Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
RAIS SAMIA AIPAISHA JUU BEI YA CHOROKO KWA 100% TOKA TZS 500|800 FY 2020|21 HADI TZS 1,610 FY2021|22 KWA KILO,

Mhe Rais baada ya kufanikiwa kuongeza bei ya Mbaazi kwa zaidi ya 3200%/kg,

Pamba kwa zaidi ya 125%/kg Alizeti kwa zaidi ya 120%/kg,

Sasa ni zamu ya choroko ambayo nayo kwa mfumo uleule bei yake imepanda kwa zaidi ya 100%/kg,

Ukitafuta wastani wa ongezeko la bei kwa mazao yote ya kibiashara yaliyovunwa mpaka sasa utagundua Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kila zao kwa zaidi ya 100%/kg ndani ya kipindi chake hiki kifupi,

Yaani ameongeza bei mara mbili zaidi ya bei ya awali,

Sote ni mashahidi, Wakati bei za bidhaa nyingine mbalimbali ikipanda mwaka hadi mwaka bei ya choroko haijawahi kuvuka Tshs 1,300 kwa zaidi ya mwongo mmoja leo.

Rais pekee mwanamke Barani Africa na Rais wa kwanza Mwanamke EAC,

Mama Samia Suluhu Hassan kwakutambua kuwa zaidi ya 80% ya Watanzania anaowaongoza wanategemea kilimo,

Wakati 58.1% ni wakulima huku 65% ya malighafi zote za Viwandani zinatokana na kilimo

Huku 100% ya chakula chote duniani kinatokana na kilimo huku kilimo kikichangia 27% kwenye Pato la Taifa (GDP) ,

Mama ameamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye Uzalishaji na Masoko ya mazao yatokanayo na kilimo,

Hii ni tofauti kidogo na watangulizi wake wote tangu tupate Uhuru.

Rais Samia amekataa kuuza choroko kwa warehouse recipt Finance (WRF-Stakabadhi ghalani) ili kuondoa gharama za uendeshaji anazokatwa Mkulima kupitia AMCOS kwa kuruhusu biashara huria,

Nandio maana leo wakulima wa choroko wamempokea Rais Samia kama Mama yao kwa kuipaisha bei ya choroko zao.

Kasi ya Rais Samia imeshangaza wengi hasa wakulima wa mazao ya kibiashara,Bei ya choroko nchi China inafikia US$ 1,581/Tani, karibu Tshs 3,500,000,

Bei ipo na ni nzuri nje huenda shida ilikuwa ni haya matozo 232 ambayo Mama Samia aliyoyatoa ndio maana kila kitu ni mseleleko tu.

photo_2021-11-11_10-22-38.jpg
 
Kwani kampeni zimeshaanza? Wengine nao wakianza kampeni zao msiwapeleke kwenye kamati.
Kampeni ya nini au sijakuelewa,
Yaani umpinge mkt wa chama?
Watakuja na Fomu moja kama Magu vile,

CCM inahazina aise huyu Samia huyu
 
Tuambie Kama nchi zingine Bei hazijapanda kwenye hayo mazao ili tumdemkie huyo mama Kama unavyotaka, vinginevyo tujue tu kuwa upo kwenye siasa chafu za kumsifu mtu kwa Mambo asiyofanya ili kuwatapeli wananchi au kutafuta uteuzi

Ni haki ya raia kupewa taarifa sahihi ya mwenendo wa nchi yao

Kumbuka kwenye Katiba ya mbingu, ipo ibara inasema "USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO"
 
Acha kutisha wewe kama Tanzania imepanda na mwandishi anasema bei imepanda kosa Lake liko wapi?
 
Haya mambo yanaamuliwa na Demand vs Supply sio na mtu...ht enzi za JPM korosho ilifika mpaka 4000 kwa kilo then ika drop na haijawahi kufika hapo tena...bei ktk soko la dunia ikipanda lazima na huku ipande, leo mnamsifia kesho bei ktk soko la dunia ikishuka mtatafta pa kuficha nyuso zenu. So mjitahidi kuweka akiba ya maneno.
 
Vinapanda kwakuwa pesa ipo, Purchasing power iko juu,

Watu wanayo pesa tayari najua umeanza kushuhudia kwa macho ya nyama,
Kipimo cha watu kuwa na pesa au purchasing power kuongezeka ni watu kujaa bar, makanisani sadaka kuongezeka,kukosa frem za biashara kariakoo au posta au mijini,kupungua kwa wakaanga Mihogo mitaani,guest na beach kujaa wikiend,shida ya usafiri wikiend asubui kwa jioni,mauzo ya nyama buchani.
Hizi ni baadhi ya vipimo vichache kujua wingi na uchache wa pesa mtaani
 
Haya mambo yanaamuliwa na Demand vs Supply sio na mtu...ht enzi za JPM korosho ilifika mpaka 4000 kwa kilo then ika drop na haijawahi kufika hapo tena...bei ktk soko la dunia ikipanda lazima na huku ipande, leo mnamsifia kesho bei ktk soko la dunia ikishuka mtatafta pa kuficha nyuso zenu. So mjitahidi kuweka akiba ya maneno.

Hii demand 'Vs supply ni wakati wa Mama tu au unazikwepa juhudi zake?

Tuache roho mbaya Rais Samia anafanya kazi kubwa sana,
 
Haya mambo yanaamuliwa na Demand vs Supply sio na mtu...ht enzi za JPM korosho ilifika mpaka 4000 kwa kilo then ika drop na haijawahi kufika hapo tena...bei ktk soko la dunia ikipanda lazima na huku ipande, leo mnamsifia kesho bei ktk soko la dunia ikishuka mtatafta pa kuficha nyuso zenu. So mjitahidi kuweka akiba ya maneno.
Aaaaah! vurugu la korosho unalikumbuka lakini?
 
RAIS SAMIA AIPAISHA JUU BEI YA CHOROKO KWA 100% TOKA TZS 500|800 FY 2020|21 HADI TZS 1,610 FY2021|22 KWA KILO

_______________________________

Mhe Rais baada ya kufanikiwa kuongeza bei ya Mbaazi kwa zaidi ya 3200%/kg,Pamba kwa zaidi ya 125%/kg Alizeti kwa zaidi ya 120%/kg,Sasa ni zamu ya choroko ambayo nayo kwa mfumo uleule bei yake imepanda kwa zaidi ya 100%/kg, Ukitafuta wastani wa ongezeko la bei kwa mazao yote ya kibiashara yaliyovunwa mpaka sasa utagundua Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kila zao kwa zaidi ya 100%/kg ndani ya kipindi chake hiki kifupi, yaani ameongeza bei mara mbili zaidi ya bei ya awali,Sote ni mashahidi, Wakati bei za bidhaa nyingine mbalimbali ikipanda mwaka hadi mwaka bei ya choroko haijawahi kuvuka Tshs 1,300 kwa zaidi ya mwongo mmoja leo,

Rais pekee mwanamke Barani Africa na Rais wa kwanza Mwanamke EAC, Mama Samia Suluhu Hassan kwakutambua kuwa zaidi ya 80% ya Watanzania anaowaongoza wanategemea kilimo, 58.1% ni wakulima huku 65% ya malighafi zote za Viwandani zinatokana na kilimo na 100% ya chakula chote duniani kinatokana na kilimo huku kilimo kikichangia 27% kwenye Pato la Taifa ( GDP) ,Mama ameamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye Uzalishaji na Masoko ya mazao yatokanayo na kilimo,Hii ni tofauti kidogo na watangulizi wake wote tangu tupate Uhuru.

Rais Samia amekataa kuuza choroko kwa warehouse recipt Finance ( WRF-Stakabadhi ghalani ) ili kuondoa gharama za uendeshaji anazokatwa Mkulima kupitia AMCOS kwa kuruhusu biashara huria,Nandio maana leo wakulima wa choroko wamempokea Rais Samia kama Mama yao kwa kuipaisha bei ya choroko zao,
Kasi ya Rais Samia imeshangaza wengi hasa wakulima wa mazao ya kibiashara,Bei ya choroko nchi China inafikia US$ 1,581/Tani, karibu Tshs 3,500,000,Bei ipo na ni nzuri nje huenda shida ilikuwa ni haya matozo 232 ambayo Mama Samia aliyoyatoa ndio maana kila kitu ni mseleleko tu.

... Kazi iendelee...
Zao la cacao vipi?
 
Kanda ya ziwa pamba imenunuliwa kwa tsh. 1750, toka tsh. 900 ya mwaka jana. Bahati mbaya wengi hawakulima mwaka jana baada ya kuchoshwa na Bei,mkopo na mvua kubwa zilizopitiliza na ugonjwa wa pamba kuzeeka ( kuwa nyekundu) kabla ya wakati.
 
Back
Top Bottom