Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unamaanisha kukwepa utelezi na kuingiza korobgoni?Neno la mwisho la heading ni tata kidogo.
Anasema watu watulie eti nchi haijauzwa anaihangaikia na kuitafutia pesa nje ya nchiHalafu ajabu licha ya kutupekeka korongoni, anataka abiria tunyamaze tusilalamike, au wale watakaotaka kuongea, basi wampongeze!
Hiyo ndio mindset inayotuongoza kwa sasa, mjinga ameshika usukani, alipoambiwa anapotupeleka sipo, akatujibu ameziba masikio, sasa ametumwaga korongoni, anataka tumshangilie, tukigoma anatoa adhabu kwetu.
kwa mama zakaria au ujiji ?Mwananyamala
Daaah!!Neno la mwisho la heading ni tata kidogo.
Haimhusu !!Mwenye machungu na bandari ambayo ht haikuhusu
Pesa ziko humu humu. Geita gold, kahama gold, sijui Mara gold hizi Ni pesa tumezigawa kwa wazungu. Bado Kuna zile tunawapa wazungu bure Kama fidia ya mikataba ambayo tunasaini huku tunakunywa wiski.Anasema watu watulie eti nchi haijauzwa anaihangaikia na kuitafutia pesa nje ya nchi
Inawezekana kabisa hii move ni ya "tengeneza tatizo,halafu litatue,kesho unaonekana wewe ndiye bingwa" kwa ajili ya 2025.President Samia is putting herself on fire, to keep herself warm. What a hilarious predicament!
kama darasa la Saba Msukuma amepewa udr itakuwaje Kwa form four failure?sio kweli!
ndo angepewa u-Dr?
Usitukane mkuuMahakama yamehitisha suala la Bandari lakini wewe unaendeleza porojo! Yaani unapingana na mahakama halali.
Kenge wewe
Samia kabadilika sana siku hizi.Hakuna kazi hata moja iliyowahi kukosa changamoto. Iwe ni Urais, Uwalimu, Udaktari, Ukulima, Biashara na Uwekezaji, Udereva, Uhandisi, Uchungaji au Ushekhe, Uwanafunzi, au nyingine yoyote, isiyo na changamoto, japo uwingi na uzito wa changamoto hutofautiana.
Na wanaofanikiwa, siyo watu wanaokosa changamoto, bali ni watu wenye kutafuta majibu sahihi ya changamoto zinazowakumba.
Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoanguka, ni uwezo wa kutafuta majibu ya changamoto, zinapojitokeza. Kwenye utatuzi wa changamoto, kuna makundi matatu:
1) Wapo ambao wakipata tu changamoto, hawatafuti majibu ya changamoto, hunyosha mikono na huishia hapo hapo. Hawa huwa wafu wa mafanikio.
2) Wapo wanaotafuta suluhu za mkato, wakakosa hekima, maarifa, ujuzi na tafakari, huishia kutafuta suluhu za changamoto ambazo huleta madhara mabaya zaidi hata kuzidi changamoto walizotaka kuzitatua.
3) Wapo wanaotafuta suluhisho la changamoto zinazowakumba, hutafuta suluhisho sahihi, huzivuka changamoto, na huibuka wakiwa washindi. Hawa ndio watu wenye mafanikio siku zote.
Bahati Mbaya, Rais wetu Samia Suluhu Hassan, anaangukia kwenye kundi ka pili. Yaani mtu anayetafuta suluhisho la matatizo kwa kuzalisha matatizo makubwa zaidi maradufu ya tatizo analotaka kulitatua. Amekuwa kama dereva wa lorry lililobeba shehena kubwa ya mzigo wenye thamani kubwa, linalopanda mlima wenye utelezi ambao upande mmoja wa barabara ni mlima mrefu, na upande wa pili ni gema refu kuelekea korongoni (sawa na yale makorongo ya milima ya Lukumburu, kama unaelekea Songea). Mlima una utelezi, dereva anawaomba watu walisukumie lorry kwenye korongo refu ili kuukwepa utelezi. Na kwa kufanya hivyo anaamini ametatua tatulizo la kuupanda mlima wenye utelezi, asijue kuwa kwa kusukumia lorry korongoni, ameliua lorry, ameteketeza shehena yenye thamani, na lorry halitaweza kuendelea na safari.
Kuna tatizo kubwa kwenye mkataba wa bandari wa DP, ambalo ni uhovyo na ushenzi wa mkataba. Rais Samia haumizwi na ubovu wa mkataba, anaumizwa na sauti za wanaolalamikia uhovyo wa mkataba. Hahangaiki na kutatua uhovyo wa mkataba, bali anahangaika kuzima sauti za wanaolalamikia mkataba wa hovyo. Kwake kuwakamata Dr. Slaa, Mwambukusi na Mdude na kuwabambikia kesi za uhaini anaona ametatua tatizo la kusikia kelele zinazokosoa uhovyo wa mkataba. Hajui wala hatambui kuwa kwa kufanya hivyo anatengeneza matatizo makubwa zaidi dhidi yake na Serikali yaje kuliko hata uhovyo wa mkataba. Sasa afahamu kuwa:
1. Kelele dhidi ya mkataba wa kishenzi wa DP, zitaongezeka kutoka ndani ya nchi.
2) Kelele dhidi ya udikteta wa utawala wake zimeanza kutoka ndani ya nchi na jamii ya kimataifa. Tayari Amnesty International wamelaani maamuzi yake, Human Rights Watch wamepaza sauti dhidi ya utawala wake. Siku si nyingi kutakuwa na kauli toka Jumuiya ya Ulaya na Marekani.
3) Taasisi zote ambazo hutoa misaada na mikopo kwa sharti nchi iwe na mfumo wa utawala unaoheshima demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu, hazitatoa msaada wala mkopo kwa Serikali ya Samia. Ni suala la wakati tu.
4) Hata ambao hawakuwahi kujua uhovyo wa mkataba wa DP, watafahamu sasa kutokana na hizo kesi za kubambikia watu, na matamko ya taasisi za jamii ya kimataifa.
5. Uchumi ambao tayari ni legelege utalegea zaidi kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo unaweza kubambikiwa kesi na Serikali wakati wowote.
Rais Samia badala ya kutafuta msaada wa kusukuma gari liupite utelezi, ametafuta watu wa kumsaidia kulisukumiza lorry korongoni.
Kuna watu inaonekana wamedhamiria sana kuhakikisha Samia anakuwa Rais wa nusu mhula tu. Na hao wamekazana sana kuhakikisha kila siku idadi ya wanaomchukia Rais inaongezeka.Inawezekana kabisa hii move ni ya "tengeneza tatizo,halafu litatue,kesho unaonekana wewe ndiye bingwa" kwa ajili ya 2025.
Pia inawezekana kuna "mafundi" wameweka switch ya taa "upside down" kwa ajili ya 2025.
Hiyo PHD kasomea chuo gan?sio kweli!
ndo angepewa u-Dr?