Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

Kwenye Kilimo, Mama anaenda vizuri. kila zao huku Morogoro lipo juu. Karafuu Morogoro kg ni elfu 13,000 toka elfu 5,000 miaka iliopita, iliki kg ni elfu 20,000, pilipili manga kg ni elfu 7,000 toka elfu 3,000 miaka iliyopita. nimeona kwa mara ya kwanza ndizi ambazo zilikosa soko kabisa huku morogoro kwa miaka mitatu iliyopita sasa zimeanza kutafutwa. mbaazi na ufuta huku sasa bei nzuri, mbaazi imefika kg 1 kwa tsh 1,ooo ambalo plastiki la kg 20, ni tsh 20,000. Kwa miezi 5 ya uongozi wake nasema anatisha kwenye kilimo.
 
Huyu Mama mbona kama anakuja kasi sana aise

Kila kona Samia, Samia

Wakulima mwaka huu wananunua mabati balaa kumbe mama kawafurahisha
Huko Pemba wakulima WA karafuu wanacheka balaa. Huu mwaka gari zitakosa parking. Mahindi bado.
 
Purchasing power imeongezeka na nini wakati mishahara haijaongezwa kwa miaka sita na biashara nyingi zinakufa au zimekuwa DORO? 😳
Vinapanda kwakuwa pesa ipo, Purchasing power iko juu

Watu wanayo pesa tayari najua umeanza kushuhudia kwa macho ya nyama
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 kazi kubwa kwa sera zipi? Za tozo zinazopingwa kila kona nchini? Za ukosefu wa ajira?
Hii demand 'Vs supply ni wakati wa Mama tu au unazikwepa juhudi zake?

Tuache roho mbaya Rais Samia anafanya kazi kubwa sana,
 
Vinapanda kwakuwa pesa ipo, Purchasing power iko juu

Watu wanayo pesa tayari najua umeanza kushuhudia kwa macho ya nyama

Pesa iko wapi? Ya kukusanya tozo? Tusimvuruge Mama bila sababu. Kuongoza nchi kutegemea wapambe waongo waongo ni kijitafutia shida zisizo za lazima
 
Purchasing power imeongezeka na nini wakati mishahara haijaongezwa kwa miaka sita na biashara nyingi zinakufa au zimekuwa DORO? 😳

Kabisa mkuu biashara zinachechemea. Ila huwezi kufanya siasa bila uongo uongo?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kule Twitter nilimsikia jamaa akisema wanavamiwa usiku wa manane na maccm kuporwa karafuu zao walizovuna na hawana pa kwenda kudai haki yao.
Huko Pemba wakulima WA karafuu wanacheka balaa. Huu mwaka gari zitakosa parking. Mahindi bado.
 
Mungu tunajua Upo,Msimamie mama huyu kila maadui watafunane wenyewe,
 
Wewe si mkulima, vinginevyo usingetamka maneno hayo. Mfuko unajaa, tofauti unaiona bila kupepesa macho eti mpaka nipate ushuhuda nchi nyingine.... Loooooooo balaaaaaa,.
Huu ni msimu wa neema ktk mazao duniani kote yaliko mazao, na si juhudi ya mama
 
Hata mbaazi sasa bei ipo juu, ikumbukwe kuwa Kuna mwaka hakukuwa na soko kabisa, watu waliambiwa wale wenyewe kwani ni mboga, watu wakaamua kuziacha huko mashambani
 
Na kweli "kazi ieendelee". Wakati wa "hapa kazitu#", nchi jirani na kwingeneko walikuwa "lockdown". Kwao huko sasa ni njaa na mahitaji makubwa ya mazao ya kilimo. Kwetu sisi matunda ya kutokuweka "lockdown" sasa ndio yanaonekana. Ukichanganya na "diplomasia ya uchumi" hakuna shaka maendeleo kwa kasi
Acheni unafiki nyie vibwengo wa mwenda zake lock down ilikuwa 2020 lakini soko la bidhaa tanzania limekauka tangu 2016 mwanzoni sasa sijui mnataka kundanganya nani asiye jua, mpeni mama pongezi zake hata kama hamumtaki.
 
Mnafiki ni wewe unayesukumwa na chuki dhidi ya mwendazake. Lakini yawezekana hujui mazao mengi huchukua muda gani hadi kuvunwa. Labda na wewe ni mmoja wa wale walioimbishwa "elimu, elimu, elimu!" na "kuzungusha mikono!". J2 njema
 
Kanda ya ziwa pamba imenunuliwa kwa tsh. 1750, toka tsh. 900 ya mwaka jana. Bahati mbaya wengi hawakulima mwaka jana baada ya kuchoshwa na Bei,mkopo na mvua kubwa zilizopitiliza na ugonjwa wa pamba kuzeeka ( kuwa nyekundu) kabla ya wakati.
Hizo sababu ulizotaja hapo ndio zimefanya bei ipande. Hizo unazoita bahati mbaya ndio zimeamua soko, sio mama Samia
 
Mnafiki ni wewe unayesukumwa na chuki dhidi ya mwendazake. Lakini yawezekana hujui mazao mengi huchukua muda gani hadi kuvunwa. Labda na wewe ni mmoja wa wale walioimbishwa "elimu, elimu, elimu!" na "kuzungusha mikono!". J2 njema
Jibu swali langu acha hoja zako za kitoto hizo hayo mazao hata yangechukua miaka 200 bado circle ya mazao itakuwepo kila mwaka kwa sababu wakati wewe unapanda leo wenzio walisha panda mwaka jana na wengine mwaka juzi na wengine miaka 10 iliyo pita hivyo circle ya mazao itakuwepo kila mwaka, miaka 4.5 iliyo pita soko la mazoa tanzania lilidorola hasa kwa mazao yanayo tegemea sana soko la nje lakini pia hadi mahindi ambayo ni ya miezi mitatu hadi sita kuvuna yalidorora unataka kuniambia nini wewe !? Hata kama una mapenzi na mwendazake lazima tukubaliane kwamba kwenye uchuni wa nchi sera na falsafa yake iliharibu sana uchumi wa kijamii, yeye alikuwa anafurahia pesa kujaa hazina wakati hazipo kwenye mzunguko.
 
Huu ni msimu wa neema ktk mazao duniani kote yaliko mazao, na si juhudi ya mama
2016 - 2020, ilikuwa ni marufuku kupeleka nje mazao na kuuza huko. Kauli ya W/MKUU Majaliwa ilikuwa hivi: Ukikutikana na mazao katikia lori lako unayasafirisha nje ya nchi, mazao hayo yatataifishwa na lile Lori litataifishwa.

Muulize mkulima maarufu aliyekuwa mmiliki wa mabasi ya SUMRI aliyeamua kuhamishia mtaji wake katika kilimo na kujikita huko RUKWA, alivyokuwa akiilalamikia serikali katika siasa zake za kuuwa kilimo.

Haiwezekani katika kipindi hicho uwe na matatizo katika bidhaa zote za kilimo (Mahindi, mbaazi, korosho n.k) bila kuitupia macho serikali.

Kwa wengi huomba wakati hawanacho lakini pale unapojaliwa kuwa nacho na kuongezewa tunasahau kushukuru. Tujifunze kushukuru hata mara 100 pale tunapojaaliwa kupata chochote. Mama anastahili sifa, pamoja na kuwa mwenyewe si mpenda sifa.
 
Hizo sababu ulizotaja hapo ndio zimefanya bei ipande. Hizo unazoita bahati mbaya ndio zimeamua soko, sio mama Samia
Hata kama hivyo ndivyo, inamaanisha unacheza katika maeneo ya bahati, nuru, kisimati au nyota ukipenda. Amini utavyoamini, lakini kama ujio wa Mama ndio umeleta bahati ya kupanda bei za mazao ya kibiashara yauzwayo nje ni heri sana. Kwa maana kwa mkulima hoja ni mfuko ujae mapesa. Kumbe basi tulihitaji ujio wa Mama Samia ili mkulima akomboke!
 
Mnafiki ni wewe unayesukumwa na chuki dhidi ya mwendazake. Lakini yawezekana hujui mazao mengi huchukua muda gani hadi kuvunwa. Labda na wewe ni mmoja wa wale walioimbishwa "elimu, elimu, elimu!" na "kuzungusha mikono!". J2 njema
Mmmmmm, si kwa hasira hizi. Si ajabu nikisema kuwa hapa wenzangu mmetoka nje ya hoja. Yote yazungumzwe lakini hoja moja ni ya msingi kwa mkulima - Mfuko wa mkulima mwaka huu kwa 100% zaidi ya mwaka jana. Hili ndilo la muhimu kwa mkulima.

Poroja pigini, lakini mwenyewe alisema pale Tegeta- Kawe kuwa kelele za mlango hazimzuii mlalaji kupata usingizi. Nafikiri na mkulima asema hivyo hivyo. Nawe JF unasemaje?
 
Hata mbaazi sasa bei ipo juu, ikumbukwe kuwa Kuna mwaka hakukuwa na soko kabisa, watu waliambiwa wale wenyewe kwani ni mboga, watu wakaamua kuziacha huko mashambani
Soko lilikuwepo na lipo siku zote inategemeana na wewe unapokwenda sokoni una lugha gani. Soko la mbaazi, mahindi, korosho, pamba na kahawa liko nje ya Tanzania. Unawatukana wote, toka Kenya mpaka umoja wa Ulaya halafu unategemea wakufungulie soko lao. Akili mali!
 
Katika hili kwakweli pongezi kwa Mama ni mpambanaji, acha forces za market ziamue, mbona maisha hayapo complicated hivyo [emoji3]
 
Back
Top Bottom