Rais Samia, bado RC Chalamila na RC Hapi

Rais Samia, bado RC Chalamila na RC Hapi

Katika awamu ya tano kuna vijana viongozi waliotia fora kutumia madaraka vibaya.

Mama Samia amewakonga mioyo watanzania kwa kumuondoa Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai, aliyetia fora kwa kuongoza kwa ubabe, uonezi na uporaji.

Sasa bado viongozi wawili, RC wa Mbeya Chalamila, mtu asiye na staha wala karama ya uongozi, na RC wa Iringa, Hapi aliyewahi kuwadhalilisha wazee wa chama, kina Makamba na Kinana.

Hawa walikuwa vile vile wanatumika, lazima nao waende zao.
Jidu matarajio yamefikiwa kwa 50% ndani ya wiki tatu!! Hongera kwa maono, nahisi hii 50% iliyobaki itakuwa funzo kwa wengineo pia
 
Sikiliza,. Mimi sio Chalamila na wala sina maslahi ya moja Kwa moja kutoka kwake. Lakini penye ukweli lazima niseme. Tuhuma nyingi Kwa Chalamila kimsingi si tuhuma Bali majungu, ufuata mkumbo na ulimbukeni tulionao watanzania wengi kuzungumzia Mambo ambayo hatuyajui vizuri.
Kwa hili lililotokea una maoni gani? au unadhani ni figisi tu?
 
Hatimaye Kimeeleweka Sasa
Ole Sabaya
Albert
......
.......
........
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Teabag Inatoa Rangi Tu Mpaka Kikombe Kifurike 😅😄😃😂😁😀
 
Sikiliza,. Mimi sio Chalamila na wala sina maslahi ya moja Kwa moja kutoka kwake. Lakini penye ukweli lazima niseme. Tuhuma nyingi Kwa Chalamila kimsingi si tuhuma Bali majungu, ufuata mkumbo na ulimbukeni tulionao watanzania wengi kuzungumzia Mambo ambayo hatuyajui vizuri.
Njoo umtetee tena!! Tuliwaambia hapa hana busara za uongozi mkatuita tuna wivu.
 
Hivi Happy ndio anaitisha mkutano saa 4 asubuhi ahalafu anakuja saa sita? Hafai kuwa kiongozi wa umma kama hiyo ndio tabia yake
 
Tofautisha vichekesho vya kuchombeza na hoja za msingi,acha chuki zako za kijinga.Kama ni kukosa maadili hakuna kati yao ambae alimzidi JPM kwa kuropoka hovyo,kutukana watu,kudhalilisha watu,wanawake,walifikwa na maafa na kuongopa hadharani.Hayo yaliendana na mtu aliyekuwa ofisi kuu.

So far hakuna hoja serious ya kimaadili,kuvunja kiapo chake au kushindwa kusimamia maendeleo,kwa hiyo tafuta excuses zingine.Mbeya kuwa na RC dizaini ya Makala fisadi na asiyeweza kuwajibika ilikuwa hasara ila Chalamila kaiweza vizuri,watu jeuri wapelekee mtu jeuri.

Nilichomkubali Chalamila ni kudhibiti ubadhirifu hapo mkoani na hacheki na nyani
Ulitetea kwa gazeti refu kweli cjui leo utajificha wapi. Emb:icile!!
 
Back
Top Bottom