Rais Samia: Dereva aliyeamua kuliingiza lorry kwenye korongo kwa kukwepa utelezi

Rais Samia: Dereva aliyeamua kuliingiza lorry kwenye korongo kwa kukwepa utelezi

Sikiliza wewe uliyekosa adabu na akili.kwa Taarifa yako ni kuwa Rais samia ndiye Rais bora kabisa tuliye naye kwa sasa katika Bara hili la Afrika kwa sasa ni kiongozi wa mfano na kuigwa ,ni kiongozi anayeishi mbele ya wakati na mwenye maono ya mbali. Ni kwa ushujaa wake na upeo wake mkubwa wa kimaono na kiuongozi ndiyo maana ametuvusha kama Taifa katika nyakati zote ngumu ambazo Dunia imezipitia na kutetemeshwa ,lakini Rais samia alisimama imara na kutuvusha
Sawa ngiri maji Dollar ikifika 5000 ndo utajua anaishi mbele ya maono au amekalia maono ,
 
Huelewa hata maana ya uchumi dhaifu. Una upeo mdogo sana katika mambo mengi. Nikupe mfano mdogo unaoendana na kiwango chako cha uelewa:

Fikiria kuna watu wawili:

Mtu wa kwanza, mwakajana alitengeneza mapato ya shilingi bilioni 10. Mwaka huu ametengeneza mapato ya shilingi bilioni 10 na milioni 100. Hivyo ongezeko la mapato yake ni mioni 100 ambayo ni 1%.

Mtu wa pili, mwakajana alitengeneza mapato ya ni shilingi milioni 2. Mwaka huu ametengeneza pato la shilingi milioni 2 na laki 1. Hivyo ameongeza pato lake kwa shilingi laki. Hili ni ongezeko la 5%.

Ukija kwenye uhalisia, licha ya huyu wa pili kupata ongezeko la 10%, bado ni maskini, bado yupo mbali sana kutoka kwa huyu wa kwanza mwenye ongezeko la 1%.

Ongezeko la mtu wa kwanza ni 1%, katika figure ni milioni 100.
Wa pili ana ongezeko la 5% lakini katika figure ni laki 1. Kwenye uhalisia, ongezeko la huyu wa pili, kwa sababu uchumi wake ni dhaifu sana, ni 0.1% ya ongezeko la huyu wa mwanzo.

Tanzania, nchi ambayo wastani wa pato lake ni kama dola 1,000 tu kwa mwaka, ni nchi maskini, yenye uchumi dhaifu na duni, ukilinganisha hata na baadhi ya nchi za Afrika ambazo zina uchumi nafuu:

Mauritius $10,134
Botswana $6,910
Namibia $5,100
Gabon $8,635
Seychelles 14,653


TANZANIA
Uv ccm hawana akili ya maana zaidi ya kusifia matope ya bibi yao ,ndo kiapo walicholishwa usiiumize kichwa kuelemisha watu wajinga kama huyo
 
Katiba ya hovyo, Ingetakiwa sasa awe Jambiani akiwalea wajukuu.

Han uwezo w ku-deal na changamoto kutoa kauli, kuongoza Taifa.
Hili ukilisema utasikia nani kama mama rais asiwezia kutumia hata 1% kutatua changamoto zetu badala ya anafikiria vitu vyepesi vyepesi ,tu kuna siku hata wanaomtetea watachoka kwa kweli
 
Hakuna kazi hata moja iliyowahi kukosa changamoto. Iwe ni Urais, Uwalimu, Udaktari, Ukulima, Biashara na Uwekezaji, Udereva, Uhandisi, Uchungaji au Ushekhe, Uwanafunzi, au nyingine yoyote, isiyo na changamoto, japo uwingi na uzito wa changamoto hutofautiana.

Na wanaofanikiwa, siyo watu wanaokosa changamoto, bali ni watu wenye kutafuta majibu sahihi ya changamoto zinazowakumba.

Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoanguka, ni uwezo wa kutafuta majibu ya changamoto, zinapojitokeza. Kwenye utatuzi wa changamoto, kuna makundi matatu:

1) Wapo ambao wakipata tu changamoto, hawatafuti majibu ya changamoto, hunyosha mikono na huishia hapo hapo. Hawa huwa wafu wa mafanikio.

2) Wapo wanaotafuta suluhu za mkato, wakakosa hekima, maarifa, ujuzi na tafakari, huishia kutafuta suluhu za changamoto ambazo huleta madhara mabaya zaidi hata kuzidi changamoto walizotaka kuzitatua.

3) Wapo wanaotafuta suluhisho la changamoto zinazowakumba, hutafuta suluhisho sahihi, huzivuka changamoto, na huibuka wakiwa washindi. Hawa ndio watu wenye mafanikio siku zote.

Bahati Mbaya, Rais wetu Samia Suluhu Hassan, anaangukia kwenye kundi ka pili. Yaani mtu anayetafuta suluhisho la matatizo kwa kuzalisha matatizo makubwa zaidi maradufu ya tatizo analotaka kulitatua. Amekuwa kama dereva wa lorry lililobeba shehena kubwa ya mzigo wenye thamani kubwa, linalopanda mlima wenye utelezi ambao upande mmoja wa barabara ni mlima mrefu, na upande wa pili ni gema refu kuelekea korongoni (sawa na yale makorongo ya milima ya Lukumburu, kama unaelekea Songea). Mlima una utelezi, dereva anawaomba watu walisukumie lorry kwenye korongo refu ili kuukwepa utelezi. Na kwa kufanya hivyo anaamini ametatua tatulizo la kuupanda mlima wenye utelezi, asijue kuwa kwa kusukumia lorry korongoni, ameliua lorry, ameteketeza shehena yenye thamani, na lorry halitaweza kuendelea na safari.

Kuna tatizo kubwa kwenye mkataba wa bandari wa DP, ambalo ni uhovyo na ushenzi wa mkataba. Rais Samia haumizwi na ubovu wa mkataba, anaumizwa na sauti za wanaolalamikia uhovyo wa mkataba. Hahangaiki na kutatua uhovyo wa mkataba, bali anahangaika kuzima sauti za wanaolalamikia mkataba wa hovyo. Kwake kuwakamata Dr. Slaa, Mwambukusi na Mdude na kuwabambikia kesi za uhaini anaona ametatua tatizo la kusikia kelele zinazokosoa uhovyo wa mkataba. Hajui wala hatambui kuwa kwa kufanya hivyo anatengeneza matatizo makubwa zaidi dhidi yake na Serikali yaje kuliko hata uhovyo wa mkataba. Sasa afahamu kuwa:

1. Kelele dhidi ya mkataba wa kishenzi wa DP, zitaongezeka kutoka ndani ya nchi.

2) Kelele dhidi ya udikteta wa utawala wake zimeanza kutoka ndani ya nchi na jamii ya kimataifa. Tayari Amnesty International wamelaani maamuzi yake, Human Rights Watch wamepaza sauti dhidi ya utawala wake. Siku si nyingi kutakuwa na kauli toka Jumuiya ya Ulaya na Marekani.

3) Taasisi zote ambazo hutoa misaada na mikopo kwa sharti nchi iwe na mfumo wa utawala unaoheshima demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu, hazitatoa msaada wala mkopo kwa Serikali ya Samia. Ni suala la wakati tu.

4) Hata ambao hawakuwahi kujua uhovyo wa mkataba wa DP, watafahamu sasa kutokana na hizo kesi za kubambikia watu, na matamko ya taasisi za jamii ya kimataifa.

5. Uchumi ambao tayari ni legelege utalegea zaidi kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo unaweza kubambikiwa kesi na Serikali wakati wowote.

Rais Samia badala ya kutafuta msaada wa kusukuma gari liupite utelezi, ametafuta watu wa kumsaidia kulisukumiza lorry korongoni.
Wivu tu tunataka mkataba tunataka DP World apewe bandari
 
Back
Top Bottom