Rais Samia azindua Kitabu cha Maisha ya Rais wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi

Rais Samia azindua Kitabu cha Maisha ya Rais wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi

Huyu dogo hafahamu watu walivaa kaniki kwa kukosa sabuni
Hahaha.. umenikumbusha kaniki enzi hizo ndo vazi rasmi la kina mama, msuli kwa kina baba, chacha au viatu vya mgogo kwa vijana wa mjini ndio ilikuwa fasion yenyew. Chai ya mkono mmoja yan chai na kiazi 1 cha kuchemsha, tena ikipikwa chai sifuria ya lita tano inahisabiwa vijiko vitano vya sukari yan kila lita kijiko kimoja. Ilikuwa ngumu kumjua kijana wala mzee maana wote ilikuwa ni hali moja kupauka na kunyong'onyea kutokana na kukosa lishe bora nk, bila kusahau suruali za midabwada. Aisee nchii kidogo tu ingekuwa nusu ya jahanamu
 
hivi unaweza kupoteza muda wako kabisa unasoma kitabu cha huyu mzee??unapata faida gani humo ndani?kwa background ip?kwa legacy ipi?
kuna mwingine alikuwa anaitwa mkapa naye alitoa kitabu nasikia,mtanzania yupi??
Kama una muda wa kusomba vitabu vya Shigongo...... Unashindwaje kupata muda wa kusomba kitabu cha mzee wetu....!!? Inawezekana kabisa hakuwa Rais bora lakini kuna la kujifunza toka kwake.
 
Niliwahi kusikia Mama Sitii alikamatwa Airport Dar akitokea Zenj na dhahabu kibao akiwa safarini kwenda Uarabuni kuziuza. Ikapigwa juu juu na Mrema wa mambo ya ndani. Mzee RUKHSA kwa stories nilizosikia hakuwa msafi hata kidogo.
Mwinyi alikuwa mtu wa kuruhusu watu waishi wanavyotaka bila kuvunja sheria tu! Wakununua mali anunue, wa kuponda mali aponde raha ila tu usivunje sheria!

Sama mtu kama huyu unaweza sema hana Legacy? Aliwatoa wazee matopeni kunua sukari kwa foleni, nguo hamna yani upuuzi tu!
 
Watu hawajui kama kuna kipindi mtu kuendesha gari ilikuwa mwisho saa fulani
Kumiliki TV mpaka uwe na kibali pia

Ova
Kibali cha muda kibali cha Mafuta unawaogopa Wehu tunaambiwa ndio Usalama wa Taifa basi ilikuwa tafrani moja kwa moja
 
Niliwahi kusikia Mama Sitii alikamatwa Airport Dar akitokea Zenj na dhahabu kibao akiwa safarini kwenda Uarabuni kuziuza. Ikapigwa juu juu na Mrema wa mambo ya ndani. Mzee RUKHSA kwa stories nilizosikia hakuwa msafi hata kidogo.
Mwalimu pia alikomaa sana na Mzee rukhsa wetu lakini Mwinyi alikuwa na msimamo na HURUMA.
Hivi ingekuwa ni Waziri wa mwendazake amemshika mke wa Raisi si angetumiwa makamanda wa Kijeshi waende kumgawana Nyama
 
Hahahaaaa...... Hakika bwashee!
Watu tulikuwa tunaenda zenji na pport!
Watoto hawajui hilo
Kuna vitu huku bara vingi vilikuwa hakuna ukivitaka uende zenji..especially vifaa vya umeme
Nchi zimetoka mbali

Ova
 
Sio kama Mzee Rukhsa hakujua kuwa Katiba unampa Mamlaka ya Kifalme na Nguvu kubwa sana ndani ya Mipaka yetu alilijua sana hilo ila alikuwa ni MKARIMU na MPOLE mwenye BUSARA.
 
hivi unaweza kupoteza muda wako kabisa unasoma kitabu cha huyu mzee??unapata faida gani humo ndani?kwa background ip?kwa legacy ipi?
kuna mwingine alikuwa anaitwa mkapa naye alitoa kitabu nasikia,mtanzania yupi??
Mkuu wewe ulizoea mipasho ya diamond nenda sisi tutasoma
 
Back
Top Bottom