Rais Samia futa kabisa kitu kinachoitwa Polisi jamii

Rais Samia futa kabisa kitu kinachoitwa Polisi jamii

Nakumbuka kuna askari kata mmoja alianzisha sungusungu kijijini kwetu hakika nilimgomea nilimwambia mimi ni mlipa Kodi nina TIN number kwahiyo hayo mambo ya kipuuzi mimi sitaki njoeni mulinde wenyewe.Swali langu ni je nikiumizwa huko kwenye kulinda nani atawajibika na majeraha yangu?
Eti askari kata jamaa una dharau sana...

Kitu kinachoitwa polisi tu ni kimelaaniwa.. PGO Yao hawaijui,mgambo atajuaje majukumu yake ikiwa msimamizi wake tu nae ni bichwa maji
 
Walioanzisha hiki kitu kinachoitwa polisi jamii walikusudia mema lakini implementation yake zero.

Hakuna fungu linalotoka wizara ya mambo ya ndani au jeshi la polisi kwaajili ya posho na mishahara ya vijana wa polisi jamii.

Inawezekanaje mtu ambaye hana mshahara au posho maalumu aruhusiwe kumfanyia mtu arresting?

Inawezekanaje mtu ambaye hana mshahara wala posho maalumu aruhusiwe kishinda kituo cha polisi na kufanya majukumu ya kipolisi?

Akiharibu ataripotiwa kwa nani?

Nani mwajiri wake?

Mwezi uliopita Jirani yangu polisi jamii alikwenda kufanya operation haramu na wenzake 2 jumla wakawa watatu.
Katika kurupushani na wabeba mkaa polisi jamii mmoja akauwawa kwa kucharangwa mapanga kama Kuni. Akazikwa na familia yake kimyakimya. Kwa wanaofanya habari za uchunguzi nitawapa ushirikiano.
Hii imetokea maeneo ya mpakani mwa Pwani na Dar es salaam lakini hawa vijana 3 ni wakazi wa Dar es salaam ila wanahangahika mpaka Pwani. Wanashirikiana na baadhi ya polisi wa Chanika na Mvuti

Hawa polisi jamii wana upuuzi mwingi sana. They are unprofessional, mafunzo mafupi tu wanajiita polisi .
Tusiruhusu kuwa na vyombo vingi vya ulinzi. Ni ushamba na kufungua milango ya uhalifu
Wengine wanakaa barabarani kuvizia boda boda wanaweza kumrukia boda utafiri huyo boda ameua labda kumbe wanataka elfu 5 tu ya rushwa..wapo hapo firee..na kariakoo sanasana.
 
Haoo ni kuuwawa tuu ***** zao police wafanye kazi gani etyy polisi jamiii mbona kenya huku hakuna huoo ujinga
tangu lini umehamia kenya wewe? Wewe si ni jirani yangu kabisa hapa setumbi mbeya?
 
Kuna mmoja alipigwa mpaka kuvunjwa taya maeneo ya TAZARA (Mfugale). Traffic walikuwa wamekaa kwenye kibanda halafu wanawatuma hao Polisi Jamii wakamate magari na pikipiki zinazopita Service Road.

Jamaa bila kuuliza alienda kuvamia pikipiki ya mtu (sio bodaboda) nadhani ilikuwa Yamaha au BMW, na kuchomoa funguo bila ya taarifa.

Mwenye bike aliipaki vizuri na kuanza kumshushia kipondo jamaa. Walipokuja wenzie pamoja na traffic jamaa alishachezea knuckles kadhaa takatifu.

Mwenye pikipiki alianzisha madai hapo hapo kuwa jamaa kamvamia hivyo kamchukulia ni jambazi sababu hakuwa na uniform wala kujitambulisha, kamuharibia computer system ya pikipiki yake kutokana na kuchomoa funguo kwa nguvu bila kuzima na kapoteza simu yake iliyokuwa mbele ya pikipiki karibia na ignition.

Sijui waliishia wapi ila kwa dalili zilizopo walitozwa malipo maana mwenye pikipiki mbali ya kuwa mpigaji mzuri, alikuwa akijua sheria na haki zake.

Kwa kifupi Polisi Jamii ni vibaka waliopewa baraka zote na Polisi Tanzania.

Hongera kwa kupewa haki yake huyo sungusungu mavi.
 
Back
Top Bottom