Rais Samia hana mchezo wala subira kwa atakayechezea fedha za umma

Rais Samia hana mchezo wala subira kwa atakayechezea fedha za umma

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Rais Samia anahangaika huku na kule kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo, anahangaika kila mahali kutafuta wawekezaji , anashindwa kupata hata muda wa kupumzika na Familia ili kuona watanzania wanapata huduma Bora na karibu kabisa ya makazi yao, anasafiri huku na kule kutafuta fursa za kibiashara kwa Taifa letu, anahangaika usiku na mchana kuona maisha ya mtanzania yanabadilika na kuwa Bora kila kukicha

Anafanya hayo yote kwa kutambua Hali ya kiuchumi ya watanzania, anafanya hayo ili mgonjwa akienda hospitalini apate huduma Bora na kwa wakati, akute madakitari,vifaa Tiba na dawa za kila aina, Anataka mwanafunzi anayetoka familia maskini awe na uhakika wa kusonga mbele kielimu akifaulu, anataka mwanafunzi akimaliza kidato Cha sita apate mkopo wa elimu ya juu, anataka wakulima wapate pembejeo kwa Bei nafuu, anataka huduma za maji na umeme ziwe za uhakika na kufika kila mahali ili kufungua fursa za ajira kwa vijana

Anataka kuona vijana wanapata fursa za ajira na kuajirika, anataka kuona vijana wanakopeshwa kupitia Halimashauri zao ili waweze kupata mitaji ya kuwekeza katika shughuli za kiuchumi zitakazo wapunguzia utegemezi na umaskini wa kipato, anataka kuona akina mama wanawezeshwa ili kuchangia katika maendeleo ya familia na kuondoa utegemezi kwa Waume zao, anataka kuona kila mtu ana faidika na jasho lake, anataka kuona Kiwango Cha umaskini kikipungua katika nchi yetu

Rais Samia anatambua namna watanzania wanavyohangaika kuijenga nchi yao, anatambua namna wanavyojinyima kulipa Tozo , ushuru na Kodi mbalimbali kuijenga nchi yao kwa mikono yao wenyewe, anatambua namna vijana wanavyohangaika huku na huku kutafuta vibarua ili kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha

Hivyo Rais Samia hawezi kukubali mtu au watu au kikundi kinachoweza kuchezea fedha za umma, Hawezi kumvumilia kiongozi au mtumishi wa umma atakaye fuja fedha za umma ,hawezi kumwonea haya au aibu mtu atakayechota fedha za umma na kuweka mfukoni mwake, hata mpa nafasi ya pili kwa mtu atakaye shindwa kutambua kuwa uongozi Ni utumishi kwa watu na hawezi kuhangaika kutafuta fedha kuja kujenga nchi yetu halafu mwingine afanye kazi ya kuzichota kwa manufaa yake binafsi

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono na kumwamini Rais wetu mpendwa, Tuendelee kumpa ushirikiano, Tuendelee kumshauri kwa staha heshima na busara, Rais wetu Ni msikivu Sana kwetu watanzania, Rais wetu anayo dhamira njema na uchungu mkubwa Sana na nchi yetu, Rais wetu anatamani kuona sisi vijana na watanzania wote kwa ujumla tukiondoka katika Hali ya umasikini wa kipato, Anataka kuona hakuna mtanzania anayelia kwa kuonewa na kulala na njaa kwa kukosa chakula

Rai yangu kwa viongozi na watumishi wa umma mliopata bahati ya kuwa sehemu ya serikali, mtambue kuwa uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo mmepata bahati ya kuwatumikia watanzania wanyonge wanaohitaji huduma Bora kutoka kwenu, Tambueni uongozi ni dhamana mnayopaswa kuitumia kuwafuta machozi na kuwatua mizigo watanzania,Tendeni haki kwa haki,

Tangulizeni mbele maslahi ya umma, ondoeni Tamaa Binafsi muwapo makazini kwenu, Rizikeni na kile mkipatacho kwa kutambua kuwa huku mtaani Kuna vijana wanatamani wangefanya kazi hata wangepata nafasi ya kujitolea tu, Tambueni kuwa mmepata bahati ya kipekeee Kati ya mamillioni ya watanzania wenye sifa Kama zenu au kuwazidi. Mwisho Tambueni kuwa kiongozi haimaanishi kuwa mna akili kuliko watanzania wote wasio katika uongozi ,Hivyo kuweni wasikivu, wanyenyekevu,wavumilivu,wakalimu na wenye upendo kwa watu wote wanaohitaji na kuja katika ofisi zenu kupata huduma

Kazi iendeleee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Rais Samia Ni kiongozi Bora kabisa aliyepo kwa Sasa katika viongozi wote wa Afrika , Nadhani umesikia huko kwingine badala ya kuwaza maendeleo wanawaza namna ya kubadili katiba zao ili waendelee kutawala kwa muda mrefu

Kama mtu anatawala miaka mia na maendeleo yapo na Maisha mazuri kuna shida gani?
 
Kama mtu anatawala miaka mia na maendeleo yapo na Maisha mazuri kuna shida gani?
Kiongozi mzuri Ni Yule anayeweza kutengeneza viongozi wengine aina yake, Kama Ni hivyo Obam angekuwa bado yupo madarakani mpaka Sasa maana alikuwa anakubalika bado na wamarekani
 
Kwani zile bilioni 350 mgao haukumfikia?
 
Wana wanapigia hadi masterb..
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
 
RIPOTI ya CAG imewataja Wapigaji wa Fedha za Umma hakuna Hatua zozote zinazochukuliwa ni SIASA TU
 
Lucas kama ungeitoa hoja hii wakati ule wa utawala wa JPM ningeweza kusema unafanya hivyo pengine kutokana na uficho mkubwa wa habari uliokuwepo katika "public domain" katika nyakati hizo.

Lakini kwa sasa ninakushangaa, yaani husikilizi hata malalamiko ya wabunge wa chama chako wanapoongea kwa uwazi pale wawapo bungeni!

Lucas, Lucas, Lucas!?

Jaribu kuwa hata mkweli kwa nafsi yako wewe mwenyewe, na kwa dhamira njema moyoni mwako wewe mwenyewe.
 
Rais Samia Ni kiongozi Bora kabisa aliyepo kwa Sasa katika viongozi wote wa Afrika , Nadhani umesikia huko kwingine badala ya kuwaza maendeleo wanawaza namna ya kubadili katiba zao ili waendelee kutawala kwa muda mrefu

Hapa inatakiwa machafuko ili hiki chama cha majizi kitoke ili nchi yetu iianze upya kiutawala.
 
Hapa inatakiwa machafuko ili hiki chama cha majizi kitoke ili nchi yetu iianze upya kiutawala.
Hakuna machafuko Wala wakuleta machafuko maana serikali ya CCM chini ya Rais Samia haina mchezo na wabadhirifu wa fedha za umma, Ni serikali sikivu ndio maana wananchi Wana imani na matumaini na serikali hii na wanaamini Hakuna atakayebakia salama endapo atabainika kugusa pesa zao
 
Lucas kama ungeitoa hoja hii wakati ule wa utawala wa JPM ningeweza kusema unafanya hivyo pengine kutokana na uficho mkubwa wa habari uliokuwepo katika "public domain" katika nyakati hizo.

Lakini kwa sasa ninakushangaa, yaani husikilizi hata malalamiko ya wabunge wa chama chako wanapoongea kwa uwazi pale wawapo bungeni!

Lucas, Lucas, Lucas!?
Jaribu kuwa hata mkweli kwa nafsi yako wewe mwenyewe, na kwa dhamira njema moyoni mwako wewe mwenyewe.
Amini Nakwambia hakuna atakayebakia salama na kusalimika ikiwa atabainika kufuja pesa zetu, uwe na subira utaona Moto utakao wawakia, hakika watajuta
 
Back
Top Bottom