Rais Samia: Dereva aliyeamua kuliingiza lorry kwenye korongo kwa kukwepa utelezi

Rais Samia: Dereva aliyeamua kuliingiza lorry kwenye korongo kwa kukwepa utelezi

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Hakuna kazi hata moja iliyowahi kukosa changamoto. Iwe ni Urais, Uwalimu, Udaktari, Ukulima, Biashara na Uwekezaji, Udereva, Uhandisi, Uchungaji au Ushekhe, Uwanafunzi, au nyingine yoyote, isiyo na changamoto, japo uwingi na uzito wa changamoto hutofautiana.

Na wanaofanikiwa, siyo watu wanaokosa changamoto, bali ni watu wenye kutafuta majibu sahihi ya changamoto zinazowakumba.

Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoanguka, ni uwezo wa kutafuta majibu ya changamoto, zinapojitokeza. Kwenye utatuzi wa changamoto, kuna makundi matatu:

1) Wapo ambao wakipata tu changamoto, hawatafuti majibu ya changamoto, hunyosha mikono na huishia hapo hapo. Hawa huwa wafu wa mafanikio.

2) Wapo wanaotafuta suluhu za mkato, wakakosa hekima, maarifa, ujuzi na tafakari, huishia kutafuta suluhu za changamoto ambazo huleta madhara mabaya zaidi hata kuzidi changamoto walizotaka kuzitatua.

3) Wapo wanaotafuta suluhisho la changamoto zinazowakumba, hutafuta suluhisho sahihi, huzivuka changamoto, na huibuka wakiwa washindi. Hawa ndio watu wenye mafanikio siku zote.

Bahati Mbaya, Rais wetu Samia Suluhu Hassan, anaangukia kwenye kundi ka pili. Yaani mtu anayetafuta suluhisho la matatizo kwa kuzalisha matatizo makubwa zaidi maradufu ya tatizo analotaka kulitatua. Amekuwa kama dereva wa lorry lililobeba shehena kubwa ya mzigo wenye thamani kubwa, linalopanda mlima wenye utelezi ambao upande mmoja wa barabara ni mlima mrefu, na upande wa pili ni gema refu kuelekea korongoni (sawa na yale makorongo ya milima ya Lukumburu, kama unaelekea Songea). Mlima una utelezi, dereva anawaomba watu walisukumie lorry kwenye korongo refu ili kuukwepa utelezi. Na kwa kufanya hivyo anaamini ametatua tatulizo la kuupanda mlima wenye utelezi, asijue kuwa kwa kusukumia lorry korongoni, ameliua lorry, ameteketeza shehena yenye thamani, na lorry halitaweza kuendelea na safari.

Kuna tatizo kubwa kwenye mkataba wa bandari wa DP, ambalo ni uhovyo na ushenzi wa mkataba. Rais Samia haumizwi na ubovu wa mkataba, anaumizwa na sauti za wanaolalamikia uhovyo wa mkataba. Hahangaiki na kutatua uhovyo wa mkataba, bali anahangaika kuzima sauti za wanaolalamikia mkataba wa hovyo. Kwake kuwakamata Dr. Slaa, Mwambukusi na Mdude na kuwabambikia kesi za uhaini anaona ametatua tatizo la kusikia kelele zinazokosoa uhovyo wa mkataba. Hajui wala hatambui kuwa kwa kufanya hivyo anatengeneza matatizo makubwa zaidi dhidi yake na Serikali yaje kuliko hata uhovyo wa mkataba. Sasa afahamu kuwa:

1. Kelele dhidi ya mkataba wa kishenzi wa DP, zitaongezeka kutoka ndani ya nchi.

2) Kelele dhidi ya udikteta wa utawala wake zimeanza kutoka ndani ya nchi na jamii ya kimataifa. Tayari Amnesty International wamelaani maamuzi yake, Human Rights Watch wamepaza sauti dhidi ya utawala wake. Siku si nyingi kutakuwa na kauli toka Jumuiya ya Ulaya na Marekani.

3) Taasisi zote ambazo hutoa misaada na mikopo kwa sharti nchi iwe na mfumo wa utawala unaoheshima demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu, hazitatoa msaada wala mkopo kwa Serikali ya Samia. Ni suala la wakati tu.

4) Hata ambao hawakuwahi kujua uhovyo wa mkataba wa DP, watafahamu sasa kutokana na hizo kesi za kubambikia watu, na matamko ya taasisi za jamii ya kimataifa.

5. Uchumi ambao tayari ni legelege utalegea zaidi kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo unaweza kubambikiwa kesi na Serikali wakati wowote.

Rais Samia badala ya kutafuta msaada wa kusukuma gari liupite utelezi, ametafuta watu wa kumsaidia kulisukumiza lorry korongoni.
 
Halafu ajabu licha ya kutupekeka korongoni, anataka abiria tunyamaze tusilalamike, au wale watakaotaka kuongea, basi wampongeze!

Hiyo ndio mindset inayotuongoza kwa sasa, mjinga ameshika usukani, alipoambiwa anapotupeleka sipo, akatujibu ameziba masikio, sasa ametumwaga korongoni, anataka tumshangilie, tukigoma anatoa adhabu kwetu.
 
sio kweli!
ndo angepewa u-Dr?
Udokta wa kupewa hauangalii kiwango cha elimu, bali ulichofanya. Unapewa tu kama chuo kinachokupa kimetufhishwa na jambo fulani ulilolitenda.

Na hivi vyuo vya Serikali, mkuu wa Serikali anaweza kupewa hata bila ya kufanya jambo lolote la maana.

Nchi za watu makini, vyuo vya setijali huwa havitoi huo udokta kwa Rais wa nchi yao, mara nyingi hutoa kwa viongozi wa mataifa mengine inapodhihirika kiongozi huyo amefabya mambo makubwa.
 
Back
Top Bottom