Rais Samia: Bado ninaisikia sauti ya Hayati Magufuli akiniambia kuhusu miradi na Dodoma kuwa Makao Makuu

Rais Samia: Bado ninaisikia sauti ya Hayati Magufuli akiniambia kuhusu miradi na Dodoma kuwa Makao Makuu

Mngetuwekea na kapicha/Mchoro ili tuone jinsi hizo Ringroads zitakazofanya kazi,maana kwa sisi wengine wenye uelewa mdogo bado mnatuchanganya tu...
sina picha mkuu lakini nitajitahidi kukuelekeza kwa ufahamu wangu ulivyo juu ya hii barabara, hii barabara itachepuka pale mtumba(mji wa kiselikali).

inaelekea kaskazini na kusini

kisha inaelekea magharibi had nara

inaungana na barabara kuu inayoelekea singida,

kwa ufupi ring road inaizunguka Dodoma, Dodoma mjini inakuwa katikati imezungukwa na ring road, mtu anaetoka morogoro
kama anaenda mikoa ya singida, Tabora au Mwanza.

atakuwa hana ulazima wa kupita katikati ya mji ili kuepusha msongamano wa magari hasa magari makubwa, akifika mji wa kiselikali kabla hajaingia dodoma mjini, atachepuka kwenye ring road, atatokezea nara.

kisha ataendelea na safari yake pasipo kupitia dom town,
 
Tunaweza kubadilisha mwngi kuifanya Dodoma inawiri lakini itaendelea kuwa mbaya kwa sababu ubaya wa Dodoma ni wa asili. Hali ya hewa ni mbaya, hatuwezi kubadilisha. Ardhi yake ni mbaya, tunaweza kurekebisha kiasi lakini hatuwezi kubadilisha...
Kama neno lako la mwisho lingekuwa na kiulizo, ningejibu NDIYO.
 
Rais Samia leo akiwa anaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara za pete(ring road) jijini Dodoma amesema bado sauti ya mtangulizi wake hayati Magufuli anaisikia ikimtaka akamilishe miradi yote aliyoiacha....

Ni vyema ukakumbuka na mengine yale mazuri ya Magufuli, kama vile kupunguza matumizi serikalini yasiyo ya lazima na ubadhirifu wa mali ya umma.

Usipofanya Hivyo utakuwa unacheza mikononi mwa adui zako pale nchi itakapopata CREDIT RATING mbaya kutokana na matumizi kuwa zaidi ya mapato na nchi kushindwa kumudu madeni yake!

Miradi unayokamilisha ni mikubwa na yenye kuhitaji fedha nyingi ambazo TOZO kwa wananchi haziwezi kufanikisha. Chunga sana mapato na pia matumizi ya serikali yako kwani umezungukwa na mchwa!
 
Tunaweza kubadilisha mwngi kuifanya Dodoma inawiri lakini itaendelea kuwa mbaya kwa sababu ubaya wa Dodoma ni wa asili. Hali ya hewa ni mbaya, hatuwezi kubadilisha. Ardhi yake ni mbaya, tunaweza kurekebisha kiasi lakini hatuwezi kubadilisha...
uliishi dodoma ipiii mzeee , dodoma imepangika lbd kama hujaishi dodoma.
 
Back
Top Bottom