizi wa fedha za serikali ,lakini pia naomba hao wahusika wafikishwe mbele ya sheria ili kuwajibika kwa walichokifanya.
#kaziiendelee
Siyo rahisi mtu kula pesa ya umma sema huyu mtu wenu ni mdini sn
 
Yupo mkuu wa Shule X akishirikiana na SlO wa zamani wametafuna pesa kisha mkuu wa Shule X kahamishwa Pia na mratibu wa kata W iliopo kijiji shells nae kahamishwa.lakini wote hao hawakukabidhi miradi
Ili akatafune kwingine. Mama kama kweli ameamua kufukunyua haya ya ujenzi wa madarasa ya COVID, basi mnyororo wa wawajibishwa ni mrefu.
 



 
Hao Ndiyo Walioshindwa Kula Kwa Urefu Wa Kama Ama Wavimbiwa Wakaanza Kutoa HewA
 
Moja ya nukuu maarufu ulimwenguni ni ile ya Mwanafalsafa Edmund Burke inayokemea watu wema kutochukua hatua pale maovu yanaposhamiri. Hali huwa tofauti Taifa linapoongozwa na kiongozi mwenye uadilifu.

Juma hili, Rais Samia akiwa ziarani kanda ya Ziwa alitangaza utenguzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo na upotevu wa mapato katika halmashauri hizo.

Rais Samia amekuwa akisisitiza umuhimu wa viongozi na watendaji kujiepusha na matumizi mabaya ya ofisi. Wakurugenzi wote waliotenguliwa ikawe funzo kwa watendaji wasio waadilifu kubadilika na kuelewa falsafa ya Rais Samia.

Kama mwananchi na mlipa kodi ninatoa pongezi za dhati kwa uthubutu na ukali wa Rais kwa watendaji wazembe, Rais wetu endelea kuwashughulikia watendaji wote wazembe wasioendana na kasi yako inayolenga kuleta ustawi kwa nchi yetu.

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
 
Akimalizana na wakurugenzi aje atusafishie Tanesco na makamba wake.
 
Ktk hao wanne kuna wasukuma watatu kasoro lubuva tu kweli ukabila na udini hautoisha africa.sukuma gang inapotezwa mdogo mdogo mpaka sasa score inasoma sa100 3 **** gang 0
 
Upo Mkuu😎
 
Mpaka siku wakianza kufukuzwa kazi, kufilisiwa na kupelekwa mahakamani immediately ndio huu mchezo utaisha. Otherwise wataendelea kuchukua risk ya kutuibia kila siku. Kutumbuliwa haiwezi kuwa shida kamą una mzigo wa pesa ya kufanya maisha mengine.
 
Hao kosa lao itakuwa wamekula wakavimbiwa, Rais hapendi hilo anataka ule kwa kiasi.

Huyo mkurugenzi wa Iringa sio yule alieshutumiwa kwa ubakaji siku chache zilizopita? kama ndie akapumzike tu, yeye alikuwa hachagui vyakula anabugia chochote.
Yule ni mzee bhana anaanzaje kubaka, kama sijakosea ni zaidi 65yrs
 
Wezi wa kuku wako magereza wakisota, nakumbuka kuna mtu alifungwa miaka huko morogoro kwa kukutwa na maini ya swala, lakini wakurugenzi wakiiba mamilioni wanatumbuliwa halafu inashia hivo.
 
 

Attachments

  • E7840291-380C-47B3-9D3D-6DBA3CF48099.jpeg
    617.6 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…