Mh.Raisi Mimi ni mmoja wa watu ambao walipinga waziwazi hatua zilizpchukuliwa na Raisi aliyepata kwenye kupambana na suala la Corona.
Ulipokuja wewe ulionyesha seriousness kwenye suala hili na tunakupongeza sana.
Umeshauriwa na wataalamu vizuri kuhusu hili janga na umewasikiliza na hata juzi tumeona ukisema wimbi la tatu lipo na limeshaingia nchini na wagonjwa wapo.
Mama Samia sasa hivi kwenye shughuli zako nyingi unavaa barakoa hata kwenye vikao vya ndani umeonyesha kuchukua tahadhali kwako na kwa wanaokuzunguka.
Jana ulitoa tena ujumbe kama raisi kuwaasa wananchi kuwa ni lazima wachukue tahadhari kuepuka ugonjwa wa corona ikiwapo kuzuia mikusanyijo isiyo ya lazima, kugusana, kuvaa barakoa, kupaka sanitizer na mengine mengi ILA
Nimeshindwa kuelewa tena imekuwaje umempigia simu msanii Nandy na kumpongeza kufanya tamasha la Nandy festival dodoma na ukaonyesha shauku ya ungependa kuwepo.
Bado nachanganyikiwa hapa, kwanza ilippaswa uzuie hata Hilo tamasha kufanyika kwa sababu ni wewe ulisema kuna wimbi la tatu la corona na kutoa tahadhari zote.
Ni kweli Kuna kitu hakipo sawa juu ya suala hili la corona? Unapiga simu kuongeza tamasha ambalo watu wamesongamana na hakuna hatua zozote za kujilinda na corona?
Nilitegemea ungewawajibisha watu walioruhusu hili tamasha kufanyika kipindi hiki ambacho Kuna wimbi la tatu.
Nchi ni ngumu sana hii kwa kweli.