Rais Samia azungumza na Rais wa China, asisitiza Mpango wa Kuendeleza Miundombinu na Kukuza Uwekezaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 3, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Ukumbi wa The Great Hall of the People.

Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia amesema uhusiano wa nchi hizo mbili ni muhimu na ametoa wito wa kuendelea kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali pamoja na kuendeleza ushirikiano katika Mpango wa Kuendeleza Miundombinu na Kukuza Uwekezaji (Belt and Road Initiative) ili kuleta manufaa yanayoonekana kwa wananchi.

Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa sekta binafsi nchini China kuwekeza Tanzania katika uzalishaji wa vyanzo vya nishati mbadala na miundombinu ya usambazaji.

Soma Pia: Rais Samia akutana na Rais wa China, Xi Jinping na ujumbe wake
WhatsApp Image 2024-09-04 at 17.31.32_c6c2a424.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping aliyeambatana na Mkewe Profesa Peng Liyuan mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa The Great Hall of the People kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kwa Wakuu wa Nchi na Serikali watakaoshiriki Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) Jijini Beijing tarehe 04 Septemba, 2024.
WhatsApp Image 2024-09-04 at 17.31.30_6f5a5ec1.jpg
Katika mkutano huo, Rais Xi alisema kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati yake na Tanzania ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi zote mbili na kuendeleza uhusiano wa kihistoria ulioasisiwa na waasisi na kurithiwa na vizazi vya sasa.

Rais Xi pia amesema China inaiona Tanzania kuwa ni mfano mzuri wa mahusiano kati ya nchi zinazoendelea katika muktadha wa ushirikiano wa China na nchi za Afrika.

China na Tanzania zimekubaliana kuendelea kubadilishana uzoefu na kupeana mafunzo katika maeneo mbalimbali ya kiserikali.

Akizungumzia kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), Rais Samia ameeleza imani yake kuwa mkutano huo utakuwa na mchango mpya katika kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya Afrika na China na kuhamasisha mchakato wa viwanda na kilimo cha kisasa barani Afrika.

Baada ya mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia, Rais Xi Jinping na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa Hati ya Makubaliano (MOU) baina ya Tanzania, Zambia na China kuhusu uboreshaji wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China (CPPCC), Wang Huning.

Soma Pia: Rais Samia kuhutubia kwenye Mkutano wa FOCAC nchini China
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 3, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Ukumbi wa The Great Hall of the People.

Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia amesema uhusiano wa nchi hizo mbili ni muhimu na ametoa wito wa kuendelea kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali pamoja na kuendeleza ushirikiano katika Mpango wa Kuendeleza Miundombinu na Kukuza Uwekezaji (Belt and Road Initiative) ili kuleta manufaa yanayoonekana kwa wananchi.

Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa sekta binafsi nchini China kuwekeza Tanzania katika uzalishaji wa vyanzo vya nishati mbadala na miundombinu ya usambazaji.

Soma Pia: Rais Samia akutana na Rais wa China, Xi Jinping na ujumbe wake
View attachment 3087125
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping aliyeambatana na Mkewe Profesa Peng Liyuan mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa The Great Hall of the People kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kwa Wakuu wa Nchi na Serikali watakaoshiriki Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) Jijini Beijing tarehe 04 Septemba, 2024.
View attachment 3087133
Katika mkutano huo, Rais Xi alisema kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati yake na Tanzania ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi zote mbili na kuendeleza uhusiano wa kihistoria ulioasisiwa na waasisi na kurithiwa na vizazi vya sasa.

Rais Xi pia amesema China inaiona Tanzania kuwa ni mfano mzuri wa mahusiano kati ya nchi zinazoendelea katika muktadha wa ushirikiano wa China na nchi za Afrika.

China na Tanzania zimekubaliana kuendelea kubadilishana uzoefu na kupeana mafunzo katika maeneo mbalimbali ya kiserikali.

Akizungumzia kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), Rais Samia ameeleza imani yake kuwa mkutano huo utakuwa na mchango mpya katika kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya Afrika na China na kuhamasisha mchakato wa viwanda na kilimo cha kisasa barani Afrika.

Baada ya mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia, Rais Xi Jinping na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa Hati ya Makubaliano (MOU) baina ya Tanzania, Zambia na China kuhusu uboreshaji wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China (CPPCC), Wang Huning.

Soma Pia: Rais Samia kuhutubia kwenye Mkutano wa FOCAC nchini China
Wa Kilimanjaro mjitayarishe kuhamishwa ,mlima mnauharibu , wachina wanaweza kuulinda vema. Mnakwenda Msomera johnthebaptist
 
Back
Top Bottom