Rais Samia, funga mwaka iliyofanywa Serikalini ni balaa

Rais Samia, funga mwaka iliyofanywa Serikalini ni balaa

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Mhe Rais nadhani huu Ni muda sahihi wakujua ni mteule yupi uliyemteua anaishi fikra zako na yupi anaishi fikra za tumbo lake na familia yake. Watumishi wachache wa Umma wamegawana kumbi za Serikali na hoteli kwa vikao ambavyo sidhani Kama vina tija.

Mhe. Wazir Mkuu alitumbua watendaji wa wizara ya fedha kwa kujilipa mamolioni ya fedha. Watu wamemdharau na Leo hii wizara na idara za serikali ambazo zote zipo Dodoma wamehamia mikoani kufanya vikao.

Fedha hii wanayogawana ingesambazwa kwenye huduma lipo Jambo ungetatua.

Nikuombe bila kutumbua omba taarifa ya kila wizara wamefanya vikao vya kazi au semina ngapi kwa mei na Juni na majina ya washiriki. Utagundua wapo watu wamelipwa mara tatu kwa siku zilezile na wapo dodoma ila Wana malipo ya safari nie ya Dodoma. Waidhinishaji wa fedha hizi ni wateule wako.

Je, wamekuelewa unataka Nini?

Umofia kwenu
 
Halafu utasikia watubutu wanakwambia eti ^Kazi iendelee!^ Au ya ufisadi na rushwa!???
 
Ni kweli, maafisa wa ngazi za juu pamoja na magari ya ofisi na madereva wao wana tabia ya kujitenegezea safari nje ya kituo chao cha kazi yaani Dodoma. Tabia hii ilianza kutamalaki baada ya kwisha uchaguzi!!. Kwa sasa sio siri tena, viongozi wengi wanaopaswa kuwa Dodoma wanakuwa Dar mwishoni mwa wiki. 🧐
 
Nikuombe bila kutumbua omba taarifa ya kila wizara wamefanya vikao vya kazi au semina ngapi kwa mei na Juni na majina ya washiriki. Utagundua wapo watu wamelipwa mara tatu kwa siku zilezile na wapo dodoma ila Wana malipo ya safari nie ya Dodoma. Waidhinishaji wa fedha hizi Ni wateule wako. Je, wamekuelewa unataka Nini?

Umofia kwenu
Kaamua kuwarejeshea tabasamu. Wamemuelewa sana.
 
Wacha watu wale aisee kama pesa ipo acheni kabisa.
 
Hao ndio local investors mkuu,

Wanasaidia kuchangamsha uchumi,

Huo sio ufisadi,

Ufisadi ulikua awamu ya Tano tu refer ropoti ya CAG.

Ripoti ya CAG ijayo hutasikia mambo kama haya.
 
Acha waptu wapige pesa tena hela yenyewe ni 120000 kwa mtu mmoja, wabunge wanalipana 340000 kwa siku x 90 + 12M salary per moon huku kazi kubwa ni kugonga meza, mtumishi wa umma anafanya kazi kubwa sn maana ndiyo mpishi.
 
Back
Top Bottom