Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rais Samia amesema Tunaishi katika zama za mataifa kukubaliana katika biashara na kwa kiasi kikubwa kupungua kwa misaada.
"Tunaishi katika zama za mataifa kukubaliana katika biashara na kwa kiasi kikubwa kupungua kwa misaada. Tunaishi kwenye zama za kuongezeka kwa masharti ya mikopo. Wakati huo huo kuna ongezeko la mahitaji ya wananchi. Kwa msingi huo, hatuna budi kujenga uwezo wetu wa ndani kwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kujenga uchumi unaojitegemea kwa kiasi kikubwa.
Soma Pia: Rais Samia: Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka
Hatutaweza kwenda 100% kujitegemea lakini kwa kiasi kikubwa tunaweza kujitegemea kwa mapato yetu ya ndani. Kwa mantiki hiyo, kodi hizi tunazokusanya sambamba na vyanzo vingine vya mapato ya serikali ndizo zitazotuwezesha kuendelea kuendesha huduma za jamii na kwa kiasi fulani kutekeleza miradi ya maendeleo nchini. Katika mnasaba huo, nadhubutu