Rais Samia azindua Rasmi Mradi wa Mkakati wa Treni ya Umeme ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma, leo Agosti 1, 2024

Rais Samia azindua Rasmi Mradi wa Mkakati wa Treni ya Umeme ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma, leo Agosti 1, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Akizindua Rasmi Mradi wa Mkakati wa Treni ya Umeme ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma, leo tarehe 1 Agosti, 2024.

Rais Samia amewapongeza watanzania wote kwa kukamilisha mradi huu na amesema anapenda mradi huu uiunganishe Tanzania hadi Burundi kwasababu Afrika ipo disconnected hivyo kurudisha nyuma ukuaji wa biashara. Kuungana na Burundi na DRC kutapunguza uhitaji wa soko la nje maana biashara nyingi zitafanyika hapa.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

Aidha, Rais amesema mojawapo ya athari za mradi huu ambayo imeshaanza kuonekana ni kupungua kwa mabasi barabarani ambapo kwa wafanyabiashara ni mbaya lakini kwa nchi ni nzuri maana inapunguza ajali na kuwezesha udhibiti mzuri wa usafiri barabarani.

Dhumuni la SGR ni kuwezesha biashara na na hadi sasa yapo mabehewa ya kusafirisha mizigo mingi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), SGR kwa sasa inasafirisha wastani wa watu 7000 kwa siku.
 
Sisi waleee tumekaa hapa tunasubiri
GT2BYa5WsAAPb-Q.jpg
 
Njia ni lie ile lilipo shirika la ndege ilipo mwendo kasi ndipo SGR inaeleke tutawasingizia sana ngedere na bundi si hawana mtetezi.
 
Hakuna Mtangazaji ambaye nilikuwa ninamkubali kutokana na IQ yake Kubwa ila leo hii nimekuvua rasmi Vyeo vyote.

Tizameni TBC1 mumsikie Pumba zake. Hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom