Pre GE2025 Rais Samia: Barabara ya Handeni - Kiberashi - Singida Ijengwe kwa PPP

Pre GE2025 Rais Samia: Barabara ya Handeni - Kiberashi - Singida Ijengwe kwa PPP

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nikikumbuka enzi hizo JPM anaanzisha SGR wataalam wa mambo wakawa wanasema hiyo reli mpaka ikamilike itachukua wastani wa miaka 15-20 na itatumia sio chini ya 20trilion machawa wakaja juu na kuwabeza Sana, siunajua Jiwe alikuwa fiksi Sana kwamba pesa ya kuujenga huo mradi ipo cash na itamalizika baada ya miaka mitano. Yaan Kwa kifupi SGR imesizisha mambo mengi km na hiyo njia ya Handeni,kiberashi.
 
Huyu mama si kapewa $2.5 bln na Korea ya Kusini? Anashindwa nn kutoa $200 mln kujenga barabara ya Handeni-Singida?
 
Huu mradi una hasara nyingi kuliko faida!
1. Inabuniwa ili kuzoohofisha Barbara ya Tanga, himo,Moshi ,Arusha,babati
2. Inabuniwa ili tunyonywe miaka isiyo julikana.
3. Imebuniwa ili kuongeza upigaji.
 
Mirad kbao imesmama.njombe Itoni lusitu imesmama .njombe makete kitulo umesimama.songea rrwanda to ituli mwanza daraja la magu lmesmama.darara la itembe simiyu lmesmama. Barabara ya kamanga sengerema imesmama handeni barabara imesmsama tumalize kwanza hzo kwa chache ndo tufanye mirad mipya mh Rais wetu kpenzi.
 
Ukiona mbinu unayopendelea wewe, wenzako ambao mko katika hali sawa na wenyewe wanaijua lakini haiwatumii; basi kuna mawili. Either wewe mjinga sana au wao wajinga sana.

Nchi maskini bado zinahitaji kujenga infrastructure project kama merit good kuchochea uchumi wao. Barabara za PPP zinaongeza product costs mapema kabla ya hata huo uzalishaji wenyewe aujaanza.
 
Kweli kabisa, PPP mimi siikuballi, kama barabara ya chalinze Moro imeshindikana sembuse Handeni.

Bora ijengwe polepole kw miaka miwili au mitatu, kila mwaka kilometa 150. Barabara za umma zisiwe za kulipia
Mimi sikatai wish tujenge wenyewe labda tujitathmin kwanza, sawa kuna huu mradi wa barabara at least kuna mwangaza, je kuna miradi mingapi ya kimkakati inahitaji fedha tukisema tunauzungumzia na huu utaonekana kwa karibu? na ndio maana serikali imeona ili ku_rescue na utekelezaji wake uende kwa haraka ni vyema tushirikiane na sekta binafsi. Utanzania kwanza wkt wa utekelezaji hilo ni suala jingine kbs
 
Tukiyafurahia mazuri haya tunaitwa MACHAWA....

Kwa makubwa na mazuri ayafanyayo mh.Rais SSH ni uamuzi wenu kutuita majina yoyote mpendayo.....

#Mh.Rais Samia anaupiga mwingi ilioje!
Nenda Palestine Jiulize 1950 nakadhalika wale majew walikuwa wanaingia mikataba ya aina gani?
 
PPP ya Kafulila,kwanini haendi Pemba na Unguja, kuwaelezea na kuwapa miradi
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Ujenzi kukaa na Wizara ya Uchukuzi kukubaliana kwa pamoja kutafuta mwekezaji atakayeshirikiana nao kujenga barabara ya Handeni - Kiberashi - Kijungu - Chemba - Kwamtoro - Singida (km 340) kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP).

Rais Samia ameeleza hayo leo tarehe 01 Machi, 2025 alipotembelea Bandari ya Tanga na kuzungumza na wafanyakazi wa Bandari Mkoani Tanga na kusisitiza umuhimu wa barabara hiyo katika kurahisisha usafiri na kuchochea uwekezaji kati ya Mkoa wa Tanga na Singida.

View attachment 3254836

“Barabara hii ni muhimu sana kwa maendeleo yetu ya Bandari, nimezungumza na Waziri hii barabara tuifanye kwenye PPP, tusiwaachie Wizara ya Ujenzi hii barabara haitakwenda haraka”, amesema Rais Samia.

Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Rais Samia ameeleza kuwa barabara hiyo ni muhimu kwani ndiyo inayotarajiwa kubeba magari makubwa ya mizigo yanayotoka Tanga na kupeleka maeneo mengine na hivyo kuagiza iwekewe mageti ‘road tolls’ kwa ajili ya watu kulipa.

View attachment 3254841

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameeleza kuwa barabara ya Handeni - Kiberashi hadi Singida ikijengwa italeta ufanisi mkubwa wa Bandari ya Tanga kwani itapunguza usafiri wa kwenda Singida kwa takribani kilometa 250 na kupunguza matumizi ya mafuta kati ya lita 100 mpaka 120.
Maneno yamezidi hakuna wakandarasi
 
Sawa Mama anafanya ya heri

Tangu mama amteue Kafulila kwakweli PPP imeanza kufanya Chochote,

Hongera Samia,
Hongera Kafulila

Hongera kabla ya utekelezaji ?
Mmeshaahidiwa mangapi tangu Uhuru wa Tanganyika na hadi Leo hayajafanyika ?

Eti hongera ! 🤔🤔
Kwa ahadi tu kabla ya utekelezaji??
Iła Watu kama wewe aisee!
 
Back
Top Bottom