Rais Samia boresha kila kitu tutakusahau, ila ukimaliza mchakato wa Katiba tutakukumbuka milele

Rais Samia boresha kila kitu tutakusahau, ila ukimaliza mchakato wa Katiba tutakukumbuka milele

Hakuna kiongozi yoyote ambaye yuko tayari kuibadilisha katiba ili ajipunguzie madaraka.
Kwa Wazanzibari wote wamekuwa wakiamini kuwa Serikali ya Muungano inawanyonya na inawachelewesha kupata maendeleo, huu ndiyo wakati muafaka wao kufanya kweli. Kwa kuwa Rais wa Muungano ni Mzanzibari na Rais wa Muungano ni Mzanzibari pia
 
CCM hawataki KATIBA.
SI mama wala wajumbe, wana damu mikononi mwao, wanaogopa tume mbalimbali zilishatoa majibu hasa mauaji ya zanzibar, kifo cha akwilina , mtwara, kibiti na mizoga ya koko beach, hawawezi kubali.
Jana wamekubali mchakato wa katiba mpya uendelee
 
Unalilia katiba, lakini inaweza kubadilishwa kinyume na ulivokua unategemea na ukanyonywa zaidi. Cha msingi ni kuandaa wazalendo tu
Unawaandaaje wazalendo bila Katiba? Huoni hiyo inajenga kikundi cha madikteta kama wale kina Magufuli, Bashiru Ally, Polepole, Makonda, Sabaya?
 
J K Nyerere alikuwa Pan Africanist na hicho ndicho kilicho mpamanua dhidi ya wenzie kama akina Jomo Kenyatta au Milton Obotte. Miaka yote alifikiria kuunga mkono mapambano ya nchi zinazopigana na wakoloni.

Mwinyi alikuwa mwana Diplomasia mliberali na ndiyo maana akafungua milango ya uchumi wa soko huria miaka ya 1985-95 na kujipatia jina la Ruksa. Uanzishaji wa Madaladala na uuzwaji wa mitumba uliopo mpaka leo ni moja kati ya maamuzi yake bora kabisa.

Mkapa alikuwa Mwandishi na Mwana Diplomasia mbobezi na muumini wa uchumi wa sekta binafsi. Alijipambanua kwa ile sera ya "Uwazi na Ukweli" na tukaona magazeti na vituo vya TV na Radio binafsi vikishamiri. Na tukashudia na kasi kubwa ya kuuzwa kwa mashirika ya umma (privatisation). Ni baba wa mapinduzi ya uchumi huu wa kisasa tulionao.

Kikwette alikuwa Mwanasiasa aliyegeuka Mwana Diplomasia. Alibebwa na kauli ya "Maisha Bora kwa Watu Kila Mtanzania". Na kwa kusema ukweli alijitahidi kuwa kila mtu aweze kupata riziki kutokana na mazingira aliyopo. Tutamkumbuka kwa kupanua Uhuru wa maoni, demokrasia na usuluhishi wa migigoro kwa majadiliano.

Magufuli alikuwa ni Mkemia aliyejihuisha kuwa mhandisi wa miundombinu. Kwa miaka aliyohudumu kama Waziri kwenye Awamu ya Mkapa na Kikwette alijenga barabara barabara na madaraja mengi kuliko kiongozi yeyote. Hiyo ndiyo ilimpambanua na kuwa Rais wa miundombinu katika kipindi chake cha u-Rais kwa kauli yake ya "Hapa Kazi Tu". Aliona miundombinu ndiyo itakuwa chachu ya kujenga uchumi. Lakini kipindi chake kifupi kimeacha majeraha mengi kwenye haki za kiraia, Utawala bora, ukandamizaji demokrasia, utekwaji wa WAKOSOAJI, uwapo wa kikundi cha WASIOJULIKANA, dhuluma kwa wafanyabiashara kupitia TASK FORCE na mengine mengi.

Aidha ile kauli ya Baba wa Taifa mwaka 1982 kuwa "Katiba hii imenipa Madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu", ilijidhihirisha kipindi cha Magufuli.

Kimsingi kila Rais au kiongozi falsafa yake hujengwa na kile alichokifanya sana au kile kilichomjengea umaarufu.

Je Rais Samia Ni Nani?
Rais Samia ni Public Administrator ambaye amehudumu kama Waziri wa Mazingira na Muungano kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais kipindi cha Jakaya Kikwette.

Lakini hicho siyo kilichomjenga kuweza kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye Makamu wa Rais wa Tanzania kwenye awamu ya Magufuli.

Mwaka 2014 SSH alichaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge Maalum la Katiba (BMLK) chini ya Samuel Sitta (RIP). Hii kazi aliyoifanya kama Naibu Spika wa BMLK ndiyo imemjengea haiba aliyonayo.

SSH anaamini katika kufanya mambo kwa kufuata katiba, anaamini katika Utawala wa Sheria. SSH anataka kila Mtanzania atendewe haki, hapendi dhuluma kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa Taifa. Ana amini katika Uhuru wa vyombo vya habari na ukosoaji chanya. Ana amini katika ushirikiano wa kimataifa utakuza uchumi kupitia uwekezaji.

Kwa maoni yangu yote anayofanya Rais SSH ni mazuri lakini yasipowekwa kwenye MUSTAKABALI SAHIHI yatapotea.

Kitu pekee kitakacho yafanya mambo anayosimamia yabakie kuwa ya kudumu ni KUMALIZIA mchakato wa KATIBA, kile ambacho ndiyo kinajenga haiba yake.

Kwenye Ilani ya CCM ya 2015, kulikuwa na ajenda ya kumalizia mchakato wa KATIBA. Kwa hiyo CCM kama Chama kinataka Katiba mpya ya wananchi.

Bahati mbaya mtangulizi wake Magufuli hakunona kama ni KIPAUMBELE kwa kuwa haiba yake ilijengwa na miundombinu.

JK hakumaliza mchakato wa KATIBA mpya kwa sababu alikuwa DHAIFU (Hili tusibishane, kwa kuwa hata JJ Mnyika aliwahi kutamka Bungeni).

Nini Afanye Samia?
Anaweza kuwapata wataalamu wa Sheria na Katiba ambao siyo ndumila kuwili (kama Polepole + Kabudi) wakazi huisha Rasimu zile 2 ya Warioba na ya Sitta/ Chenge). Wakaangalia katika vipengele vinavyokinzana ni vipi vina masilahi mapana ya Taifa letu la Tanzania. Kisha wakaipeleka kwenye hatua ya REFERANDUM

Namsihi Rais SSH kama anapita humu JF au wasaidizi wake wamwambie kuwa Yeye ni Tunda la BMLK, na Tanzania itamkumbuka milele na milele kama atatuachia KATIBA mpya ya wananchi.

Atakumbukwa kwenye UKURASA mmoja na J K Nyerere hata kama atakaa kipindi kimoja cha miaka 5.

Afrika Kusini na Kenya wanafaidi matunda ya Katiba ya Wananchi. Kule tumeona namna Institutions zilivyo STRONG kuliko PERSONALITIES. Magufuli alikuwa VERY STRONG person akazizidi na Institutions zetu zote za Mahakama, Bunge, Polisi, Magereza, nk

Tanzania HATUTAKI VIINGOZI WENYE NGUVU tena Ila tunataka TAASISI ZENYE NGUVU
Sielewi hofu ya samia Suluhu nini Juu ya Mabadiliko ya Katiba. Hii inanifanya niamini kumbe na yeye ni walewale tu
 
Njia nzuri ya katiba ni kufanya AMENDMENT na katiba haitakiwi kuwa kana gazeti la zamani la mzalendo au kitabu cha ABBOTT au kitabu cha VINE AND REES cha plant and animal biology al maarufu kama mkate

Katiba ni ka kitabu kadogo saana
Sahihi
 
Back
Top Bottom