Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

Kanda ya ziwa pamba imenunuliwa kwa tsh. 1750, toka tsh. 900 ya mwaka jana. Bahati mbaya wengi hawakulima mwaka jana baada ya kuchoshwa na Bei,mkopo na mvua kubwa zilizopitiliza na ugonjwa wa pamba kuzeeka ( kuwa nyekundu) kabla ya wakati.
Km wakulima wengi hawakulima mwaka jana means Supply imekua ndogo then Demand imekua kubwa, which means price lazima ipande kwakua wanunuzi wapo teyari kulipa bei ya juu kunyang'anyana kidogo kilichopo..
supply is inversely proportional to demand.

Na hiki ndicho kilichotokea ht huko duniani, watu walijifungia hawakulima or Kuzalisha wametumia akiba imeisha now wanatafta malighafi kwa bei yoyote...

Na hili limejitokea ht kwa mafuta ya kula kupanda kutoka 3000 kwa Lita mpaka 8000 kwa Lita, or Mbolea kupanda bei...
ila wapiga matarumbeta hawatafuti majibu ya kitaalam wanakuja na mapambio.

Sasa subirini dunia ikawe sawa na covid. wazalishaji wakubwa huko america ya kusini warudi mashambani then tutarudi kuujadili huu uzi.
 
RAIS SAMIA AIPAISHA JUU BEI YA CHOROKO KWA 100% TOKA TZS 500|800 FY 2020|21 HADI TZS 1,610 FY2021|22 KWA KILO

_______________________________

Mhe Rais baada ya kufanikiwa kuongeza bei ya Mbaazi kwa zaidi ya 3200%/kg,Pamba kwa zaidi ya 125%/kg Alizeti kwa zaidi ya 120%/kg,Sasa ni zamu ya choroko ambayo nayo kwa mfumo uleule bei yake imepanda kwa zaidi ya 100%/kg, Ukitafuta wastani wa ongezeko la bei kwa mazao yote ya kibiashara yaliyovunwa mpaka sasa utagundua Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kila zao kwa zaidi ya 100%/kg ndani ya kipindi chake hiki kifupi, yaani ameongeza bei mara mbili zaidi ya bei ya awali,Sote ni mashahidi, Wakati bei za bidhaa nyingine mbalimbali ikipanda mwaka hadi mwaka bei ya choroko haijawahi kuvuka Tshs 1,300 kwa zaidi ya mwongo mmoja leo,

Rais pekee mwanamke Barani Africa na Rais wa kwanza Mwanamke EAC, Mama Samia Suluhu Hassan kwakutambua kuwa zaidi ya 80% ya Watanzania anaowaongoza wanategemea kilimo, 58.1% ni wakulima huku 65% ya malighafi zote za Viwandani zinatokana na kilimo na 100% ya chakula chote duniani kinatokana na kilimo huku kilimo kikichangia 27% kwenye Pato la Taifa ( GDP) ,Mama ameamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye Uzalishaji na Masoko ya mazao yatokanayo na kilimo,Hii ni tofauti kidogo na watangulizi wake wote tangu tupate Uhuru.

Rais Samia amekataa kuuza choroko kwa warehouse recipt Finance ( WRF-Stakabadhi ghalani ) ili kuondoa gharama za uendeshaji anazokatwa Mkulima kupitia AMCOS kwa kuruhusu biashara huria,Nandio maana leo wakulima wa choroko wamempokea Rais Samia kama Mama yao kwa kuipaisha bei ya choroko zao,
Kasi ya Rais Samia imeshangaza wengi hasa wakulima wa mazao ya kibiashara,Bei ya choroko nchi China inafikia US$ 1,581/Tani, karibu Tshs 3,500,000,Bei ipo na ni nzuri nje huenda shida ilikuwa ni haya matozo 232 ambayo Mama Samia aliyoyatoa ndio maana kila kitu ni mseleleko tu.


... Kazi iendelee...
Yeye anazinunulia wapi huyo Raisi nimpelekee
 
Mleta mada ndio Musiba wa awamu hii
 
Wanasema Asante Covid 19 kwa kuwachapa kwa hakika wahindi mpaka jeuri ya rais wao Modi kuwasupport kulima mbaazi,choroko nk,zikalegea na kshindwa maana walaji wakui ni wahindi.
Shukrani za pili kwa uchina Kama kweli walitengeneza hiki kirusi rafiki kwa bara la afrika
 
Kipimo cha watu kuwa na pesa au purchasing power kuongezeka ni watu kujaa bar, makanisani sadaka kuongezeka,kukosa frem za biashara kariakoo au posta au mijini,kupungua kwa wakaanga Mihogo mitaani,guest na beach kujaa wikiend,shida ya usafiri wikiend asubui kwa jioni,mauzo ya nyama buchani.
Hizi ni baadhi ya vipimo vichache kujua wingi na uchache wa pesa mtaani
Hapo kupungua kwa wakaanga mihogo nimecheka sana.
 
Hizi sifa nyingine zinalenga kumharibia na sio kumjenga. Mwakani bei itakaposhuka napo mtamlaumu?

Amandla...
 
Kwani kampeni zimeshaanza? Wengine nao wakianza kampeni zao msiwapeleke kwenye kamati.
Nilikuwa najiuliza hili bandiko na komenti mbona zimekaa kishabiki shabiki, but jibu ndilo hilo aseee😃!.
 
RAIS SAMIA AIPAISHA JUU BEI YA CHOROKO KWA 100% TOKA TZS 500|800 FY 2020|21 HADI TZS 1,610 FY2021|22 KWA KILO

Mhe Rais baada ya kufanikiwa kuongeza bei ya Mbaazi kwa zaidi ya 3200%/kg,Pamba kwa zaidi ya 125%/kg Alizeti kwa zaidi ya 120%/kg,Sasa ni zamu ya choroko ambayo nayo kwa mfumo uleule bei yake imepanda kwa zaidi ya 100%/kg, Ukitafuta wastani wa ongezeko la bei kwa mazao yote ya kibiashara yaliyovunwa mpaka sasa utagundua Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kila zao kwa zaidi ya 100%/kg ndani ya kipindi chake hiki kifupi, yaani ameongeza bei mara mbili zaidi ya bei ya awali, Sote ni mashahidi, Wakati bei za bidhaa nyingine mbalimbali ikipanda mwaka hadi mwaka bei ya choroko haijawahi kuvuka Tshs 1,300 kwa zaidi ya mwongo mmoja leo.

Rais pekee mwanamke Barani Africa na Rais wa kwanza Mwanamke EAC, Mama Samia Suluhu Hassan kwakutambua kuwa zaidi ya 80% ya Watanzania anaowaongoza wanategemea kilimo, 58.1% ni wakulima huku 65% ya malighafi zote za Viwandani zinatokana na kilimo na 100% ya chakula chote duniani kinatokana na kilimo huku kilimo kikichangia 27% kwenye Pato la Taifa (GDP) ,Mama ameamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye Uzalishaji na Masoko ya mazao yatokanayo na kilimo,Hii ni tofauti kidogo na watangulizi wake wote tangu tupate Uhuru.

Rais Samia amekataa kuuza choroko kwa warehouse recipt Finance (WRF-Stakabadhi ghalani) ili kuondoa gharama za uendeshaji anazokatwa Mkulima kupitia AMCOS kwa kuruhusu biashara huria,Nandio maana leo wakulima wa choroko wamempokea Rais Samia kama Mama yao kwa kuipaisha bei ya choroko zao.

Kasi ya Rais Samia imeshangaza wengi hasa wakulima wa mazao ya kibiashara,Bei ya choroko nchi China inafikia US$ 1,581/Tani, karibu Tshs 3,500,000, Bei ipo na ni nzuri nje huenda shida ilikuwa ni haya matozo 232 ambayo Mama Samia aliyoyatoa ndio maana kila kitu ni mseleleko tu.

Kazi iendelee
mkuu hivi biashara ya mazao inalipa?
 
Mimi nimepiga ela choroko ufuta na mbazi sasa tunasubiri korosho na pembejeo tumepokea mara mbili bure,hiv mama alichelewa wapi,raha sana!! ila afanyefanye atupe katiba mpya.
 
Mahindi na mchele vitazame kwa jicho la tatu mama, wasukuma tuna mda mrefu hatujaongeza mke.
 
Tuambie Kama nchi zingine Bei hazijapanda kwenye hayo mazao ili tumdemkie huyo mama Kama unavyotaka, vinginevyo tujue tu kuwa upo kwenye siasa chafu za kumsifu mtu kwa Mambo asiyofanya ili kuwatapeli wananchi au kutafuta uteuzi

Ni haki ya raia kupewa taarifa sahihi ya mwenendo wa nchi yao

Kumbuka kwenye Katiba ya mbingu, ipo ibara inasema "USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO"
Kusema ukweli mama ameweka mazingira mazuri ya biashara ya mazao baada ya kuboresha mahusiani na majirani na jumuia ya kimataifa na pia kuondoa yale ma non-triff barriers. Mama Samia kwenye hili amejitahidi sana. Anasitahili pongezi na kutambuliwa. Mazao yote kwa sasa bei ziko vizuri sana.
 
Mbona mimi niko Bukoba na simtaki 2025? Ongelea nafsi yako sio unajumuisha wengine.
Uko bukoba ya wapi mkuu?

Wananchi wengi wa Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla wanamkubali sana mama.

Labda wewe ni wale polisi au tra waliokatazwa kutumia mabavu na kinambikia watu makesi kwa hiyo umekosa ulaji...polee...utazoea tu mdogomdogo.
 
Naunga Juhudi za Samia Leo hata kesho,
Mimi ni nani nisiome haya,

Watu hawatekwi tena,
Maiti hazikutwi tena Baharini,
Wanasiasa wako huru wanafurahi na familia zao,

Wakulima wanashangilia bei ya mazao yao,

Bodaboda faini ten tu,

Umeme elfu 27 na nguzo hulipi,

Ivi mnatakaje wengine?
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mwakajana nilinunua ufuta 1500 nikauza 1300 hasara,nikanunua mbazi 450 kika uza 250 hasara.mwaka huu tumepiga pesa,na korosho sijui itakuwaje,kwamara ya kwanza kusini pembejeo tumepewa bure!sisi tunamuombea dua mzuri MAMA.
 
Back
Top Bottom