The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Jumatatu, Februari 24, 2025, amezindua jengo jipya la Halmashauri ya Bumbuli, mkoani Tanga, akisisitiza umuhimu wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Mara baada ya kuzindua jengo hilo, Rais Samia ameeleza furaha yake kwa kupokelewa vizuri na wananchi wa Bumbuli wakiongozwa na Mbunge wao Januari Makamba akisema amefurahi pia kuona mabango ya upendo kutoka kwa wananchi ambayo yanayosomeka: "Tunakupenda sana Mama."
Rais Samia amewashukuru wakandarasi, washauri, na wafanyakazi wa Halmashauri kwa juhudi zao katika kuhakikisha jengo linakamilika kwa ubora, akisema kuwa kazi yao ni mfano mzuri wa ushirikiano wa kiutendaji.
Vilevile ameeleza kuwa, jengo hilo limejengwa kwa lengo la kuhakikisha watumishi wa Halmashauri wanafanya kazi katika mazingira bora na wananchi wanapata huduma kwa urahisi.
"Jengo hili ni la wananchi wa Bumbuli. Huduma zote zitapatikana hapa, na naomba mlitumie kwa manufaa yenu. Lengo letu ni kuboresha huduma kwa wananchi na kutoa fursa kwa watumishi wetu kufanya kazi zao kwa ufanisi," alisema Rais Samia.
Kwa uzinduzi huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekazia dhamira yake ya kuhakikisha maendeleo yanaendelea kusogea kwa kasi na wananchi wanapata huduma bora karibu.
Aidha, aliwataka viongozi wa maeneo husika kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa viwango vya juu vinavyostahili.
Akiwa Korogwe, Rais Dkt. Samia aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Bwawa la Mkomazi pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji za Mkomazi na Chekechea wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Mradi wa Mkomazi, wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 18, unatarajiwa kuhudumia vijiji 28 katika kata saba za Wilaya ya Korogwe, huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 2025.
Katika Wilaya ya Bumbuli, Rais Dkt. Samia alizindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, hatua inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya mkoa wa Tanga. Kuanzia mwaka 2021 hadi mwanzoni mwa mwaka huu, serikali imepeleka takribani shilingi trilioni 3.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku sekta ya afya pekee ikipokea shilingi bilioni 65.6 ili kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa mkoa huo.
Mara baada ya kuzindua jengo hilo, Rais Samia ameeleza furaha yake kwa kupokelewa vizuri na wananchi wa Bumbuli wakiongozwa na Mbunge wao Januari Makamba akisema amefurahi pia kuona mabango ya upendo kutoka kwa wananchi ambayo yanayosomeka: "Tunakupenda sana Mama."
Vilevile ameeleza kuwa, jengo hilo limejengwa kwa lengo la kuhakikisha watumishi wa Halmashauri wanafanya kazi katika mazingira bora na wananchi wanapata huduma kwa urahisi.
"Jengo hili ni la wananchi wa Bumbuli. Huduma zote zitapatikana hapa, na naomba mlitumie kwa manufaa yenu. Lengo letu ni kuboresha huduma kwa wananchi na kutoa fursa kwa watumishi wetu kufanya kazi zao kwa ufanisi," alisema Rais Samia.
Kwa uzinduzi huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekazia dhamira yake ya kuhakikisha maendeleo yanaendelea kusogea kwa kasi na wananchi wanapata huduma bora karibu.
=============================
SHWANGWE LA SAMIA, KOROGWE, BUMBULI NA LUSHOTO NI MITANO TENA
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi katika maeneo ya Bumbuli, Lushoto, Mkomazi, na Korogwe, akilenga kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi. Katika ziara hiyo, alisisitiza umuhimu wa mshikamano kati ya serikali na wananchi katika kutekeleza miradi inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania.SHWANGWE LA SAMIA, KOROGWE, BUMBULI NA LUSHOTO NI MITANO TENA