Rais Samia: Bado ninaisikia sauti ya Hayati Magufuli akiniambia kuhusu miradi na Dodoma kuwa Makao Makuu

Rais Samia: Bado ninaisikia sauti ya Hayati Magufuli akiniambia kuhusu miradi na Dodoma kuwa Makao Makuu

Rais Samia leo akiwa anaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara za Pete (Ring Road) jijini Dodoma amesema bado sauti ya mtangulizi wake Hayati Magufuli anaisikia ikimtaka akamilishe miradi yote aliyoiacha, ikiwemo huo wa ujenzi wa Barabara za Ring Roads zitakazowezesha kuipanga na kuipendezesha jiji la Dodoma.

Rais Samia amesema ameachiwa urithi mzito wa kukamilisha miradi yote na atafanya kama alivyowaahidi Watanzania kuwa hakuna hata mradi mmoja utakaoshindwa kukamilika na wananchi wasiwe na wasiwasi.
Mama anashida sana kwa kweli hiyo ni kauli ya kinafiki sana .mbona nape na makamba kila siku wanamtukana halafu ndo kwanza anawakingia kifua
 
Sio huyu aliyesema akiwa ughaibuni kwamba JPM alikuwa anamu-undermine ?!!!!

By the way so called miradi ya mtu na sio ya Watanzania ndio inafanya watu wasione hivi vitu ni mali yao..., na kama ni mali ya watanzania kwanini sauti ikutese; kwanini usifanye sababu ndicho kilichokuweka hapo / kazi yako...
Ndiye huyu huyu, anajifanya anacheza na akili zetu
 
Mbona thread za magufuli mmezifukuws nyingi hivi what happens guys?
 
Back
Top Bottom