Rais Samia: Demokrasia siyo Cocacola

Kwa maana hiyo hata UDIKTETA ni 'DEMOKRASIA'?

Anaelewa anachikizungumzia?

Kama kweli rais kayasema haya, anatofauti gani na hawa watu waliomo humu JF kama akina Johnthebabtist, Magonjwa, Etwege, na wengineo wa aina hiyo?
Kumbe kubambika kesi na kuteka ni demokrasi!
 
Kila nchi ina demokrasia yake....

Demokrasia huendana na MILA NA TARATIBU ZA WATU....

Kwa kuwa demokrasia ni suala huria ndio waarabu na waafrika tuwe na sheria za ndoa za jinsia moja?!!!

Kwani nayo ndio demokrasia hiyo ya nchi za MAGHARIBI.....
Kumbe kuteka na kubambika kesi ni mila na demokrasi!
 
Hivi rais wetu mama Samia Suluhu Hassan na aliekuwa rais mwanamke wa Liberia Johnson Salif (sikumbuki spellings) Nani mwenye busara? Tukiwapima
 
Ndio kwa mara ya kwanza nasikia demokrasia zinatofautiana kutegemea na nchi uliyopo...

Maana tulipofunzwa katika somo la Uraia na baadaye Civics, tulifunzwa demokrasia ni moja na hata mifano iliyotumika kama vielelezo ilitumia demokrasia iliyohubiriwa nchi za magharibi...
 
Asiige misemo ya Nyerere. Maana huyo pia anamchango mkubwa wa kutufikisha kwenye hii kadhia tuliyopo. Kwasababu ya fikra na imani hizo, sasahivi wananchi wanapambana kujikomboa mara ya pili.
Na hatari kubwa aliyonayo ni kuishia kuonekana kilaza. Nyerere alikuwa smart kichwani. Alijua jinsi ya “kuzungusha” maneno kisomi na kuacha watu wanachambua hadi kuchanganyikiwa.
 
Watokee wapi?!!

Kauli ya mwenyekiti wetu ndiyo ya mwisho....

Huu ni utaratibu wa CCM.....si lazima ufanane na MWINGINE popote pale.....

#SiempreCCM
Mkuu salute. Unaitendea haki zamu yako ya ulinzi wa kasri. Bia yetu, kawe alumni na msemaji ukweli hawakufikia viwango kabisa.
 
Kila nchi ina demokrasia yake....

Demokrasia huendana na MILA NA TARATIBU ZA WATU....

Kwa kuwa demokrasia ni suala huria ndio waarabu na waafrika tuwe na sheria za ndoa za jinsia moja?!!!

Kwani nayo ndio demokrasia hiyo ya nchi za MAGHARIBI.....
Sikukutaja tu kwenye listi hiyo ya wapuuzi, lakini wewe pia ni hao hao wapuuzi, ushahidi ukiwa hao uliyoandika hapo juu na michango karibu yote unayoandika humu JF.
 
Mtemi Hangaya Yuko sawa kabisa.
Kumbe huyu mama ni chuma Cha pua kwa wapinzani.
 
Kwani demokrasia haianzii ngazi ya familia na ndani ya vyama?!!
Akili yako ilivyo finyu unajisikia umejibu hoja kwa jibu zito sana.
Kama ni hivyo, hakuna sababu ya kuwepo na sheria nchini, na hatutahitaji katiba kama mnavyoimba kila siku. Kumbe yoite haya ni ufinyu wa akili.
Na sidhani kuwa utaelewa nilichokuandikia hapa.
 
Kumbe kubambika kesi na kuteka ni demokrasi!
Inaelekea 'Maza Mizinguo' anaamini hivyo.
Sasa hivi kaanza kampeni za kuendelea kushika madaraka, bila ya kuchaguliwa na kura za wananchi hapo 2025; hiyo yeye anaiona kuwa ni demokrasia kwa vile CCM wameifanya iwe ni 'jadi' ya Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…