SI KWELI Rais Samia hakupokelewa vyema ( leo) alipokwenda kuhani nyumbani kwa Julie Manning

SI KWELI Rais Samia hakupokelewa vyema ( leo) alipokwenda kuhani nyumbani kwa Julie Manning

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1

Screenshot 2026-03-21 163149.png
 
Tunachokijua
Kipande hiko cha video kinachoonesha kundi la watu wakiufukuza msafara, kimekuwa kikisambaa katika nyakati tofauti kwenye mitandao ya kijamii na kuelezwa kuwa ni msafara wa baadhi ya viongozi wa Tanzania wakifukuzwa na wananchi.

Madai

Machi 21, 2026 kupitia mtandao wa Youube chaneli moja kupitia mtandao huo ilichapisha tena video hiyo na kuweka kichwa kinachosomeka:

"B🅰️LAA‼️RAIS SAMIA SULUHU AFUKUZWA KWA MAANDALIZI YA MAZISHI YA MAMA JULIE MANNING"

Video hiyo imeunganishwa na simulizi ya mwanamke anayesikika akieleza zaidi kwa kuihusisha video hiyo na msafara wa Rais Samia kwenye mazishi ya Jaji Julie Manning alipokwenda kuhani.

Msiba wa Jaji julie Manning

Machi 20, 2026 kupitia vyanzo mbalimbali ilitangazwa kuwa Jaji Mstaafu na mwanafunzi pekee wa kike katika kundi la kwanza la wafunzi wa kwanza wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) amefariki dunia.

Rais Samia na msiba wa Jaji Julie Manning

Baada ya msiba huo kutangazwa Machi 20, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alituma salamu zake za rambi rambi kupitia mitandao yake ya kijamii ikiwemo X kwa kuelezea masikitiko yake juu ya msiba huo.

Uhalisia wa video inayodaiwa ni msafara wa Rais Samia.

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa video inayosambaa si ya mwaka 2026 lakini pia si ya tukio la nchini Tanzania.

Video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia Septemba 5, 2021 ambapo ilihusu wananchi wa Kenya kuufukuza msafari wa aliyekuwa Naibu wa Rais wa Kenya Dr. William Samoei Ruto.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha video hiyo Septemba 5, 2021 ikiambatana na ujumbe:

"Wanasiasa kama Rigathi Gachagua, Ngirici na Kang’ata hawakuweza kuhamasisha watu kumuunga mkono Naibu Rais Ruto. Ameonekana kuzomewa huko Kieni. Inaonekana Ruto anaweza kubaki na uungwaji mkono mkubwa katika eneo la Rift Valley la Wakalenjin pekee. Huu ni ukweli ambao wasaidizi wake kama Murkomen wanapaswa kuutambua."

Tovuti ya Tuiko ya nchini Kenya ilichapisha pia taarifa kuhusiana na tukio hilo na miongoni mwa sehemu ya taarifa hiyo ni:

"Msafara wa Naibu Rais William Ruto uliokuwa ukielekea Kieni kwa ibada ya kanisani ulikumbana na upinzani Jumapili, Septemba 5, baada ya kundi la vijana kuwazomea wakiwa kando ya barabara."

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa hakuna taarifa yoyote inayothibitisha kuwa Rais Samia alihudhuria msiba wa Julie Manning. Machi 20, 2026 Rais Samia alishiriki swala ya Eid na kisha baadaye kwenye baraza la Eid.
Walienda kupima upepo haaa haaa kama ni kweli hiki kilichotokea mama andelee jificha tu ndani aisije kutana na wafiwa wa octoba 29 wakampiga mawe
 
Huu nao ni uzi eti.

Kama hukufa tarehe 29 wewe pia mnafiki maana ulijifungia ndani uendelee kula ugali.
 
Alikwenda bila kujua msimamo wa marehemu Jaji, tofauti yake na marehemu, marehemu alipata nafasi kwa uwezo na sio gender.
Marehemu kama mpenda haki inawezekana alilaumu hatua alizochukua za kuua watu.
 
Watu kama hawa wakibanwa wanalalamika vyombo vya habari haviko huru...
 
Back
Top Bottom