PreGE2025 Rais Samia elewa No reform maana yake ni damu za Watanzania

PreGE2025 Rais Samia elewa No reform maana yake ni damu za Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Kuna watu hapa Machawa wanamdanganya huyu Raisi Samia. Raisi Samia kukitokea umwagaji damu hapa wakulaumiwa sio machawa maana watajikausha, Mchimbi ndiyo kabisa ataona nafasi yake ya kung’ara, Kikwete hata simu yako hata pokea. Maana yake ni kwamba mambo yakiwa mabaya utabaki wewe peke yako.

Ni madai gani hasa, pesa gani hasa , kunufaisha gani hasa kunakuzuia kiasi kwamba uko tayari kuuwa Watanzania kuliko kuwapa haki tu za kupiga kura na kuwachagua viongozi wawapendao! Pamoja na wizi kwenye mikataba pesa Dubai na makampuni uliyonayo unataka ukistaafu tukukumbuke kwa wizi na mauaji au tuku kumbuke kwa maendeleo na haki kwa wananchi?

Tunao kupenda tunasema usisikilize machawa fuata nafsi yako. Bila reform za maana kuna uwezekano kanisa wa damu kumwagika na kila damu ya mtu mmoja kwa Mungu wewe ndiye utakuwa muuaji sio Polisi wala usalama wa taifa maana mazingira wewe ndiye umeyaweka.

Huwezi kumlaumu Lissu ambaye yeye anataka chaguzi huru sasa hata kwa mungu anakosa gani? Na kushauri fanya reform tena reform kubwa.
 

Attachments

  • IMG_2995.jpeg
    IMG_2995.jpeg
    99.5 KB · Views: 30
Tuliza matako we bwege, km una hamu ya kumwaga damu nenda Sudan au Gaza. We ni wale wachawi wanaokunywa damu za watu.
 
Back
Top Bottom