Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora akaongee na wanahabariMambo ya ardhi ni very sensitive, atakua ameyatimba
Sijawahi kuipenda CCM Wala kuipigia kura ila huwa napenda baadhi ya viongozi na utendaji wao....umeelewa au ni wewe mmoja wapo kundi la wale ccm.baya unashangilia na zuri unashangilia ukisema kaupiga mwingi
Lakini Jamaa alikua anasisitiza kabisa,kua haya ni maelekezo ya Dr Samia amenituma nisimamie haki za watu, sasa kama kuna watu waliweka imani zaidi kwake hilo ni tatizo lao!!Muelekeo wa jamaa alikuwa maarufu kuliko namba moja.
Watu waliweka imani zaidi kwake kuliko
Vipi Lukuvi hamumtaki?Wizara ya ardhi ni sehemu mujarabu kwake... mafisadi wa ardhi walifanya na wanafanya sherehe ya huo utenguzi.
Alifanya kwa kiasi chakeVipi Lukuvi hamumtaki?
Ndg kwenye swala la haki kusimama,lazima upande mmoja ucheke,na upande mwingine ulie! Kwenye maridhiano ndiyo pande zote mbili mtacheka au wote mtalia! Kwa mfano umevamia kiwanja cha mtu ukajenga kwa documents fake, siku mwenye haki yake akija kuidai,ni wwe lazima utalia na mwenye kiwanja chake yeye atacheka!!Mama kamuokoa huyu, maana alikuwa anaenda kuongeza hasara ktk nchi...
Nchi yetu unaijua vizuri shida ni huyo atakae kuja sifikirii kama ataendeleza mapambano labda amteue Kafulila kuwa mbunge halafu ampe uwaziri wa ardhi.Kashaonyesha mfano kinachotakiwa aliyekaimu nafasi yake naye ni muda wa kuendeleza yaliyoachwa na mtangulizi wake.!!
Jerry yeye akapige kazi hiyo wizara mpya na kuleta mabadiliko.!!
Hao wahuni na wezi ni watu ni hatari sana....Katika vitu nilivyoshangaa ni huyo Slaa kuondoka Ardhi na pia inaonekana wahuni na wezi wana nguvu sana ya ushawishi...
Ni hatari kuliko maelezo wakitupia suti utajua ni watu aisee..Hao wahuni na wezi ni watu ni hatari sana....
Aliyatimba ' negatively ' kwa hao mafisadi wa ardhi. Lakini kwetu sisi watu wa kawaida alikuwa tumaini letu,Mambo ya ardhi ni very sensitive, atakua ameyatimba
Kweli kabisa lilikuwa tumaini la wanyongeAliyatimba ' negatively ' kwa hao mafisadi wa ardhi. Lakini kwetu sisi watu wa kawaida alikuwa tumaini letu,
Kama amefanya vema huko alipokuwa,basi ndiyo maana amehamishiwa kwingine ili aoneshe umahiri wake.Kumuacha mtendaji mmoja sehemu ileile moja kwa muda mrefu ni kudumaza akili,upeo na maamuzi yake.Basi,aachwe aoneshe/asambaze upendo.Sijawahi kuipenda CCM tangu uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi wa mwaka 1995 kipindi hicho nakumbuka nilikuwa darasa la tano.
Lakini nilikuwa navutiwa na utendaji wa baadhi ya viongozi wa serikali ya CCM katika idara mbalimbali mfano wa viongozi hao wa chache ni Lyatonga Mrema, Samuel Sitta, professor Mwandosya, Jaji Warioba, professor Asadi n.k
Turudi kwa Jerry Slaa sina haja ya kuweka maelezo mengi juu ya utendaji wake wa kazi katika wizara ya ardhi mimi ni miongoni mwa watu ambao tulikuwa tunamfuatilia kwa makini jinsi alivyokuwa anatimiza majukumu yake kutatua migogoro ya ardhi sehemu mbalimbali za nchi hii iliyodumu kwa miongo kadhaa iliyopita.
Kwa kweli wananchi maskini na wanyonge walipata haki zao zilizoporwa na mafisadi papa kwa kushirikiana na viongozi waliokosa uadilifu tena walifikia hadi kunajisi mahakama na 'documents' zao feki.
#Mama bring back Jerry Slaa wizara ya ardhi.
Pia soma > Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele
Samia huyu hajawahi muonea Mtanzania wa kawaida huruma' Eti amtume Jerry aende abomoe kituo cha mafuta 'shell' Eti sababu kimejengwa kwenye makazi ya watu. Hizo zilikuwa jitihada au kujiongeza binafsi za Jerry.Lakini Jamaa alikua anasisitiza kabisa,kua haya ni maelekezo ya Dr Samia amenituma nisimamie haki za watu, sasa kama kuna watu waliweka imani zaidi kwake hilo ni tatizo lao!!
Mkuu umenena sahihi kabisaaa.Samia huyu hajawahi muonea Mtanzania wa kawaida huruma' Eti amtume Jerry aende abomoe kituo cha mafuta 'shell' Eti sababu kimejengwa kwenye makazi ya watu. Hizo zilikuwa jitihada au kujiongeza binafsi za Jerry.
Ataona aibu kwa mambo aliyofanya mtangulizi wake…… TUMPE MUDANchi yetu unaijua vizuri shida ni huyo atakae kuja sifikirii kama ataendeleza mapambano labda amteue Kafulila kuwa mbunge halafu ampe uwaziri wa ardhi.