Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amehitimisha Mkutano Mkuu wa chama hicho kwa kutoa wito wa mshikamano na umoja miongoni mwa wanachama kuelekea kipindi cha uchaguzi.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu, Rais Samia amesema kuwa tayari hali inaonyesha ushindi kwa CCM, hivyo ni muhimu chama hicho kuingia kwenye uchaguzi kikiwa na nguvu moja na si makundi.
"Ukiangalia tu hali ilivyo, CCM tayari ilishashinda. Tuingie kwenye uchaguzi bila makundi," amesema Rais Samia.
Ameongeza kuwa kipindi cha uchaguzi ni nyeti na kinahitaji umoja, mshikamano na upendo ndani ya chama, hasa ikizingatiwa kwamba kutakuwa na ushindani wa kugombea nafasi mbalimbali, jambo ambalo linaweza kusababisha makundi.
"Tutakapoanza kugombea kutakuwa na makundi, hilo ni la kawaida. Lakini baada ya mchakato huo, tuhakikishe chama kinabaki kuwa kimoja. Tuingie kwenye uchaguzi tukiwa na nguvu moja, si kwa mapande mapande," amesisitiza.