Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Lile jambo lilifanyika kwa kukurupuka sana. Wakati huo wanasiasa wetu hawa wa Afrika Mashariki walitaka kuleta mpasuko na uadui.
 

ana target yake usimcheke,kuna mbulumundu kibao wameanza kukatika viuno baada ya hii kauli yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787]ndio hao aliwarenga.
 

sio uongo kwamba aliyepita kabla yake alikuwa anasafiri tu!!!!
 
Hv kweli sahivi mtu alete bati za 15,000 nisimpongeze nianze kuwaza kulinda viwanda vya ndani? Hv faida kiwanda kinachopata wananigawia nile na wanangu? Bora vife tu sio kwa kututesa huko. Kama viwanda vya sukari havizalishu sukari ya kukidhi mahutaji ya nchi kwa hiyo tusiagize sukari kutoka nje?
 
Huu ni ushahidi nchi inaanza kuelewa maana ya ujirani mwema na soko huria
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amesifu ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki na kusema tulikuwa tunachomeana kuku mipakani, dhambi tupu viumbe wa Mungu tunamwaga petrol kuwachoma haikuwa na maana.

Rais Samia amesema hayo katika kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.

Chanzo: Swahili times
 
Kuumbuana namna hii wala sio poa aisee...

Amesema " That Was Nonsense"...wakati yeye alikuwa Makamu wa Rais.

Kumbe naamini zile tetesi Mama alikuwa hakubaliani kabisa na Dictator.

Lakini yote hii ni likatiba letu la hovyo..yani hata Makamu anashindwa mshauri Rais.

Huu ni umakolo. Tunahitaji katiba mpya aisee.

Hizi ni aibu kwa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…