Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Lile jambo lilifanyika kwa kukurupuka sana. Wakati huo wanasiasa wetu hawa wa Afrika Mashariki walitaka kuleta mpasuko na uadui.
 
Ujumbe wangu ni kwamba Samia ni mnafiki na anafikiri kuwa kila mtu ni mjinga kama wewe.Yeye alikuwa ni makamu wa Rais kipindi vifaranga vinachomwa moto,ametuambia kuwa alifanya jitihadha gani yeye kama makamu wa Rais kipindi hicho ili kuokoa vifaranga visichomwe moto?

ana target yake usimcheke,kuna mbulumundu kibao wameanza kukatika viuno baada ya hii kauli yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787]ndio hao aliwarenga.
 
Mbona hata marehemu ilikuwa ndo tabia yake kuwashusha wenzake waliopita.

Yeye alidiriki kusema waliopita hawajafanya chochote zaidi ya ufisadi na akawataka wakae kimya.

Leo anapimiwa sawa na alivyowapimia wenzake.

Ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa upanga.

sio uongo kwamba aliyepita kabla yake alikuwa anasafiri tu!!!!
 
Hv kweli sahivi mtu alete bati za 15,000 nisimpongeze nianze kuwaza kulinda viwanda vya ndani? Hv faida kiwanda kinachopata wananigawia nile na wanangu? Bora vife tu sio kwa kututesa huko. Kama viwanda vya sukari havizalishu sukari ya kukidhi mahutaji ya nchi kwa hiyo tusiagize sukari kutoka nje?
 
Katika kongamano la biashara lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambalo limehusisha viongozi wawili wakubwa ambao ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema kwamba hakukuwa na haja ya kuchoma vifaranga waliokamatwa nchini Tanzania kutoka nchi jirani.

Amesema pia kuna kipindi ilitokea pia Sukari kutoka nchi ya Uganda iligomewa na wafanya biashara kutoka Tanzania, hivyo amemueleza Rais Museven kwamba hivi sasa Sukari kutoka Uganda itanunuliwa na wafanyabiashara wa Tanzania!

Amehimiza pia kwamba vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili viondolewe!

Hayo yamesemwa wakati Kongamano hilo likifungwa.
Huu ni ushahidi nchi inaanza kuelewa maana ya ujirani mwema na soko huria
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amesifu ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki na kusema tulikuwa tunachomeana kuku mipakani, dhambi tupu viumbe wa Mungu tunamwaga petrol kuwachoma haikuwa na maana.

Rais Samia amesema hayo katika kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.

Chanzo: Swahili times
 
Kuumbuana namna hii wala sio poa aisee...

Amesema " That Was Nonsense"...wakati yeye alikuwa Makamu wa Rais.

Kumbe naamini zile tetesi Mama alikuwa hakubaliani kabisa na Dictator.

Lakini yote hii ni likatiba letu la hovyo..yani hata Makamu anashindwa mshauri Rais.

Huu ni umakolo. Tunahitaji katiba mpya aisee.

Hizi ni aibu kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom