Rais Samia boresha kila kitu tutakusahau, ila ukimaliza mchakato wa Katiba tutakukumbuka milele

Pamoja na kumpamba mama hana mpango wa kubadili katiba.
labda ungetumia muda wako kuiomba CHADEMA wabadili katiba ili Mbowe awaachie na wengine.
 
Kwa mara hii inawezekana hasa kutoka kwa Wazanzibari ambao mara nyingi wanaongelea kuwa wanataka ZNZ yenye Mamlaka Kamili. Ni fursa ya ZNZ sasa kuweza kuifanya ZNZ isimame na ijipange kiuchumi
Samia ni rais, lkn she is free to excute her power to that extent.
 
Pamoja na kumpamba mama hana mpango wa kubadili katiba.
labda ungetumia muda wako kuiomba CHADEMA wabadili katiba ili Mbowe awaachie na wengine.
Kama huelewi maana ya kupata katiba mpya iliyo bora unabaki kuwa ni mzigo kwa taifa.
Haya malalamiko kuwa kila rais anakuja na mambo yake na kukosa dira kama taifa inatokana na kukosa katiba iliyo bora.
Vinginevyo wewe ni mbinafsi sana, au mnafki sana au hauna akili kabisa.
 
Sasa tueleze kwa nini CCM haitaki katiba ya wananchi,ina tatizo gani kubwa hadi CCM ihofie? si wana CCM ndio waliipitisha kwa nini hawataki kumalizia?
 
Wewe inaonekana kichwani kuna utupu. Watu wanaongelea katiba inayolinda maslahi ya umma na Taifa, wewe unaongelea mambo ya uchaguzi!! Hopeless kabisa. Badala ya kuwaza ustawi wa Taifa, unawaza uchaguzi. Mawazo mafupi kabisa.

Tunataka katiba itakayowahakikishia Watanzania na Taifa lao ustawi wa wakati wote, bila ya kujali nani ni Rais, anatoka chama gani. Tunataka umma uwe juu ya Serikali, juu ya Bunge na juu ya mahakama.

Katiba yetu hii mbovu, yeyote anayekuwa kiongozi, akitaka kuwa dikteta, hakuna atakayemdhibiti. Marehemu aliamua kuwa dikteta, nani aliweza kukohoa? Hata ndani ya CCM, hakuna aliyethubutu. Robo tatu ya wagombea ubunge walioshinda kwenye kura za maoni, aliwakata majina yao, nani aliweza hata kuhoji?

Tunataka katiba inayozuia mtu mmoja kufanya chochote atakacho, hata kama wananchi wote hawataki.
 
Hao ni vichwa vigumu, lakini tusikate tamaa kuwapa elimu ya bure mpaka waelewe
 
Straight Up Bams, umeliweka vizuri kiasi hata mbumbumbu ataelewa
 
Huyu mama bila kunipatia katiba mpya siwezi kumkumbuka kwa lolote, maana haya anayofanya ni ya kawaida tu hayana maajabu yeyote yale...

Ila akinipatia katiba mpya aaaa picha yake itakaa sebureni kwangu miaka nenda rudi. Na kila siku nitamwombea kwa Mungu apate maisha marefu.
 
Hitaji la haraka la watanzania si katiba mpya bali ni kujenga utengamano na mshikamano pasipo kuangalia itikadi ya siasa. Sisi ni watanzania kwanza kabla ya chote kile. Mchakato wa katiba utaishia kutugawa tena!!
 
Yote hayo yatapatikana ndani ya Katiba mpya ya wananchi
 
Pamoja na kumpamba mama hana mpango wa kubadili katiba.
labda ungetumia muda wako kuiomba CHADEMA wabadili katiba ili Mbowe awaachie na wengine.
Who are you kumsemea Mama?
 
CCM hawataki KATIBA.
SI mama wala wajumbe, wana damu mikononi mwao, wanaogopa tume mbalimbali zilishatoa majibu hasa mauaji ya zanzibar, kifo cha akwilina , mtwara, kibiti na mizoga ya koko beach, hawawezi kubali.
ccm si ndio nyie nyie
 
Sasa tueleze kwa nini CCM haitaki katiba ya wananchi,ina tatizo gani kubwa hadi CCM ihofie? si wana CCM ndio waliipitisha kwa nini hawataki kumalizia?
Wale wenye CCM wenyewe wanataka sana Katiba Mpya ya wananchi kwa kuwa hata wao wakati wa Mwendazake waligaragazwa sana
 
Katiba MPYA Ni token moja yenye maksi nyingi Sana

Atakaye komaa nayo atakumbukwa milele.

Abraham Lincoln alikuwa Rais wa 16 wa marekani lakini ndio RAIS maarufu kuliko wale wenzake wa kipindi kile na anakumbukwa Hadi leo

Alipitisha Sheria za kuwaachia watumwa

Aliiunganisha marekani iliyokuwa inataka kugawanyika sababu ya civil war baina Southerners and northerners .

Japo alitawala kipindi kidogo Sana muhula mmoja Ila alifanya akumbukwe. Hadi leo

Ukienda pale Washington DC Kuna bonge la monument/statue wamemjengea Ni phenomenal.
 
Mtanzanyika Huru umeliweka vizuri, hata hapa Kenya Mwai Kibaki anapata heshima kwa kuwezesha Katiba huru ya wananchi
 
Turudi hapa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…