Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda ya maonesho kuhusu masuala mbalimbali ya Elimu kabla ya kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidia Maendeleo ya Elimu Duniani na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amepongeza uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023, akisema ni uamuzi sahihi unaokuja wakati mwafaka wa kuimarisha sekta ya elimu. Ameeleza kuwa tangu mapitio ya mwisho ya sera hiyo mwaka 2015, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na ukuaji wa uchumi, hivyo kuna haja ya kuwa na sera mpya inayokidhi mahitaji ya sasa ya rasilimali watu na viwango vya juu vya elimu.
Amesema GPE imetoa shilingi bilioni 518 kusaidia sekta ya elimu nchini tangu 2013. Fedha hizo zimetumika kujenga shule 2,980, matundu ya vyoo 7,973, nyumba za walimu 64, mabweni 15 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, na madarasa 300 ya awali.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema sekta ya elimu imepiga hatua kubwa kutoka kujadili upatikanaji wa elimu hadi kufikia lengo la elimu bora. amesisitiza kuwa kila mdau anapaswa kujitafakari kuhusu maboresho yanayohitajika. Pia, ameongeza kuwa Bunge, kama mdau wa elimu, lipo tayari kurekebisha sheria zinazohitajika ili kuendana na mabadiliko ya sera mpya.
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023, amesema:
"Wataalam wetu wamechambua vizuri mwenendo wa uchumi wetu, mwelekeo wa dunia, kasi ya maendeleo ya teknolojia na kujifunza kutoka kwa wenzetu. Dhamira yetu katika hili ni kumuandaa kijana anayejiamini na mwenye nyenzo stahiki za kukabiliana na ushindani wa Kikanda na Kimataifa, ili kwa kutumia utajiri wa rasiliamali zetu aweze kunufaika kiuchumi."
"Serikali itaendelea kuajiri walimu wenye sifa na kuwapa mafunzo stahiki ili waendane na mwelekeo wa sera hii [Sera ya Elimu na Mafunzo]. Aidha tutapitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kama mama wa taaluma zote duniani".
"Idadi ya wasiojua kusoma na kuandika nchini Tanzania imepungua kutoka asilimia 70 miaka ya 1960 asilimia 83."
"Sera hii inajibu hitaji la muda mrefu la kuweka mfumo wa kutambua na kurasimisha ujuzi na stadi zinazopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo tulionao."
"Ujuzi, sera na mitaala hiyo pia imeleta somo la ujasiriamali ambalo litakuwa la lazima kwa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne."
"Kwa utaratibu ulivyokuwa mtoto alikuwa anamaliza elimu ya lazima ya miaka 7 akiwa na umri wa miaka 12 hadi 13, umri ambao unamfanya akose sifa za kuajiriwa na hivyo kumfanya awe tegemezi, kupitia sera hii mtoto akiwa na miaka 6 wakati anahitimu elimu ya msingi ya lazimakwa miaka 10 atakuwa na umri wa miaka 16 na hapo atakuwa amemaliza kidato cha nne"