Rais Samia aweka rekodi ya Dunia. Aongeza Fedha za miradi ya maendeleo kutoka Trilioni 5.91 Mwaka 2015 Hadi Kufikia Trilioni 15.4 Mwaka 2024

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Ukiona vyaelea Ujue Vimeundwa ,ukiona miradi ya maendeleo inachipua na kumalizika kwa uharaka ,ufanisi na kwa kupendeza ujue juu yake kuna mikono ya Rais Samia ,ukiona Bwawa la Mwalimu Nyerere lililoachwa likiwa 34% limekamilika kwa uharaka na kwa ubora wa 100% ujue ya kuwa kuna mkono wa Mama wa shoka ,jasiri muongoza njia, simba wa nyika,shujaa wa Afrika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ambao umewekwa juu yake..

Ukiona leo hii watanzania kwa furaha na tabasamu wanasafiri katika treni ya Umeme kupitia SGR kutoka Dar hadi Dodoma huku wakila kiyoyozi na hewa safi ya oksijeni. ni lazima ujue hiyo ni kazi njema na tukuka ya Mheshimiwa Rais Samia Mama yetu Mpendwa. Ukiona ujenzi wa shule bora za kisasa na za ghorofa zinajengwa kila sehemu,miradi ya afya kama vile vituo vya afya,miradi ya maji safi na salama inasambazwa mpaka vitongojini huko ni lazima ufahamu ni ujasiri wa kimaamuzi uliofanywa na Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Ipo hivi hayo yoote na mengine mengi yamewezekana na kuona miradi kila kona ya nchi yetu kwa sababu Mama yetu Mpendwa ameongeza Bajeti ya miradi ya maendeleo kutoka Trilioni 5.91 mwaka 2015 hadi kufikia Trilioni 15.4 Mwaka 2024. Hii maana yake ni kuwa Mama na Rais wetu Mpendwa ameamua Kugusa Maisha ya watanzania moja kwa moja badala ya kuweka na kutenga mapesa ya kulipana maposho na kununua vitumbua maofisini kwa ajili ya chai.

Lakini pia wakati anaingia madarakani Mwaka 2021 bajeti ya miradi ya maendeleo ilikuwa ni Trilioni 12 tuu. Hivyo unaweza kuona ongezeka la mabilioni kwa mabilioni ya pesa yaliyoongezeka chini ya uongozi shupavu ,imara na madhubuti wa Jemedari wetu kipenzi. Yaani Mama akikusanya mapato anayarudisha haraka sana na moja kwa moja kwa watanzania kupitia miradi ya maendeleo. Ndio sababu watanzania wanalipa mapato na kodi kwa hiari yao kabisa na kuona fahari kulipa kodi kwa sababu wanaona tija ya pesa zao na namna inavyotumika kuleta na kuchochea maendeleo.

Ndio maana ya kuona Maisha ya watanzania yakiboreka kila uchao,furaha ikiongezeka vifuani kwa watanzania,amani ikitawala ,ajira zikimwagwa kwa vijana kila wakati na kila mwaka na kwa secta zote,huduma muhimu na za kijamii zikisogezwa malangoni pa watanzania. Yaani ni tabasamu na furaha tu kwa watanzania. Ni mwendo wa nyuso za matumaini badala ya watu kutembea mabarabarani wakizungumza peke yao kama vichaa au wendawazimu.

Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kuitunza kwa wivu mkubwa sana.watu aina yake hawazaliwi kila siku. Rais Samia Ni Mama mwenye Moyo msafi ,mikono safi na matendo safi.ndio maana Taifa letu linaendelea kubarikiwa kila uchao. Na sasa Tanzania ni kinara wa amani Afrika Mashariki. Hiyo yote ni kwa sababu ya Rais wetu Mpendwa. Tumlinde Rais wetu kwa gharama ya aina yoyote ile iwayo.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Labda hiyo rekodi ni ya kuwa serikali ya kifisadi ikiipiku serikali awamu ya 4 ya jk!
Hakuna ufisadi katika serikali hii. kila senti ya mtanzania inayokusanywa inakwenda kufanya kazi na kuleta matokeo chanya kwenye Maisha ya watanzania
 
2015 - 2024 hiyo ni rekodi ya dunia!!!
 
Cha ajabu ni kwamba ameongeza fedha za maendeleo zaidi kuliko raisi yoyote yule aliyewahi kutoea lakini hana miradi yoyote aliyoifanya kumzidi magufuri zaidi ya kuona mapicha picha na wizi serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…