Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 5,566
- 5,477
BILA KATIBA BORA ATAKUWA HAJATUTENDEA HAKI, ... NI BORA ACHUKIWE KWA HILO!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samia ni rais, lkn she is free to excute her power to that extent.Kwa mara hii inawezekana hasa kutoka kwa Wazanzibari ambao mara nyingi wanaongelea kuwa wanataka ZNZ yenye Mamlaka Kamili. Ni fursa ya ZNZ sasa kuweza kuifanya ZNZ isimame na ijipange kiuchumi
Kama huelewi maana ya kupata katiba mpya iliyo bora unabaki kuwa ni mzigo kwa taifa.Pamoja na kumpamba mama hana mpango wa kubadili katiba.
labda ungetumia muda wako kuiomba CHADEMA wabadili katiba ili Mbowe awaachie na wengine.
Sasa tueleze kwa nini CCM haitaki katiba ya wananchi,ina tatizo gani kubwa hadi CCM ihofie? si wana CCM ndio waliipitisha kwa nini hawataki kumalizia?Watu wengine akili zao zimepakatwa na wengine. Hivi kwa jinsi ilivyo katiba ya tanzania inapungua nini hadi mtu uamini hushindi uchaguzi kwa sababu ya katiba. Viongozi wa chadema wanajua kwa nini wanashindwa uchaguzi ila wamewaaminisha nyumbu wao eti hawashindi kwa sababu ya katiba.
Nachowaeleza hata ikiandikwa katiba mpya chini ya serikali ya ccm haitawasaidia wapinzani kuingia madarakani. Na kama lengo la wapinzani ni serikali tatu wala hilo halitatokea chini ya ccm au chama kingine kinachopenda kuwepo muungano. Lengo la madai ya serikali tatu ni ili kurahisisha kuvunja muungano.
Wewe inaonekana kichwani kuna utupu. Watu wanaongelea katiba inayolinda maslahi ya umma na Taifa, wewe unaongelea mambo ya uchaguzi!! Hopeless kabisa. Badala ya kuwaza ustawi wa Taifa, unawaza uchaguzi. Mawazo mafupi kabisa.Watu wengine akili zao zimepakatwa na wengine. Hivi kwa jinsi ilivyo katiba ya tanzania inapungua nini hadi mtu uamini hushindi uchaguzi kwa sababu ya katiba. Viongozi wa chadema wanajua kwa nini wanashindwa uchaguzi ila wamewaaminisha nyumbu wao eti hawashindi kwa sababu ya katiba.
Nachowaeleza hata ikiandikwa katiba mpya chini ya serikali ya ccm haitawasaidia wapinzani kuingia madarakani. Na kama lengo la wapinzani ni serikali tatu wala hilo halitatokea chini ya ccm au chama kingine kinachopenda kuwepo muungano. Lengo la madai ya serikali tatu ni ili kurahisisha kuvunja muungano.
Hao ni vichwa vigumu, lakini tusikate tamaa kuwapa elimu ya bure mpaka waeleweKama huelewi maana ya kupata katiba mpya iliyo bora unabaki kuwa ni mzigo kwa taifa.
Haya malalamiko kuwa kila rais anakuja na mambo yake na kukosa dira kama taifa inatokana na kukosa katiba iliyo bora.
Vinginevyo wewe ni mbinafsi sana, au mnafki sana au hauna akili kabisa.
Straight Up Bams, umeliweka vizuri kiasi hata mbumbumbu ataelewaWewe inaonekana kichwani kuna utupu. Watu wanaongelea katiba inayolinda maslahi ya umma na Taifa, wewe unaongelea mambo ya uchaguzi!! Hopeless kabisa. Badala ya kuwaza ustawi wa Taifa, unawaza uchaguzi. Mawazo mafupi kabisa.
Tunataka katiba itakayowahakikishia Watanzania na Taifa lao ustawi wa wakati wote, bila ya kujali nani ni Rais, anatoka chama gani. Tunataka umma uwe juu ya Serikali, juu ya Bunge na juu ya mahakama.
Katiba yetu hii mbovu, yeyote anayekuwa kiongozi, akitaka kuwa dikteta, hakuna atakayemdhibiti. Marehemu aliamua kuwa dikteta, nani aliweza kukohoa? Hata ndani ya CCM, hakuna aliyethubutu. Robo tatu ya wagombea ubunge walioshinda kwenye kura za maoni, aliwakata majina yao, nani aliweza hata kuhoji?
Tunataka katiba inayozuia mtu mmoja kufanya chochote atakacho, hata kama wananchi wote hawataki.
Yote hayo yatapatikana ndani ya Katiba mpya ya wananchiHitaji la haraka la watanzania si katiba mpya bali ni kujenga utengamano na mshikamano pasipo kuangalia itikadi ya siasa. Sisi ni watanzania kwanza kabla ya chote kile. Mchakato wa katiba utaishia kutugawa tena!!
ccm si ndio nyie nyieCCM hawataki KATIBA.
SI mama wala wajumbe, wana damu mikononi mwao, wanaogopa tume mbalimbali zilishatoa majibu hasa mauaji ya zanzibar, kifo cha akwilina , mtwara, kibiti na mizoga ya koko beach, hawawezi kubali.
Wale wenye CCM wenyewe wanataka sana Katiba Mpya ya wananchi kwa kuwa hata wao wakati wa Mwendazake waligaragazwa sanaSasa tueleze kwa nini CCM haitaki katiba ya wananchi,ina tatizo gani kubwa hadi CCM ihofie? si wana CCM ndio waliipitisha kwa nini hawataki kumalizia?
Mtanzanyika Huru umeliweka vizuri, hata hapa Kenya Mwai Kibaki anapata heshima kwa kuwezesha Katiba huru ya wananchiKatiba MPYA Ni token moja yenye maksi nyingi Sana
Atakaye komaa nayo atakumbukwa milele.
Abraham Lincoln alikuwa Rais wa 16 wa marekani lakini ndio RAIS maarufu kuliko wale wenzake wa kipindi kile na anakumbukwa Hadi leo
Alipitisha Sheria za kuwaachia watumwa
Aliiunganisha marekani iliyokuwa inataka kugawanyika sababu ya civil war baina Southerners and northerners .
Japo alitawala kipindi kidogo Sana muhula mmoja Ila alifanya akumbukwe. Hadi leo
Ukienda pale Washington DC Kuna bonge la monument/statue wamemjengea Ni phenomenal.
Tuwe na subira. Madam SSH ni Rais wa surpriseNgoja tuone...
Turudi hapa tenaJ K Nyerere alikuwa Pan Africanist na hicho ndicho kilicho mpamanua dhidi ya wenzie kama akina Jomo Kenyatta au Milton Obotte. Miaka yote alifikiria kuunga mkono mapambano ya nchi zinazopigana na wakoloni.
Mwinyi alikuwa mwana Diplomasia mliberali na ndiyo maana akafungua milango ya uchumi wa soko huria miaka ya 1985-95 na kujipatia jina la Ruksa. Uanzishaji wa Madaladala na uuzwaji wa mitumba uliopo mpaka leo ni moja kati ya maamuzi yake bora kabisa.
Mkapa alikuwa Mwandishi na Mwana Diplomasia mbobezi na muumini wa uchumi wa sekta binafsi. Alijipambanua kwa ile sera ya "Uwazi na Ukweli" na tukaona magazeti na vituo vya TV na Radio binafsi vikishamiri. Na tukashudia na kasi kubwa ya kuuzwa kwa mashirika ya umma (privatisation). Ni baba wa mapinduzi ya uchumi huu wa kisasa tulionao.
Kikwette alikuwa Mwanasiasa aliyegeuka Mwana Diplomasia. Alibebwa na kauli ya "Maisha Bora kwa Watu Kila Mtanzania". Na kwa kusema ukweli alijitahidi kuwa kila mtu aweze kupata riziki kutokana na mazingira aliyopo. Tutamkumbuka kwa kupanua Uhuru wa maoni, demokrasia na usuluhishi wa migigoro kwa majadiliano.
Magufuli alikuwa ni Mkemia aliyejihuisha kuwa mhandisi wa miundombinu. Kwa miaka aliyohudumu kama Waziri kwenye Awamu ya Mkapa na Kikwette alijenga barabara barabara na madaraja mengi kuliko kiongozi yeyote. Hiyo ndiyo ilimpambanua na kuwa Rais wa miundombinu katika kipindi chake cha u-Rais kwa kauli yake ya "Hapa Kazi Tu". Aliona miundombinu ndiyo itakuwa chachu ya kujenga uchumi. Lakini kipindi chake kifupi kimeacha majeraha mengi kwenye haki za kiraia, Utawala bora, ukandamizaji demokrasia, utekwaji wa WAKOSOAJI, uwapo wa kikundi cha WASIOJULIKANA, dhuluma kwa wafanyabiashara kupitia TASK FORCE na mengine mengi.
Aidha ile kauli ya Baba wa Taifa mwaka 1982 kuwa "Katiba hii imenipa Madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu", ilijidhihirisha kipindi cha Magufuli.
Kimsingi kila Rais au kiongozi falsafa yake hujengwa na kile alichokifanya sana au kile kilichomjengea umaarufu.
Je Rais Samia Ni Nani?
Rais Samia ni Public Administrator ambaye amehudumu kama Waziri wa Mazingira na Muungano kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais kipindi cha Jakaya Kikwette.
Lakini hicho siyo kilichomjenga kuweza kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye Makamu wa Rais wa Tanzania kwenye awamu ya Magufuli.
Mwaka 2014 SSH alichaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge Maalum la Katiba (BMLK) chini ya Samuel Sitta (RIP). Hii kazi aliyoifanya kama Naibu Spika wa BMLK ndiyo imemjengea haiba aliyonayo.
SSH anaamini katika kufanya mambo kwa kufuata katiba, anaamini katika Utawala wa Sheria. SSH anataka kila Mtanzania atendewe haki, hapendi dhuluma kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa Taifa. Ana amini katika Uhuru wa vyombo vya habari na ukosoaji chanya. Ana amini katika ushirikiano wa kimataifa utakuza uchumi kupitia uwekezaji.
Kwa maoni yangu yote anayofanya Rais SSH ni mazuri lakini yasipowekwa kwenye MUSTAKABALI SAHIHI yatapotea.
Kitu pekee kitakacho yafanya mambo anayosimamia yabakie kuwa ya kudumu ni KUMALIZIA mchakato wa KATIBA, kile ambacho ndiyo kinajenga haiba yake.
Kwenye Ilani ya CCM ya 2015, kulikuwa na ajenda ya kumalizia mchakato wa KATIBA. Kwa hiyo CCM kama Chama kinataka Katiba mpya ya wananchi.
Bahati mbaya mtangulizi wake Magufuli hakunona kama ni KIPAUMBELE kwa kuwa haiba yake ilijengwa na miundombinu.
JK hakumaliza mchakato wa KATIBA mpya kwa sababu alikuwa DHAIFU (Hili tusibishane, kwa kuwa hata JJ Mnyika aliwahi kutamka Bungeni).
Nini Afanye Samia?
Anaweza kuwapata wataalamu wa Sheria na Katiba ambao siyo ndumila kuwili (kama Polepole + Kabudi) wakazi huisha Rasimu zile 2 ya Warioba na ya Sitta/ Chenge). Wakaangalia katika vipengele vinavyokinzana ni vipi vina masilahi mapana ya Taifa letu la Tanzania. Kisha wakaipeleka kwenye hatua ya REFERANDUM
Namsihi Rais SSH kama anapita humu JF au wasaidizi wake wamwambie kuwa Yeye ni Tunda la BMLK, na Tanzania itamkumbuka milele na milele kama atatuachia KATIBA mpya ya wananchi.
Atakumbukwa kwenye UKURASA mmoja na J K Nyerere hata kama atakaa kipindi kimoja cha miaka 5.
Afrika Kusini na Kenya wanafaidi matunda ya Katiba ya Wananchi. Kule tumeona namna Institutions zilivyo STRONG kuliko PERSONALITIES. Magufuli alikuwa VERY STRONG person akazizidi na Institutions zetu zote za Mahakama, Bunge, Polisi, Magereza, nk
Tanzania HATUTAKI VIINGOZI WENYE NGUVU tena Ila tunataka TAASISI ZENYE NGUVU