Rais Samia azindua Kitabu cha Maisha ya Rais wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi

Mwinyi alikuwa mtu wa kuruhusu watu waishi wanavyotaka bila kuvunja sheria tu! Wakununua mali anunue, wa kuponda mali aponde raha ila tu usivunje sheria!

Sama mtu kama huyu unaweza sema hana Legacy? Aliwatoa wazee matopeni kunua sukari kwa foleni, nguo hamna yani upuuzi tu!
 
Watoto wa siku hizi hawajui historia!
 
Huyu mzee ameifanyia makubwa nchi yetu kwa kuitoa nchi katika umasikini wa kutupa hadi kuwa nchi yenye wastani wa maisha (yani sio tajiri wala masikini) aliingia madarakan huku nchi ikiwa nyeupe hakuna mshahara hata wa kumlipa raisi achilia mbali walimu, madaktari au wafanyakazi wa kawaida. Hakuna aliekuwa na ubavu wa kufungua hata duka la kuuza sabuni, ila Mwinyi alipoingia uchumi ukaanza kuimarika, watu wakaanza kufanya biashara zao ili kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao ya kila siku, hela mtaani ilikuwa nyingi, kandambili za mgogo zikatoweka(kabla yake mgogo ilikuwa moja ya vivazi vya fasion). Kikubwa walichofanikiwa kukifanya maadui wa mzee huyu ni kuchukua yale mabaya yote ya mtangulizi wake kumtupia mzee ruksa na kuchukua yale yote mazuri ya mzee ruhusa kumpa Mkapa. Ndio maana utasikia kijana anakwambia kuwa mwinyi aliisababishia umasikini mkubwa nchi hii kana kwamba aliikuta ni tajiri.
 
Mwinyi alifanya makubwa mengi wakati wa awamu yake. Aliipokea Tanzania ya Nyerere ikiwa hoi kiuchumi. Baada ya vita ya Kagera tuliishi maisha fulani ya hovyo sana mpaka 1985.

Mwinyi akawa mtekelezaji wa ERP (Economic Recovert Programs) za Umoja wa Mataifa. Ndipo tukaanza taratibu kuinuka kiuchumi.

Anayeponda huyu mzee kwamba hakufanya lolote inawezekana alikuwa bado anacheza gololi na watoto wenzake miaka ile.
 
mkuu umeeleza vizuri sana,. hao mbwa hawaelewi chochote, wanaongozwa na hisia tu. sisi tulioyaishi maisha kabla na baada ya Mwinyi kuwa rais tunajua alichokifanya. miguuni mistari ilijichora kwa sababu ya hizo ulizoziita kandambili za mgogo/matairi ya magari. yaani acha tu, Tanzani hii tumeyapitia mengi.
 
Hawasomi historia na kujua hali ilikuwaje wakati Nyere anatoka madarakani.Msamehe bure!
 
Huwa wakizinduaga vitabu mwaka unaofuata wanakuwa hawapo tena. Nimeota jambo hilo hilo kwa huyu mzee dah!
 
hivi unaweza kupoteza muda wako kabisa unasoma kitabu cha huyu mzee??unapata faida gani humo ndani?kwa background ip?kwa legacy ipi?
kuna mwingine alikuwa anaitwa mkapa naye alitoa kitabu nasikia,mtanzania yupi??
kwa taarifa yako hata huu upuuzi unaoandika humu bila huyu mzee kuruhusu enzi zake usingejua kitubkjnachoitwa jamii forum au smart phone
 
Kuna Stori ilivuma sana Miaka ya Tisini mwanzoni kuhusu Mzee Mwinyi kumsusia Ikulu Mchonga ninahamu nikisome hicho Kitabu.

Inasemekana alirudi zake Zanzibar kitabu kitamu sana hicho
 
Hawasomi historia na kujua hali ilikuwaje wakati Nyere anatoka madarakani.Msamehe bure!
Kila raisi (kama tulivyo binadam wengine) alifanya mabaya na mazuri. Ila sasa kinachofanyika au kilichofanyika ni kuchukua yale yote mazuri ya mzee Mwinyi aliyoifanyia nchi hii akapewa Mkapa, na yakachukuliwa yale yote mabaya ya mtangulizi wake (hapa nafikiri mtangulizi anafahamika) akabebeshwa Mwinyi (hatujui ni kwa faida gani) Kwahiyo vigumu sana vijana wa kisasa kuyajua mema aliyofanya mzee Mwinyi na ukizingatia kizazi cha sasa kiko busy na kina Diamond, Konde boy na Ali Kiba
 
Huyu dogo hafahamu watu walivaa kaniki kwa kukosa sabuni
 
Mzee Mwinyi na Azimio la Zanzibar huyu mzee alijitahidi sana kuiondoa Siasa iliyofeli ya Ujamaa wa Kijinga lakini alizidiwa nguvu na Makomredi ndani ya CCM ambao hawakutaka mabadiliko na ndio hawa wanaotusumbua mpaka leo hii

Ee Yahwe isaidie Nchi hii.
 
hivi unaweza kupoteza muda wako kabisa unasoma kitabu cha huyu mzee??unapata faida gani humo ndani?kwa background ip?kwa legacy ipi?
kuna mwingine alikuwa anaitwa mkapa naye alitoa kitabu nasikia,mtanzania yupi??
Nasikia hata mwendazake naye alikuwa anaandika kitabu chake sema Islaeli akamuwahi kitabu kikaishia kurasa mbili tu[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…