Rais Samia azindua Rasmi Mradi wa Mkakati wa Treni ya Umeme ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma, leo Agosti 1, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Akizindua Rasmi Mradi wa Mkakati wa Treni ya Umeme ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma, leo tarehe 1 Agosti, 2024.

Rais Samia amewapongeza watanzania wote kwa kukamilisha mradi huu na amesema anapenda mradi huu uiunganishe Tanzania hadi Burundi kwasababu Afrika ipo disconnected hivyo kurudisha nyuma ukuaji wa biashara. Kuungana na Burundi na DRC kutapunguza uhitaji wa soko la nje maana biashara nyingi zitafanyika hapa.

Aidha, Rais amesema mojawapo ya athari za mradi huu ambayo imeshaanza kuonekana ni kupungua kwa mabasi barabarani ambapo kwa wafanyabiashara ni mbaya lakini kwa nchi ni nzuri maana inapunguza ajali na kuwezesha udhibiti mzuri wa usafiri barabarani.

Dhumuni la SGR ni kuwezesha biashara na na hadi sasa yapo mabehewa ya kusafirisha mizigo mingi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), SGR kwa sasa inasafirisha wastani wa watu 7000 kwa siku.

sijawaona muheshimiwa bundi na ngedere kwenye huo uzindizi au wamenyimwa mualiko!
 
Hongera sana MH Rais wetu
Kwakweli tunayo kila sàbabu ya kukushukuru kwa hatua hii kubwa tuliyopiga
Matano tena kwa mama👏👏👏👏👏
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Akizindua Rasmi Mradi wa Mkakati wa Treni ya Umeme ya SGR Dar es Salaam hadi Dodoma, leo tarehe 1 Agosti, 2024.

Rais Samia amewapongeza watanzania wote kwa kukamilisha mradi huu na amesema anapenda mradi huu uiunganishe Tanzania hadi Burundi kwasababu Afrika ipo disconnected hivyo kurudisha nyuma ukuaji wa biashara. Kuungana na Burundi na DRC kutapunguza uhitaji wa soko la nje maana biashara nyingi zitafanyika hapa.

Aidha, Rais amesema mojawapo ya athari za mradi huu ambayo imeshaanza kuonekana ni kupungua kwa mabasi barabarani ambapo kwa wafanyabiashara ni mbaya lakini kwa nchi ni nzuri maana inapunguza ajali na kuwezesha udhibiti mzuri wa usafiri barabarani.

Dhumuni la SGR ni kuwezesha biashara na na hadi sasa yapo mabehewa ya kusafirisha mizigo mingi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), SGR kwa sasa inasafirisha wastani wa watu 7000 kwa siku.

Mungu asaidie kudhibiti wale wote watakaokuwa na Nia ya kuhujumu mradi huu Mkubwa wa kimkakati katika ukuaji.wa uchumi
 
Back
Top Bottom