benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Katika kilele cha Kongamano la kumbukizi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa, Rais Samia alionesha waziwazi kukerwa na tabia ya watendaji wa juu, vigogo, Mabosi wa idara, mashirika na taasisi mbalimbali za Serikali kuwazungusha wawekezaji wanaofika nchini kutaka kuwekeza jambo linalowakatisha tamaa wawekezaji hao na baadhi kuhamishia mitaji yao katika nchi nyingine.
Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumzia hili hasa akisisitiza umuhimu wa kuishirikisha Sekta binafsi katika kutoa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi.
Mara kadhaa amekuwa akiahidi kuchukua hatua kwa watendaji katika Serikali anayoiongoza watakaokwamisha wawekezaji lakini nadhani ni muda sasa akakunjua makucha yake na kuwashugulikia wale wanaokwamisha wawekezaji hawa.
Rais Samia alitoa mfano wa Wawekezaji waliokuja nchini kutaka kuwekeza katika Sekta ya afya kwa kufunga mitambo ya vipimo vya afya katika maeneo mbalimbali ya nchi lakini hakuna aliyewasikiliza, sio Wizara ya Afya, mikoani, wilayani wala mamlaka zinazohusika na uwekezaji
Umefika wakati sasa tuone hatua zikichukuliwa, kigogo anayekwamisha mradi wa afya kwa kuwa yeye na familia yake wana uhakika wa kutibiwa nje ya nchi katika hospitali kubwa kwa gharama yoyote sio wa kufumbiwa macho, huyu ndio anapelekea vifo vya Mama na mtoto kule kijijini, huyu nddiye anasababisha ndugu zetu wanasafiri umbali mrefu kufuata vipimo vya afya. nk.
UMEFIKA MUDA MAKALI YA NYEMBE YAKATE KUCHA ZILIZOZIDI UREFU KWANI ZINAFICHA UCHAFU NA VIJIDUDU VINAVYOSABABISHA MAGONJWA NA PENGINE SIKU MOJA VITASABABISHA KIFO.
Nawasilisha: