Rais Samia awatunuku kamisheni maafisa wanafunzi kundi la 04/29 bms na kundi la 70/22 regular Chuo cha Maafisa cha Kijeshi Monduli

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwatunuku kamisheni maafisa wanafunzi kundi la 04/29 bms na kundi la 70/22 regular chuo cha maafisa cha kijeshi, Monduli mkoani Arusha leo tarehe 18 Novemba, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/21P0ou6g_Zg?si=sYJGE53fEu5KKbRP

Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 04/ 20 Shahada ya Sayansi ya Kijeshi ya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA), Monduli Mkoani Arusha, wakiwa kwenye Mahafali ya nne, tarehe 18 Novemba 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Maafisa wanafunzi Kundi la 04/20- Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na Kundi la 70/22 (Regular) mara baada ya Kuwatunuku Kamisheni katika Sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA), Monduli, Mkoani Arusha.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Tanzania (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba wakati wa Sherehe za Kutunuku Kamisheni Chuoni hapo Mkoani Arusha, tarehe 18 Novemba 2023.
 
Watoto pendwa hao kuliko sisi wafukuza magendo na wavumilia matusi ya lissu!
Lisu anashindwa kumtukana mwenyekiti wake anaemdhalilisha majukwaani kama hapo pichani. Yeye anamtukana raisi alieenda kumjulia hali hospital ya Kenya pindi amepigwa risasi, na pia kumsaidia kupata haki yake iliyokuwa imezuiwa na kina Ndugai.

Ama kweli fanya mema uende zako.
 

Attachments

  • IMG-20230520-WA0008.jpg
    109.8 KB · Views: 18
Hapo Bado hujaona vichekesho, unakuta mwanajeshi amejiunga na jeshi hajawahi pigana vita, lakini akistaafu au kufariki wanamsifia kwa utumishi uliotukuka!
Tatizo kila idara ndani ya nchi hii ni siasa tupu
 
Wanajeshi waastaafu njooni mniambie nin maana ya kamisheni

Je Ni degree ya sayansi ya kijeshi au Ni umahiri wa maswla ya kijeshi

Sifa za kupewa kamisheni ni zipi

Nawasilisha
 
Hakumshukuru mbowe aliyempa nafasi ya kuwa maarufu yule hajui kushukuru!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…