Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Wakati Watanzania wanajiandaa kwa shauku kubwa kuishi ndani ya utawala wa Rais wa JMT ambaye ametokea kuwa mwanamke, kuna majadiliano mengi yanaendelea huku na huko.
Baadhi ya majadiliano haya nayaona yana mantiki sana ila sitaenda kuyagusia kwa sasa.
Mimi nitaongelea suala la majina ya Marais wetu. Herufi zina maana sana katika kusoma alama za kiroho na hata kubashiri siku za baadae.
Samia Suluhu Hassan ni Rais wa kwanza wa JMT ambaye katika majina yake yote, hakuna jina lake hata moja ambalo linaanza na herufi moja kati ya J au M.
Marais wote waliopita, mojawapo ya majina yao la kwanza au la mwisho yalianza na J au M, huku watatu walikuwa na jina la kwanza linaanza na J na watatu walikuwa na jina la mwisho linaanza na M. Rais Samia ni wa kwanza kuvunja hii trend.
Julius Kambarage Nyerere
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin William Mkapa
Jakaya Mrisho Kikwete
John Pombe Magufuli
Samia Suluhu Hassan
Hii ina maana gani?
Mimi siyo mnajimu ila naweza kusema inaweza kuwa na maana moja kubwa. Kwanza Tanzania ya Rais Samia itakuwa tofauti sana kiuchumi, kijamii na kisiasa kuliko awamu zote zilizopita. Ni kipindi ambacho tunaweza kuona vitu vingi tulivyoona ni mazoea ya Mtanzania vikibadilika sana. Ni kipindi cha mabadiliko ya kweli na ya msingi.
Binafsi, niko 'excited' sana. Kawaida mabadiliko yanatisha ila ndiyo msingi wa maendeleo. Karl Marx alisema msuguano na migongano kati ya matabaka ndiyo chachu ya mabadiliko.
Labda wengine sijui mnaonaje kuhusu suala hili?