Pre GE2025 Rais Samia: Bado hatujapata chama mbadala wa kuiongoza nchi hii

Pre GE2025 Rais Samia: Bado hatujapata chama mbadala wa kuiongoza nchi hii

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Rais Samia aliyasema hayo akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) jana Septemba 28, 2024.

"… mabadiliko yote yanayotokea ni katika kukiimarisha chama chetu tukitambua kwamba bado hatujapata mbadala wa chama cha kuongoza nchi hii, bado hatujakipata.

"Kwahiyo ni lazima tuimarike na tusimame imara kuiendesha Tanzania ambayo tumeifungua kwa fursa nyingi sana, lazima tuimarike.

"Lakini vilevile mmeshuhudia mabadiliko ndani ya chama chetu ya vitendea kazi, tumeweza kukipatia chama vitendea kazi na hakuna sababu kwanini tushuke chini ya asilimia 80 katika chaguzi zinazoendelea, kwasababu kawa, wilaya, mkoa, na taifa kote kuna vitendea kazi na ndio maana mmesema mmeweza kuzunguka maeneo yote hayo kwasababu mmewezeshwa kufanya hivyo."


 
Rais Samia aliyasema hayo akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) jana Septemba 28, 2024

View attachment 3110057
Ili hilo lithihirike vyama vyote vipewe uwanja sawa wa kisiasa. Polisi waache kukwamisha shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani ili kupata ukweli wa nguvu ya Chama tawala kisiasa.
 
Hutanielewa wala hutaelewa km hujawahi kuongozwa na halmashauri inayoongozwa na upinzani.mwaka 1995 tulichagua mbunge wa chadema karatu dr slaa akafanya mambo makubwa yakiwemo maji kila sehemu awali chini ya ccm hatukuwah kuwa na maji na michango kila mwaka wanakula ya maji lakin chini ya chadema tukapata maji bila mchango wowote.mwaka 2000 halmashauri ikawa chn ya cdm ikafuta kodi ya minyanyasho(kod ya kichwa) wakaanza kujenga kila kata secondari na kufuta ada ya shuleni na kusomesha watoto wasiojiweza.wakati serikal inatangaza sec za kata sis tayar tuna secondari kila kijiji bila ada.barabara kukarabatiwa kwa mda zahanati kila kijiji hayo yote yalifanyka chini ya chadema,ccm hatukuona kwa CHADEMA YALIWEZEKANA.NI MENG MAZURI YA CHADEMA IKIWEMO UHURU WA KUWAJIBISHA VIONGOZ WAZEMBE na tulishamwajibisha mkuu wa wilaya wakati huo ABDALAH KIHATU akaondolewa na bosi wake MKAPA tulimtoa kwa maandamano.MAGUFULI alichukua karatu kwa nguvu uchaguz uliopita cha ajabu ule UZEMBE UWIZI UFISADI UMERUDI KWA KASI.
 
Rais Samia aliyasema hayo akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) jana Septemba 28, 2024

View attachment 3110057
It's, possible kama cdm vinaongozwa na MTU mmoja tu miaka yote na mnatumia uongo zaid kuhalalisha mambo yenu. Mfano pale mwembe Yanga mlisema Lowasa ni fisadi, lakin akawa mgombea urais wa cdm mwaka 2015 . Ina maana cdm wanatumia uongo mwingi kwenye sasa. Samia yupo sawa.
 
Aruhusu uchaguzi huru na wa haki aone moto wake, CCM inategemea wizi wa kura na mabavu ya vyombo vya dola hasa polisi na TISS.
 
Kwa mfano Chadema ambao ndio wanajiita chama kikuu cha upinzani,

sasa hivi ndio wanajifunza namna ya kuandamana.
 
Back
Top Bottom