Rais Samia hawezi kushinda urais 2025 kirahisi kama Wakurugenzi na Tume ya Uchaguzi watadhibitiwa

Tusidanganywe na wanasiasa wanaotafuta vyeo, urais hawatougusa, miaka 3 inatosha, tukianzia ilipoishia Katiba chini ya Warioba. 2026 tutapata KATIBA mpya. Amen
 
Wakosee iwepo katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, hata kama mama atashinda, kwanza atashinda kwa margin ndogo, na huko bungeni ni wazi atakosa 2/3 ya kuifanya CCM iamue chochote itakacho.
Kwenye wabunge nakubali wabunge wengi sana wa CCM watatoka ila kwenye uraisi bado sijaona kama opposition wapo serious sana
 
Mi huwa najiuliza, siku mwenyekiti wa Tume akimtangaza mtu ambaye hakugombea kabisa sijui itakuwaje? Maana akishatangaza hakuna wa kupinga chini ya katiba hii. Mathalani akimtangaza mke wake ama mtoto wake kuwa ndiye Rais, itakuwaje?
Nawasihi Kwa Jina La MUNGU Alie hai, sanduku la kura halitaleta mabadiliko chanya Kwa Watanzania Kwa sasa, KATIBA mpya kwanza, uchaguzi baadaye.AMEN
 
Lini samia alisema atashinda?
 
Rais wa Nchi Si mama Yako, pia Si mama yangu. RAIS ni kiongozi wa wananchi, HANA JINSIA, Hana DINI, HANA CHAMA Wala KABILA, ni WA Watanzania WOTE. Amen.
 
Halafu ashinde nani?

Au tutaongozwa na chama bila kiongozi mgombea?
 
Kwenye wabunge nakubali wabunge wengi sana wa CCM watatoka ila kwenye uraisi bado sijaona kama opposition wapo serious sana

Ukishapoteza wabunge wengi unapoteza nguvu ya maamuzi kama utakavyo. Baada ya hapo ni uchaguzi unaofuata ndio mnafunga safari.
 
Ukishapoteza wabunge wengi unapoteza nguvu ya maamuzi kama utakavyo. Baada ya hapo ni uchaguzi unaofuata ndio mnafunga safari.
bado vyama vya siasa vina kazi ngumu sana ya kujiimarisha katika ngazi ya mashina hii nchi ni kubwa sana
 
Ukishapoteza wabunge wengi unapoteza nguvu ya maamuzi kama utakavyo. Baada ya hapo ni uchaguzi unaofuata ndio mnafunga safari.
Kwa akili Yako uko tayari kuingia ktk UCHAGUZI Ili mradi upate wabunge wengi 2025 malengo ni kuwa 2030 uitoe CCM? Akili hiyo ni mfu, kauli Iko KISIASA zaidi, haiangalii maslah mapana ya nchi.

Unawaza kuja kuwa mbunge siku moja? Huwatendei HAKI wananchi. Hali hii itadumu Hadi lini?

Nani ataheshimu sanduku la kura?
 

CCM wapo mpaka huko chini sio kwa ushawishi bali ni kwasababu za kihistoria. Kwa taarifa yako hakuna chama chochote kitashindwa kuongoza nchi hii, kama kwa uelewa huu mdogo wa wabunge na madiwani wa CCM na nchi inaenda, sioni chama chochote kitashindwa kuongoza nchi. Kenya hapo KANU ilikuwa inaongopea watu hakuna chama kitaweza kuiongoza Kenya, leo yako wapi?

Hao CDM walikuwa nao wanafanya kazi za siasa nchi nzima, na kila kitongoji wapo, Magufuli akaanza siasa za ulevi wa madaraka kuwa huruhusiwi kufanya siasa kama hujachaguliwa eneo hilo, na bado hata wapinzani waliochaguliwa wakawa wanafanyiwa mizengwe. Ilitakiwa kusiwe na katazo hili ili haya unayoyasema uyapime vizuri.

Yaani CCM ilitakiwa ipate wanachama na wafuasi kwa ridhaa yao kama zilivyo timu za simba na yanga, na sio kutumia vyombo vya dola kuzuia wengine kufanya siasa, na wakati wa uchaguzi bado tuone mabox ya kura yakiletwa na polisi, huku wakurugenzi wakitangaza kinyume na machaguo halisi ya wananchi. Hapo ungeweza kunishawishi kuwa CCM inakubalika kama unavyotamani iwe.
 
Chama kikuu Cha upinzani kikigomea uchaguzi, uchaguzi hautofanyika. Katiba mpya ni muhimu kuliko UCHAGUZI wenyewe. Ni Kwa maslah mapana ya nchi.
 
bado vyama vya siasa vina kazi ngumu sana ya kujiimarisha katika ngazi ya mashina hii nchi ni kubwa sana

Huhitaji kujiimarisha sana kwenye matawi kama unavyosema ndio ushinde uchaguzi, sasa hivi watu wanapata taarifa kwa urahisi sana sio kama ilivyokuwa huko nyuma. Ingekuwa nchi yetu watu wanachagua kwa sera hapo wangalau, lakini watu wanachagua kwa hamasa, sura, rushwa, vitisho nk. Hata ukienda hasa huko vijijini watu wanaongozwa kwa miongozo ya watendaji wa serikali zaidi kuliko ya viongozi wa vyama. Mfano mrahisi watu wengi hawawajui mabolozi wa nyumba 10 ambao wote ni wa CCM, bali huwajua zaidi watendaji wa serikali. Maamuzi au ushawishi ambao ungeweza kufanywa na balozi, unaweza kufanywa na mtu yoyote mwenye ushawishi eneo husika.
 
Chama kikuu Cha upinzani kikigomea uchaguzi, uchaguzi hautofanyika. Katiba mpya ni muhimu kuliko UCHAGUZI wenyewe. Ni Kwa maslah mapana ya nchi.

Kwa taarifa yako CCM wanataka CDM isisue uchaguzi ili ipite kirahisi maana imechoka kushindina, na inaona aibu kushindwa na cdm. Ni kweli idadi ndogo ya wapiga kura haiwafurahishi ccm, lakini kwakuwa wanaendelea kukaa madarakani wanakomaa hivyo hivyo. Hivyo CDM wakigomea uchaguzi ni sherehe kwao, maana watakuwa na vyama vyao mapandikizi ili kutakatishia huo uchaguzi.

Kwa katiba hii ilivyo uchaguzi una maslahi kwa CCM zaidi, wakishaingia madarakani ndio wanaanza kuhubiri maslahi ya taifa. Kwao uchaguzi sio maslahi ya taifa bali ya chama. Maslahi ya taifa watayahubiri wakishakaa kwenye mzinga wa asali.
 
Wewe unatumia ubongo gani kufikiri? Mbona unakariri mambo ya kiboya? Wapiga kura wataongezeka na kuwa wengi ili kumuadhibu huyu mama anayejiita mkamua tozo wananchi wa kawaida.

Nani anaogopa box la kura boss? Uhayawani aliopandikiza Magufuli kwenye chaguzi zetu, hakuna kiongozi wa ccm ataacha kutumia mbinu ile. Na vile siku hizi hata wazungu hawaingilii hizi chaguzi zetu za kishenzi, labda yatokee machafuko na sio box la kura.
 
Acheni kuota ndoto za mchana. Yaani yeye ndo anateua hao wakurugenzi wa uchaguzi halafu tena asishinde? Rais Kikwete alishawahi pangua hiyo tume ya uchaguzi karibia kabisa na uchaguzi wa 2015. Bila tume huru ya uchaguzi hakuna mgombea wa CCM ambaye atashindwa uchaguzi wa urais.
 
CCM si wajinga kihivyo wanajua wakimwangusha Samia na wao ndo byebye kutawala maana watz watakaoongozwa na chama kingine ule msemo wa wapinzani wakitawala vita itatokea watagundua ulikuwa ni ujanja tu maana hako nako kamekuwa kakichaka ka ccm kujificha kuwahadaa wajinga ambao ni wengi Tz

Hata kwa sasa sijaona Samia kafanyeje maisha ya watz yawe magumu ,mimi nakwenda Kenya mara nyingi hali ni ngumu huko wanadai Kenyata atoke tu , sasa Samia ndiye anaongoza Kenya?

Vitu vimepanda bei ndiyo inayoonekana ni gia ya wakosoaji na sababu zipo wazi tu Samia hawezi kuzizuia ,ushauri wangu kwa wanaomkosoa Mama wawe wanakuja na hoja za msingi ,na wakumbuke watz wengi hawajui vema siasa za nchi yao ndiyo maana hawawezi kureason critically na mwisho utaona tu Samia ana shinda kwa kishindo tu
 
Mimi kura yangu anayo muhimu niwe hai na yeye mzima na hai na ateuliwe kugombea kwangu amefanya poa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…