Rais Samia azindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo. Asema Serikali imeongeza bajeti ya utafiti kutoka Tsh 7.35bn hadi 11bn

Hotuba haijanoga kabisa. Hajamuongelea Simba wa Yuda?
 
Hizo billions kama hazikulengwa kuongeza kura zingesaidia sana kilimo, tatizo kilimo ni screen saver nyuma yake kuna kutafuta kura kutoka kwa wakulima ndiyo shida inapoanzia hapo....
Kila kitu nyuma yake kuna kutafuta kura
 
Kila kitu nyuma yake kuna kutafuta kura
Kama isingekuwa hivyo hizo mbinu zinsingetumika kabisa maana zilishatumika now and then na hakuna matokeo...Hiyo ni kulambisha watoto pipi huku njaa ikiwamaliza; ni mbaya, ni hasara kwa taifa...Tuweke katiba mpya ili haya maamuzi yawe kwenye level ya kijiji na siyo watu wachache kuamua kwaajili ya wengi
 
Lakini pia yeye ana invest sana wakati wakuliman wadogo ambao wako wengi wanalima bila kutumia cash na investiments zao ni labour tu kisha wanauza soko lile lile analouza huyo mkulima aliye invest unadhani ata break even? Unless awe na political position auze ghala la taifa na hapo ndipo tunapodanganyana eti tunasaidia wakulima, how wakati vitu vipo obvious na watu hawataki kubadili chochote?
 
Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujayo.

Bashe ameomba fedha hizo leo Jumatatu Aprili 4, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maofisa ugani nchini.

Bashe amesema bei ya mbolea katika soko la dunia imepanda kwa zaidi asilimia 300.

Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.

Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais fedha hii haitapotea. Tumeshafanya hivi katika korosho kwa kugawa ruzuku ya pembeje na tumeongeza uzalishaji tani 40,000,”amesema.


Aidha, Bashe amesema jumla ya maofisa ugani 7,000 watagawiwa pikipiki na vifaa vya kupimia udongo.

“Tumeanza kuwapa elimu maofisa ugani kulingana ekolojia ya maeneo na mazao yanayozalishwa na tutawapa ekari moja kwa kila ofisa ugani, atapewa mbegu bora na mbolea ili akiwafundisha awapeleke shambani,”amesema.

Amesema kuwa majaribio yameanza katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu kwa kutenga mashamba 600 ambapo kila kijiji kitakuwa na shamba darasa ili wakulima wapate elimu stahiki.

Pia amesema maofisa ugani hao watapatiwa vifaa vya kupimia udongo na kwamba hapo mwanzo taarifa za udongo zilikuwa zinapatikana kama za uganga wa kienyeji.

Bashe amesema lengo hadi kufikia mwaka 2025 kila kata iwe na kipimia udongo chake ambapo mkulima atapimiwa udongo na kupewa cheti ambacho kitakuwa na taarifa zote za afya ya udongo wake na aina ya virutubisho vinavyotakiwa.

 
Kijana anajituma sana, aendelee kuchapa kazi aachane na akili za siasa chafu zilizozagaa kila mahala Tanzania.... Taifa bado lina hadhina ya watu Bashe yuko vizuri, kuna yule kijana Bashungwa yuko vizuri, Biteko akiacha yale mambo yake akafocus kazi yuko vizuri, Makamba junior yuko vizuri, Riz 1 yuko vizuri, yule kijana kutoka CDM wa Tunduma yuko vizuri, ...Taifa lina hazina ya vijana SHIDA SIASA CHAFU..

Jafo hatufai Mama piga chini yule Mzaramo..
 
S
 
Watakubali tuu kwamba Samia ni akili hadi kufikia 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…