Rais Samia, fanya mabadiliko ya wasaidizi wako hasa Kwenye hotuba; unaweza ukawa na wasomi ila siyo wataalam wala wazoefu

Of course inakuaje watu hawajiridhishi na hotuba ya Rais kabla ya kuitoa public?

Rais mfute Kazi mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu..hii dola za Marekani bilioni 6,250 ni pesa ambayo inazidi GDP yote ya Africa..

Makosa yapo ila kujirudia rudia sio sawa,hapo ilitakiwa isomeke dola za Marekani milioni 6,250 sawa na Shilingi til.14 na bil.600 .
 
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete walikuwa vipanga darasani.

Mwendazake na huyu sijajua historia zao za darasani zilikuwaje.

Hata kama unaandikiwa, inabidi personaly uwe vizuri kichwani, ukipitia ulichoandikiwa unapaswa kugundua nyufa mwenyewe.
Hii hotuba ya mama ningeambiwa niipe maksi kati ya 100 ningeipa 10 tena kishingo upande.
 
Ikulu na Utopolo vimeumana mwasilishaji na msomaji kedekedeee macho mzuri macho mzuri halaa halaaa ololooo olooo eee iyena!!! Oooh sana
 
Salamu za mwaka mpya haziwezi kuwa hotuba ndefu yenye maudhui kama hotuba ya mpango wa maendeleo. Tuache kulaumu laumu kila kitu.
 
Hivi Magufuli alikuwa akihutubia Taifa mwaka mpya na kueleza malengo ya serikali kwa mwaka unaofuata?Mwingine anasema eti hotuba ya jana ilitakiwa itoe mwelekeo wa bajeti ijayo!Duh ,kweli kazi ipo
 
Hivi Magufuli alikuwa akihutubia Taifa mwaka mpya na kueleza malengo ya serikali kwa mwaka unaofuata?Mwingine anasema eti hotuba ya jana ilitakiwa itoe mwelekeo wa bajeti ijayo!Duh ,kweli kazi ipo
Kwenye hotuba Magufuli ndiyo hakuwapo kabisa, na akihutubia ni matusi matupu. Let's appreciate kinachofanywa na Samia
 
Hivi iliwezekana vipi nchi kumpata Rais wa hovyo kama huyu?!
Your browser is not able to display this video.
 
Ukijua kazi ya akiba hautaongea tena hizo pumba zako
Mkuu pole, ila kwa taarifa yako tu dola bilioni 6153 alizosema mama kuwa Tanzania inazo ni pesa nyingi sana na hatujawahi kuwa na kiasi hiko tangu tukiwa british teritory mpaka sasa tukiwa free state..
 
Aisee kwanini unatumia Picha yangu kwenye Profile yako
 
Acheni kumpangia Rais SSH mambo ya kuongea. Kwanza ni hiari yake kuongea na wananchi wala siyo takwa la Katiba. Hakuna Marais 2 wanaoshabihiana kuanzia J K Nyerere hadi Magufuli juu ya kuongea mwisho wa mwaka.

Hata angesema "Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya" tu ingetosha.

Yale aliyoyaainisha ndiyo aliyoyaka tusikie. Hayo ya kwako sambulugu kawasomee wanao sebuleni kwako.
 

Mkuu tupe kwanza mipango yako ya familia . Uliyoyapanga na kufanikiwa na yajayo. Ukiwa nje ya ngoma unaona mambo rahisi sana. Gombea tukupe.
 
Mama katoa tango pori LA mwaka 2022, Nchi Ina hakiba ya bil 6253, na Yuko serious anasoma hotuba, hata kushituka hawezi, tuna Rais mweupe kichwani balaa toka tupate Uhuru, watanzania tumepatikana, Rais hajui chochote kuhusu nchi yake aibu iliyoje hii.
 
Rais anapokuwa muwasiliniaji(communicator) mzuri inasaidia kufunika mapungufu mengine.

Wema, upendo, upole, unyenyekevu, uadilifu n.k ni sifa nzuri lakini zisipowasilishwa vizuri kwa watu zinabakia kuwa vitu vya kufikirika tu badala ya kuchangia katika kuongeza mvuto wa kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…